Rais Samia: Maovu ya kuuana, kudhulumiana bado yapo Nchini, tuyakemee

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,795
11,958
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Baraza la Maulid kitaifa leo tarehe 09 Oktoba, 2022 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam



Samia Suluhu Hassan - Rais
Sina shaka tutakwepa pamoja, na waziri wa Afya yupo hapa, tutakwenda pamoja kwenye kuelimisha kuhusu maradhi yaliyoingia sasa kwenye ukanda wetu huu, suala la Ebola.

Wizara ya afya itaelimisha, viongozi wa dini mtaelimishwa ili nawenyewe waelimishe wafuasi wao kujikinga na maradhi haya.

Kuhusu swala la Maadili, nitumie nafasi hii kuwaomba sana viongozi wa BAKWATA na viongozi wote wa dini mlioko hapa kwenda kulisemea swala la maadili.

Maadili haya ni mtetereko uliotokea ndani ya taifa letu, kama wazazi, viongozi na walezi tulitetereka pahali, kwahiyo turudi tutazame wapi tulitetereka, tufundishane, tuongozane washike maadili.

Maovu ya kuuana, kuoneana, kudhurumiana bado yapo kwenye dunia yetu, na bado yapo kwenye taifa letu. Niwaombe viongozi wa dini tukayafanyie kazi nasi Serikali kwa upande wetu tutafanya kazi tunavyoweza.

Twendeni tukahimize watu wetu, tusimame na matendo mazuri. Sisi kama taifa tunatakiwa kuendelea na utaratibu wetu wa kupendana, kusaidiana na kuheshimiana ili kuwa na maisha ya furaha.

58bfe7f4-7cf7-40d6-a4ca-80a4c577cb9b.jpg

Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dkt. Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally Mbwana mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Diamond Jubilee kwa ajili ya kuhudhuria na kuhutubia kwenye Baraza la Maulid ambalo Kitaifa limefanyika Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha (kushoto) ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla
 
Na kile kitengo ndani ya taasisi cha kuchafua watu bila kujali kama ni wazee au vijana nacho kikemewe vinginevyo Karma itatenda !!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom