Rais Samia: Mbowe alijificha Nairobi aliporudi akaanza harakati za madai ya Katiba, nadhani ni Calculation akijua kwamba ana kesi

MC44

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
2,170
3,269
Mahojiano na Salim Kikeke. Inaonekana Rais yupo nyuma ya hii yote. Na yoote yanayofanyika anaangalia tuu.

Anyway Leo ndo nimemjua Rais tulienae.

----
KESI DHIDI YA FREEMAN MBOWE

Kikeke:
Nazungumzia suala hilo la kisiasa kwa sababu kiongozi wa upinzania Freeman Mbowe amefikishwa Mahakamani, amefunguliwa mashataka ya Ugaidi, wananchi wake wanasema mashtaka haya yamechochewa kisiasa

Rais Samia: Mimi sidhani kama yamechochewa kisiasa kwasababu navyojua Mbowe alifunguliwa Kesi mwezi wa Tisa mwaka jana (2020), kwa hiyo yeye pamoja na wengine na kama ulivyosema mashtaka ni ugaidi na kuhujumu uchumi. Nadhani wenziwe kesi zao zimesikilizwa na wengine wameshapewa sentence zao wanatumikia. Yeye (Mbowe) upelelezi ulikuwa haujeisha, uchunguzi ulikuwa unaendelea so amekwenda amefanya tumeingia kwenye uchaguzi, amemaliza uchaguzi nadhani sasa Polisi wamekamilisha uchunguzi wao, wamemuhitaji waendelee na kazi yao, Lakini kwasababu na kama utakumbuka Mbowe hakuwepo nchini alikuwa Nairobi, sasa kwanini kakimbia sijui. Lakini alivyoingia tu nchini Kaitisha maandamano ya Katiba na madai ya katiba. Nadhani ni Calculation akijua kwamba ana kesi ya aina hiyo na hii vurugu ambayo ana-instigate akikamatwa aseme mmhh! kwasababu ya Katiba, kwasababu tumeitisha Katiba... nadhani sina hakika.

Lakini kwasababu jambo liko mahakamani, sina uhuru wa kulizungumzia kwa sana. Nadhani tuache Mahakama zioneshe ulimwengu kwamba hizo shutuma walizomshutumu zilikuwa za kweli au siyo za kweli Mahakama itaamua.
 
Polisi na CCM huwa wanasaidiana kufichiana aibu. hii kauli ya Samia na ile ya Sirro ukiangalia kwa makini utaona wote wana mtazamo unaofanana.

Kama Mbowe alijificha Nairobi waliwahi kusema? kuna Interpol kwanini hawakutangaza ili wasaidiwe kumtafuta?

Nashawishika kuamini Rais ameongea uongo, analeta propaganda kwenye haki za binadamu, kusema Mbowe alijificha Nairobi wakati muda wote alikuwa Dsm na Moshi kumzika ndugu yake ni maneno ya kisiasa tu.
 
Unaweza mtu ukajiuliza kweli huyu ni mzima kichwani? Kujificha Nairobi vipi je kama alijifungia sehemu tulivu ili apate wasaa wa kusoma katiba ya zamani vizuri ang’amue mapungufu yake ili akidai katiba mpya awe na hoja za kuipinga hiyo ya zamani?

Utoto tu vizuri azingatie kinywa chake kinatoa nini na kwa wakati gani hatupo kwenye mduara hapa hili ni taifa akumbuke yupo baba wa familia ametengwa na watu wake wa karibu.
 
Ina maana alijificha kwa kuwa alienda Nairobi, au?!

Lakini tu-assume alijificha kwa sababu kila mmoja anafahamu viongozi wa upinzani maisha yao yalikuwa hatarini!!! Sasa tatizo lipo wapi kwa yeye kudai katiba akitokea "mafichoni"?
 
Mbona kila mtu alimuona Mbowe alipokuwa Nairobi?

Na alifanya mahojiano na vyombo vya habari vya nchini Kenya.

Hebu tuleteeni taarifa nzima tujiridhishe kuwa kweli Rais amesema hiki mnachoripoti.
 
Back
Top Bottom