Rais Samia: Majirani zetu wanazo The so called 'Tume Huru', hawana migogoro? Auliza nini kinafatwa kwenye tume huru

Mimi sitaki tume huru wala katiba mpya.

Nataka watu waelimishwe kwanza wajitambue kabla ya kuvipata vyote hivyo.

Hakuna tija ya kuwa na vifaa vipya kabla ya kujifunza kwanza kuvitumia.

Tuondoane ujinga kwanza ndio twende huko.
😍👏👊
 
Rais Samia kauliza swali zuri sana!

Katiba mpya ndio kila kitu.

Katiba Mpya ni muarobaini wa matatizo mengi likiwemo la kuwa na Uchaguzi halali utakaopatikana tu kama kuna TUME HURU YA UCHAGUZI!! Sasa kwanini SSH na handlers wake wanaiogopa Katiba Mpya hata kama sio kila kitu?

Hizo wanazosema siasa za kistaarabu maana yake siasa ambazo hazitabadilisha mfumo wa kuwanyonya wananchi na kuhakikisha ccm haitoki madarakani!! A true opposition party cannot accept the status quo!!
 
Katiba Mpya ni muarobaini wa matatizo menig likiwemo la kuwa na Uchaguzi halali utakaopatikana tu kama kuna TUME HURU YA UCHAGUZI!! Sasa kwanini SSH na handlers wake wanaiogopa Katiba Mpya hata kama sio kila kitu?
Poleni Watz... Mwenyekiti wa CCM na Rais wa sasa,wakati wa Bunge la Katiba naona labda alijiridhisha kwamba wananchi Tz, hawataki Katiba mpya bali wanachotaka ni maji, chakula nk..... hahahahaaaa...
 
Huyu mama na CCM hawawezi kuiachia hii system ya sasa ambayo ndio inawaweka pale, wanajua siku wakikubali uchaguzi huru kwa katiba au tume ndio utakuwa mwisho wao, dawa ni kuwaburuza tuu kama alivyoburuzwa mkoloni
 
Poleni Watz... Mwenyekiti wa CCM na Rais wa sasa,wakati wa Bunge la Katiba naona labda alijiridhisha kwamba wananchi Tz, hawataki Katiba mpya bali wanachotaka ni maji, chakula nk..... hahahahaaaa...

Kuna handlers wake SSH ndiyo wanamyumbisha kwani wameisha gundua weakness yake!!
 
"Wananchi wangu wana Uelewa mdogo sana wa masuala ya Siasa, Uongozi na Demokrasia hebu naomba Kazi kubwa kabla ya Katiba Mpya ianzie katika Kuwaelimisha"

Mpaka 2025 tutatukanwa mara Milioni.
 
Mimi sitaki tume huru wala katiba mpya.

Nataka watu waelimishwe kwanza wajitambue kabla ya kuvipata vyote hivyo.

Hakuna tija ya kuwa na vifaa vipya kabla ya kujifunza kwanza kuvitumia.

Tuondoane ujinga kwanza ndio twende huko.
Waliotoa maoni ya Katiba ya Warioba walikuwa kutoka Kenya??

Aruhusu tu wiki moja tu tuingie mtaani kwenye makongamano ndio aje ashangazwe na hawa watanzania.

Atabaki mdomo wazi.
 
Rais Samia kauliza swali zuri sana!

Katiba mpya ndio kila kitu.
Hakuna swali zuri hapo, Ni kufail kwa thinking capacity, làbda kwa nyinyi wenye vichwa vya panzi.

Yaliyotokea kwetu 2019 na 2020 hayawezi kutokea Kenya, Ghana and the like countries. Aliyeshinda anatangazwa, ni hicho tu what is to be realised at the end of the day.

Na ili upate hicho lazima kuwe na tume HURU ndani ya Katiba which is derived from all stakeholders ie it catters for all citizens interests
 
Hakuna swali zuri hapo, Ni kufail kwa thinking capacity, làbda kwa nyinyi wenye vichwa vya panzi.
Yaliyotokea kwetu 2019 na 2020 hayawezi kutokea Kenya, Ghana and the like countries. Aliyeshinda anatangazwa, ni hicho tu what is to be realised at the end of the day. Na ili upate hicho lazima kuwe na tume HURU ndani ya Katiba which is derived from all stakeholders ie it catters for all citizens interests
Kwani hapa aliyeshinda hatangazwi?
 
nchi zenye tume huru na bado zina migogoro, basi zina migogoro isiyo ya kiuchaguzi na kama wana migogoro ya kiuchaguzi basi tume hizo huru si mazao ya katiba ya wananchi.
Hizo ndizo tume ambazo tunataka kuziunda hapa Tanzania. Huwezi kuunda tume huru ambayo katiba haijaruhusu uhuru wake kuanzia kwenye uundwaji wake, viongozi na watendaji wake, na usimamizi wake nk
 
Rais Samia akiwa anapokea ripoti ya kikosi kazi alichounda ameongelea Tume huru ya uchaguzi na kuhoji uwepo wa kuendelea migogoro kwenye nchi za jirani zinazotajwa kuwa na tume huru.

Rais Samia ametaka kujua 'Definition' ya tume huru na ipi kiu itakayopatikana kwenye tume huru.

======

Samia Suluhu: Tume huru hizo na nini mtatulete mapendekezo, tume huru maana yake nini!

Iweje? Lakini angalieni na mifano ya waliokuwa na tume huru, Je hawana migogoro ya kisiasa? The so called 'Tume Huru'.

Kwa mfano majirani zetu wanazo The so called 'Tume Huru' lakini zinaendeshwaje? Hawana migogoro? Hawatangazi matokeo wakakimbia nchi kabisa?

Si hutangaza matokeo kisha wakakimbia! Nendeni nchi mbalimbali zenye hizo zinazoitwa tume huru, angalieni yanaendaje lakini tunaposema tume huru tunafata nini hasa huko kwenye tume huru.

Kitu gani kinatupa kiu tunahisi tutakipata kwenye tume huru huko na definition hasa ya tume huru ni nini?

===

Kuhusu maboresho ya sheria na kanuni za Uchaguzi, Rais Samia amesema watasema vipengele gani vinavyouma kwani inawezekana maboresho yakifanyika, kelele ya katiba inaweza ikaishia kwasababu zile kiu za watu zinapotaka katiba ibadilishwe ilishafanyiwa kazi.

PIA, Soma=> Ikulu, Dar es Salaam: Rais Samia apokea taarifa ya Kikosi Kazi cha Kuratibu Maoni ya wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa
Naunga mkono hoja
 
Sasa kama tume huru haizuii migogoro, si aiondoe kabisa, kwa nini tunayo?

Tume huru ndizo zinasababisha migogoro?

Hao majirani zetu kweli wana tume huru?
 
Back
Top Bottom