Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,402
Rais Samia Hassan amesema kuna maradhi ambayo hayakuwepo siku za nyuma lakini yanajitokeza siku za karibuni kwa kuwa uharibifu wa misitu unasababisha Viumbe wa Msituni wasambae kwa Wanadamu
Amesema “Nilikuwa nazungumza na Waziri Mkuu juzi, ametoka ziara Mikoa ya Kusini (Lindi), ameniambia ameona maradhi mapya yameingia. Watu wanatokwa na damu za pua na wanadondoka chini”
Rais anaongeza "Hatujui ni kitu gani, Wanasayansi wamehamia huko kwa uchunguzi zaidi kwa kuwa ni Watu wengi wanaougua kwa mfululuzo, na yote ni kwa sababu tunaharibu makazi ya viumbe kule walikowekwa na Mungu. Tunawasogeza kwetu wanatuletea maradhi”
Rais Samia amezungumza hayo leo, Julai 12, 2022 katika Maadhimisho ya Mkutano wa 20 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki ya Afrika Mashariki (AMECEA)