conservative3
JF-Expert Member
- Nov 12, 2013
- 1,116
- 762
Kuna kitu hakika Sawa.. ..km cheti cha form four kina jina linaloendana na vyeti vingine shida iko wapi wapi?
kwa kuwa aliajiliwa kwa vyeti vya huyo alieuza jina na jina jina la kazini alipaswa atumie la huyo unless akasepa mahakamani kubadili jina.
Kwa umri unaosema yaani mtu wa miaka 58 suala la vyeti vya kuzaliwa haikuwa lazima....
Kuna ambao wengi wapo wa dizain hiyo bado wanafanya kazi....

Mkuu hii story yako imenikumbusha hadithi ya Daktari bingwa mmoja wa upasuaji kule Morogoro ambaye alikumbwa na kadhia hii akiwa amebakiza miaka 2 kustaafu. Walio saidiwa wao au ndugu zao kuokolewa maisha walilia sana utadhani ni baba yao mzazi.
Huyu daktari kijijini kwao alifaulu mtoto mmoja tuu kwenda sekondari wakati huo lakini wenye mtoto walikuwa hawakutaka mtotowao akasome maana kazi za Shamba hawakuwa na mtu. Wakamuuzia mtoto mwingine nafasi.
Ndio huyo Dokta, akasoma elimu zote kwa juhudi zake hapa nchini hadi Urusi na kuwa bingwa wa upasuaji.
Kafanya kazi kwa juhudi na uadilifu mkubwa sana lakini 2 years before retirement anaonekana kuna utata kwenye majina na ni daktari fake hivyo kazi hakuna na mafao hakuna! Hata ile michango yake ya akiba ya uzeeni hakuna.
Is it fair kweli? Kaokoa maisha ya watanzania wangapi? Kwani huko alikokuwa anasoma alikuwa anasomewa na mwingine? Zoezi lile halikuwa sahihi