Rais Samia, mbolea ya ruzuku ikichelewa wakulima wa kutotegemea mvua tutapata hasara kubwa

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
11,290
17,733
Ombi kwa mheshimiwa Raisi Mama Samia.

Mpango wa mbolea ya ruzuku ni mzuri sana na wenye tija kama utatekelezwa kwa wakati. Serikali yako imesikiliza kilio cha wakulima cha muda mrefu. Hongera sana.

Pongezi pia ziwafikie washauri wako na wazira ya kilimo kwa ujumla.

Mpango huu umeanza kuwa mwiba mchungu kwa wakulima wasiotegemea mvua sababu kwa sasa tuna mazao yaliyopandwa shambani tayari ambayo yanahitaji mbolea. Ukienda kwenye maduka ya pembejeo unaambiwa mbolea hakuna sababu serikali imezuia wasambazaji wasiuze mbolea hadi mchakato wa kusajili wakulima ukamilike.

Kwa hali ilivyo mazao yatadumaa tutapata hasara. Inaonekana watendaji wanao husika wana angalia zaidi misimu ya mvua ndio maana sasa hakuna mbolea madukani.

Tunaomba mbolea iruhusiwe kusambazwa au mchakato uende haraka. Kilimo bora cha kisasa kinahitaji kalenda ya uwekaji mbolea na upuliuzaji dawa. Kitu chochote kati ya hivyo kisipofanyika siku inayo hitajika mazao yanaharibika. Mazao ya hortcultural ni rahisi sana kuharibika endapo utapitisha angalau juma(week) moja tu ile tarehe ya kuweka mbolea.

Kuna watu wamekopa mitaji ya kulimia kwenye benki hivyo madhara ya hasara hizi yataunda mnyororo wa hasara sekta nyingi za kiuchumi. Mfano mtu amekopa TADB nayo TADB imekopa AfDB hapo kila taasisi itaathirika.

Bei za bidhaa kama nyanya, vitunguu, hoho, karoti, na vya aina hiyo zitapanda bei sana kutokana na uhaba.

Sote tuna juwa kanuni ya demand and supply hivyo tunaweza kutabiri nini kitatokea miezi mitatu ijayo kwenye masoko ya mboga mboga, matunda na viungo bila kusahau wakulima wa mahindi kwa umwagiliaji.

Wakulima wa maua yanayoenda nje watayumba tutakosa pesa za kigeni. Watu wenye mikataba na viwanda au masoko ya nje watashindwa kukidhi mashariti ya zabuni za kupeleka bidhaa husika kwa wakati.

Ujumbe huu umfikie pia Waziri wa kilimo.

Natanguliza shukrani.
 
Mbolea inauzwa kwa kificho kama gunia la bangi, Bei ipo juu sana.
Kama hauna mtandao wa watu (connection) hauwezi kuuziwa mbolea.
 
Back
Top Bottom