chazachaza
JF-Expert Member
- Feb 21, 2018
- 2,829
- 3,824
Yaani huyu bibi daaah, yaani hapo aliposema hapo kwenye hiyo hazara ndo amemaliza !!,hakuna hatua yeyote atakayochukua!!. ukweli ni kwamba ,tunayemuona kwa macho sie ,Ila aliyefichama ndiye!!
Inawezekana ni kujikosha tu ila na yeye yumo. Umesahau ya awamu ya nne?Aache kulalamika lalamika anashindwa kutoa maamuzi amebaki kulialia
Suala muhimu ni kuchukua hatua stahiki. Wahusika ama watuhumiwa wanapaswa kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi. Wizi wa namna hiyo siku zote huwa ni wa kimfumo kwa kuwa unahusisha watu wengi wenye mamlaka ya kuridhia na kuidhinisha hatua moja ifanyike kabla ya kwenda kwenye nyingine inayofuata."...ninazo taarifa za hivi karibuni wafanyakazi wasio waaminifu wamechezea mifumo na kuonyesha mizigo imelipiwa Bandarini na kuruhusiwa kuondolewa ilhali malipo hayajafanyika." Amesema Rais Samia.
My take;
Je, ni rasmi upigaji umerejea kwa kasi namna ile?!
Je, wenye dhamana za uongozi katika taasisi husika hawapaswi kuwajibishwa kwalo?!
Watendaji walio chini ya mkurugenzi wa Bandari wanachezea mifumo na yeye yupo ofisini wa kazi gani?!
Kamishina wa TRA bado yupo ofisini kwa sifa zipi kama ubadhirifu wa kuchezewa mifumo namna ile unafanywa na vijana wake?
Rais analalamikia ilhali yeye ndiye mwenye uwezo wa kuchukua hatua je mimi mlima pareto huku polini nifanyeje?
Inafikirisha!
Huyo ni mpumbavu na hiyo ndiyo sifa za wapumbavu ,unalalamika maji ayafunguliwi wakati funguo za kufungulia maji umezishika weweFull kulalamika kila siku wakati taarifa anazo kinacho mshinda kuchukua hatua ni kitu gani ?