tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 18,362
- 12,380
Naingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kumchosha mtu yeyote. Nawapongeza Baraza la Mitihani (NECTA) kwa kufanya kazi nzuri ya kufichua uovu uliofanywa na Shule ya Chalinze Islamic Modern School kuwabadilishia wanafunzi 7 namba za mitihani kwa sababu wanazozijua wao wenyewe.
Lakini nasikitika kusema kwamba kazi hii nzuri iliyofanywa na NECTA kufichua uovu imetiwa shubiri na waziri wa elimu Adolf Mkenda kwa kutoa adhabu ndogo sana kwa wahusika waliotaka kuharibu mustakabali wa maisha ya mabinti wadogo wasiokuwa na hatia.
Nilitegemea Mkenda aifutilie mbali shule hii badala yake ametoa adhabu ya kufungia kituo cha mitihani. Adhabu hii ni sawa na bure kwani kufuta kituo cha mitihani huku wanafunzi wa shule hiyo wakipangiwa kituo kingine cha kufanyia mitihani hakuwezi kuwazuia kuendelea na mchezo wao wa kubadilisha namba za mitihani za wanafunzi. Suluhisho la kudumu ni kuifungia shule moja kwa moja isiendelee kutoa elimu ili liwe fundisho mujarabu kwa wahalifu wengine wanaofanya mchezo huu usiofaa.
Watoto hao waliobadilshiwa namba za mitihani wangeonekana wamefeli maisha yao yangewaribikia wakati hawana hatia yoyote. Inauma sana. Nashauri viongozi wa kiislamu waingilie kati wamlazimishe mumiliki wa shule aondoke neno Islamic kwenye jina la shule anautia aibu uislamu na kuonea watoto waislamu wenye akili kama hao wasichana wa kiislamu waliowabadilishia namba.
Kumekuwa na tuhuma kuwa vyuo vikuu vinajaa wakristo tu kwa sababu eti waislamu wengi wanafelishwa sekondari kumbe kwenye shule zenyewe za waislamu kuna tatizo. Sasa hao vilaza waliofanyiwa mitihani na wanafunzi wenye akili isingegundulika mapema wangeenda sekondari na hao wenye akili wangebaki nyumbani. Na hao waliofanyiwa mitihani hata kidato cha sita wasingetoboa.
Mitihani ya form four (CSE) tu wangeweza kupata division zero na kuongeza idadi ya waislamu wanaopata division zero sekondari. Na kuwajengea waislamu siasa kali ni hoja zisizokuwa na mashiko kuwa waislamu wanafelishwa sekondari. Kumbe vilaza walipelekwa tu na viongozi wa shule za kiislamu wenye majina ya kiislamu wasionna hofu ya Allah wamehongwa kupitisha watoto nusu kaputi kwa kudhulumu wale wenye jitihada na wanaomlingania Allah kama huyo msichana.
USHAURI
Namshauri Mh Rais mama Samia Suluhu Hassan amfute kazi waziri wa elimu Adolf Mkenda kwa kushindwa kusimamia haki. Ameshindwa kufanya kazi yake sawasawa na pia amedhalilisha dini. Haiwezekani amchafue rais wetu nje, ndani halafu wapenda haki tukae kimya.
Kwa habari zaidi kuhusu hii skandali, soma makala zifuatazo:
Profesa Mkenda asema wanafunzi saba walibadilishiwa namba za mtihani
Shule ya Chalinze Modern Islamic yafungiwa kwa muda usiojulikana