rodrick alexander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 15,150
- 20,054
Kama mikopo ya wahisani nina riba kubwa kubwa na ule wizi unaofanyika kkwenye fedha za umma wahisani pia wanahusika?
Uchumi unapokuwa mzuri, ndipo mapato ya serikali nayo yanaongezeka. Kwani si ndiyo tulishawahi kuwa na kodi ya kichwa kabisa? Pesa zilienda wapi? Wananchi wanalalamikia matumizi makubwa ya viongozi kuanzia mishahara na maviete. Lakini badala yake hao viongozi ndiyo wanabuni mbinu kandamizi kabisa za kuzidi kumfukarisha mwananchi wa kawaida.WaTanzania tuache tabia ya kupenda kuwa Tegemezi. Hakuna mtu anayemthamini masikini, hasa masikini asiyekuwa na ndoto ya kujikomboa katika hali yake. Wenyewe mmesikia mahela yaliyokusanywa kipindi hiki kifupi cha tozo za miamala ya simu. Tukijipanga tunaweza sio kusubiri hela za wafadhili tu, ambazo zinatolewa na masharti mengi - kama vile haki za mashoga nakadhalika. Marehemu JPM alisema mara nyingi - nchi hii siyo maskini. Serikali ikijipanga vizuri , matumizi mazuri ya pesa za serikali na kila mtanzania kulipa kodi- tutafika mbali. Nchi kama Denmark- wananchi wao wanalipa kodi kwa asilimia kubwa sana. Hapa kwetu ni asilimia ndogo sana ambao wanalipa kodi stahiki.
Sema nini Rais na Serikali iwaeleze watu uwazi kwamba nchi ikishakuwa uchumi wa kati ni kama mtoto ameshakua lazima kujitegemea.Hayo ndo madhara ya uchumi wa Kati.
"WATANZANIA TUACHE TABIA YA KUPENDA KUWA TEGEMEZI"WaTanzania tuache tabia ya kupenda kuwa Tegemezi. Hakuna mtu anayemthamini masikini, hasa masikini asiyekuwa na ndoto ya kujikomboa katika hali yake. Wenyewe mmesikia mahela yaliyokusanywa kipindi hiki kifupi cha tozo za miamala ya simu. Tukijipanga tunaweza sio kusubiri hela za wafadhili tu, ambazo zinatolewa na masharti mengi - kama vile haki za mashoga nakadhalika. Marehemu JPM alisema mara nyingi - nchi hii siyo maskini. Serikali ikijipanga vizuri , matumizi mazuri ya pesa za serikali na kila mtanzania kulipa kodi- tutafika mbali. Nchi kama Denmark- wananchi wao wanalipa kodi kwa asilimia kubwa sana. Hapa kwetu ni asilimia ndogo sana ambao wanalipa kodi stahiki.
Majibu wanayo wahanga wa NSSF,watumishi miaka 5 no kupanda daraja,wafanya biashara wakubwa kufanyiwa unyang'anyi na serika ikiwa ni pamoja na serikali kuikopa mifuko karibu yote ya jamii.Kuna 2.3 trillion ya world Bank na 1.3 trillion ya imf kwa ajili ya corona mpo hapo ?
Hivi JPM alikua anatoa wapi hela za ujenzi wa madarasa ?
Nimeuliza tu jamani
Wewe unatakaje? Elezea kwa hoja watakusikia na kujirekebisha! Lawama tu si jibu.Kwani wale wa Danish ambao ni wahisani wakubwa kabisa wanaofunga ubalozi wao nchini walitoa sababu gani? Sidhani kama hii kauli ina ukweli. Waseme tu hawawezi kufuata demokrasia. Wahisani wana masharti ambayo wanahofia yatawapoka madaraka na hivyo kunyang’anywa tonge mdomoni.
Wanaona ni bora kuendelea kukamua ng’ombe aliyekonda na wao waendelee na ma viete yao wakitafuna keki ya Taifa kwa kupokezana.
Kwanini umeshindwa kuona kwamba hoja ni wao kushindwa ama kukataa kufuata demokrasia?Wewe unatakaje? Elezea kwa hoja watakusikia na kujirekebisha! Lawama tu si jibu.