Rais Samia leo Juni 03 amepokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais Kagame wa Rwanda

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,204
4,692
Wasau wa JF,

Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo Juni 03 amepokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mheshimiwa Paulo Kagame.

Katika ujumbe huo uliowasilishwa na Mjumbe maalumu Vincent Biruta ,Rais Kagame alitoa pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli , alimpongeza kwa kupokea kijiti cha Urais na pia alimuhakikishia kuwa Rwanda itaimarisha ushirikiano na Tanzania

Kazi Iendelee.

 
Mnafiki utamjua tu.kagame ni mtu mwingine,kama jirani na rafiki wa magufuri hakuja msiba Leo ndo àtoe pole,huo ni kumsanifu rais wetu
Pamoja na kuwa kuhani hakuna kipindi maalum………..lakini muda wote huoooo!!!!? Au naye alikuwa anawaza kama MATAGA wengine walivyokuwa wanafikiri kuwa, baada ya MWENDAZAKE "kwenda zake",basi ndiyo mwisho wa TZ!?
 
😅
1622720872148.png
 
Mnafiki utamjua tu.kagame ni mtu mwingine,kama jirani na rafiki wa magufuri hakuja msiba Leo ndo àtoe pole,huo ni kumsanifu rais wetu
Pole za msiba hazina ukomo, hata baada ya miaka kadha unaruhusiwa kutoa pole!
 
Safi, tuzidi kuimarisha mahusiano yetu na mataifa jirani.

Rwanda ni Jirani zetu na pia ni wadau wakubwa ktk mashirikiano ya kiuchumi.
 
Yaan raia tuneshasahau kifo cha Magufuli, leo mjumbe maalum wa Paul Kagame anatoa pole kwa Tanzania, Maajabu
 
Back
Top Bottom