Rais Samia: Mara baada ya sisi kuanzisha tozo ya mitandao ya simu, Serikali ya Uingereza nayo ikaanzisha

Uingereza awawezi kuweka tozo za ovyo kama hizo.

Yaani mafisadi yamemzunguka mama na kumlisha uongo wa kishamba kweli; mwaka wa kodi U.K. unaanza 1 April baada ya hapo hakuna kodi wala tozo mpya mwaka unaofata.

Budget yetu sisi ni mwezi wa sita na inaanza papo hapo; dah halafu kuna watu wanamtaka mpaka 2030.
Sasa mnabishana na SSH ambaye yupo jikoni na Tony Blair kama consultant wake? Nyie vipi?
 
Akihutubia wananchi mkoani Kilimanjaro mheshimiwa Rais amesema mara baada ya sisi kuanzisha tozo ya kwenye mitandao ya simu ambayo ilipigiwa kelele na wananchi wengi, na Serikali ya Uingereza nayo imeanzisha tozo kama hii.

Kumbe mama anafanya vitu Hadi mataifa yaliyoendelea yanavikubali hadi kuiga.
Acheni sifa za kijinga, matumizi ya kodi na tozo huko Uingereza yanaweza kuwa haya yenu ya hovyo namna hii? Kwenye maendeleo zinapelekwa pesa kiduchu, asilimia 90 inaenda kwenye ANASA.
Bajeti ya Hovyo.PNG
 
Sasa mnabishana na SSH ambaye yupo jikoni na Tony Blair kama consultant wake? Nyie vipi?
Tony Blair taasisi yake inashauri mambo ya COVID na good governance; aina uhusiano wowote na mambo ya PR kama mada ya JF inavyodai na taasisi yenyewe ni non profitables organization.

Kitu pekee anachoweza fanya kwenye hiyo kazi nje ya majukumu yake ya taasisi kutengeneza mazingira ya U.K interest kwenye nchi zitakazotumia huduma yake. Halafu yeye mwenyewe apokei mshahara kwenye hizo kazi.
 
Rais Anapokuwa Mwongo

Katika hotuba yake alisema kwamba pesa za miamala wananchi wengi walikuwa wanalalamika lakini yeye aliamua kuwapuuza na kupunguza kidogo na itaendelea kuwepo ati kwa sababu tu hata Uingereza (UK) wameanzisha kodi hiyo.

Huu ni uongo uliopitiliza na sijui kwa sababu gani Rais mwenye dhamana anakuwa mwongo hadharani. Je, ni Tony Blair aliyemdanganya? Au anafikiria anaongoza masokwe?

Kwa taarifa yake UK hawahitaji kutumiana pesa kwenye miamala ya simu kwa sababu, mosi kila raia ana account ya Benki, raia wengi wana uwezo wa kutuma pesa kwenye account yoyote ile kwa njia ya mtandao (log in with hand-held devices) and within 2hours the amount of money will be in the recipients account.

Kwanza kujilinganisha na nchi kama UK kwenye tasinia ya technology ni ujinga uliopitiliza. Rais wetu wacha ulimbukeni. Hawa vibaraka uliowaweka ie JM na MC wanakupeleka kubaya.

Kuongoza nchi sio sawa na kuongoza NGO. Tozo ni wizi kwa sababu fedha hizo zimeshalipiwa kodi. (Double taxation ni dhuluma! Vile vile hakuna sheria iliyofuatwa kuona haki inatendeka kwa wote).

Rais SSH kama kweli anapenda kufuata yanayofanyika UK basi anza kutoa social welfare kwa kila mwananchi ambaye hana kipato.
 
Tony Blair taasisi yake inashauri mambo ya COVID na good governance; aina uhusiano wowote na mambo ya PR kama mada ya JF inavyodai na taasisi yenyewe ni non profitables organization.

Kitu pekee anachoweza fanya kwenye hiyo kazi nje ya majukumu yake ya taasisi kutengeneza mazingira ya U.K interest kwenye nchi zitakazotumia huduma yake. Halafu yeye mwenyewe apokei mshahara kwenye hizo kazi.
Hiyo haifuti ukweli kwamba Tony Blair ni mmoja wa washauri wa mama kwa masuala mbalimbali ikiwemo hiyo COVID!
 
Akihutubia wananchi mkoani Kilimanjaro mheshimiwa Rais amesema mara baada ya sisi kuanzisha tozo ya kwenye mitandao ya simu ambayo ilipigiwa kelele na wananchi wengi, na Serikali ya Uingereza nayo imeanzisha tozo kama hii.

Kumbe mama anafanya vitu Hadi mataifa yaliyoendelea yanavikubali hadi kuiga.

Basi awakaribishe wao ikulu ya chamwino, siyo kuendekeza kutafutiwa appointment hata za selfies panapo majaliwa 😁😁
 
Ok haya maswali yako yana uhusiano gani na mada husika?

Ni kweli waingereza wameiga?
Nilikuwa nakuonesha kuwa SSH ana mawasiliano ya karibu na waingereza hadi wengine ni washauri wake elekezi. Sasa wewe wa Laela una kipi cha kupinga? Yeye amesema wewe ni nani upinge?
 
Hahahaha

Watanzania tunahitaji Katiba Mpya.

Tozo tata sana

Watanzania gani mkuu. Sema wewe unahitaji katiba Mpya. Mimi binafsi sio kipaumbele changu. Sasa naangalia utekelezaji wa madarasa. Madawa. Madawati na mahospitali kama kweli watendaji tutatekeleza bila kuja kukulipia pumzi yako ya kushinda hapa mtandaoni.

Anza kujiangalia nidhamu yako ya maisha na mabaya unaowatendea wanaokuamini then tengeneza kakatiba kako. Ukianza kubadilika wewe tutafuata. Then katiba itakuwa Ni kama kufunga macho tu
 
Back
Top Bottom