Rais Samia: Mahabusu wengi kesi zao ni za kubambikwa, wenye hatia wanaachwa uraiani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,456
Rais Samia Suluhu Hassan amesema “Tulikuwa tunaangalia magereza yetu tukabaini waliofungwa na walio mahabusu idadi yao ni kama ilikuwa sawa, wengi wao ni kesi za kubambikwa ndio maana unakuta mtu yupo ndani miaka mitatu, haendi mahakamani, haulizwi na hakuna kesi ya maana.

“Tulichofanya ni kuwatoa magereza yakapata kupumua, msipofanya haki, mnapochukua rushwa kumtia mtu hatiani ambaye hana hatia na mwenye hatia mkamuacha nje anaendeleza ubabe akiamini pesa yake itambeba, ambaye hana hela anaishia jela.

“Usiangalie Duniani, umechukua fedha sawa, imekufanya umekuwa nani, imekufikisha wapi, matatizo yako ya Dunia yameisha, ni ushawishi tu wa akili, itendeeni haki sheria.”

Amesema hayo Novemba 24, 2022 alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wanasheria wa 27 Afrika Mashariki unaofanyika Jijini Arusha.
 
Kumbe anaijua haki tatizo anaiogopa pale anapoona kuna dalili ya maslahi yake kuingiliwa, awaache wapinzani wafanye mikutano ya siasa kwani ndio haki yao, na asiwabambikie kesi wale wanaotoa maoni hasa kuhusu Katiba Mpya.
 
Nani anashituka kwa maneno hayo, kama ushahidi wa watu kubambikiwa kesi upo, na ushahidi kwamba wenye pesa wako nje, serikali imewachukulia hatua gani wahusika?
Hapa ndiyo Takukuru wanatakiwa kua active kwenye Mambo Kama hayo, lakini mwisho wa siku na wao wamekua wa shiriki wa uchafu huo ndiyo maana wamekua kimya hata ukienda kulalamika wanakuangalia tu maana na wao wanapenda kitu kidogo!!
 
Hayo yote mnayajua ila mnajizima data yaani kuna Watu mpaka sasa hivi wanaamini Mahakamani ni sehemu ya kupata haki ila ukweli ni kwamba katika Watu watakaongoza gwaride la kwenda jehannam baada ya Polisi ni Mahakimu wajinga hawa...
 
Kwa hilo!

Mungu aubariki uzao wako!

Nakuunga mkono!

Lakini

Umeme, Umeme,maji,maji,mfumuko wa Bei!!!

Elimu yetu hailipi! kwasababu BILA kuajiriwa huna cha kufanya!!!

Masomo ya ufundi yawe rasmi sekondari na kule msingi stadi za kazi zifanywe kwa vitendo na ziboreshwe!!!

Elimu ya kukariri ife,vitendo vitamalaki mashuleni!

MUNGU ibariki TANZANIA nchi YANGU!
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema “Tulikuwa tunaangalia magereza yetu tukabaini waliofungwa na walio mahabusu idadi yao ni kama ilikuwa sawa, wengi wao ni kesi za kubambikwa ndio maana unakuta mtu yupo ndani miaka mitatu, haendi mahakamani, haulizwi na hakuna kesi ya maana.

“Tulichofanya ni kuwatoa magereza yakapata kupumua, msipofanya haki, mnapochukua rushwa kumtia mtu hatiani ambaye hana hatia na mwenye hatia mkamuacha nje anaendeleza ubabe akiamini pesa yake itambeba, ambaye hana hela anaishia jela.

“Usiangalie Duniani, umechukua fedha sawa, imekufanya umekuwa nani, imekufikisha wapi, matatizo yako ya Dunia yameisha, ni ushawishi tu wa akili, itendeeni haki sheria.”

Amesema hayo Novemba 24, 2022 alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wanasheria wa 27 Afrika Mashariki unaofanyika Jijini Arusha.
JE HAO WALIOWABAMBIKIZIWA HAO MAHABUSU WAMEFANYWA NINI ?
 
Back
Top Bottom