Rais Samia kwenda Zambia na Kikosi cha Viongozi wa CCM ni mkakati wa kujenga Urafiki na kilichokuwa chama Pinzani?

SOPINTO

Senior Member
Oct 19, 2020
155
385

Rais Samia kwenda Zambia na Kikosi cha Viongozi mbalimbali wa CCM Je, ni mkakati wa kujenga Urafiki na kilichokuwa chama Pinzani?​


Leo Rais Samia anatarajia kuondoka nchini kuelekea nchini Zambia kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais mpya wa nchi hiyo Hakainde Hichilema , miaka yote tumezoa Rais kuondoka na viongozi wachache wa Serikali lakini hii ya leo ni kama mpya juu ya msafara mkubwa uliobeba viongozi wa kichama zaidi kwa lengo la kuhudhuria sherehe za kuapishwa.

Viongozi wa CCM wanaoambatana na Rais ni pamoja na Naibu waziri mambo ya nje , Katibu NEC, Itikadi na Uenezi , Katibu Idara ya Oganaizesheni CCM, Waziri Mkuu mstaafu , Mjumbe wa Kamati Kuu CCM, ni kama maajabu safari hii imembeba mpaka Mbunge Comedian wa jimbo la Mtera.

Rais kuambatana na kikosi hiki inaonekana kuna ajenda maalum wanaenda kuiseti , mana serikali hii ni mpya na imeingia madarakani kwa mateso kupitia vikosi vya ulinzi ikiwemo jeshi la polisi wakati huohuo huku Tanzania kupitia utawala wa enzi za mwendazake ulisaidia mbinu mbalimbali za kumnyanyasa mzee Hichilema, sasa naona CCM wanaenda kuweka mambo sawa kwa kujinasibu kuwa kwasasa ni serikali nyingine sio ile.

Vyama vya upinzani nchini na nyie mchangamke msilale lale muwe na plan zaidi ya moja wakati mnapambania Katiba Mpya , kuwe na mkakati mwingine wa masaa 24 day and night , siku 360 , all seasons.
 
Na hii itasaidia Sana kuondoa tozo,big up Sana kwa CCM.
Samiaana Halifax ngumu ni Edgar Lungu ajaye yawning wapinzani wakijipanga asubuhi tu mama ataangushwa! Yeye ni kusoma graph tu ndo anachojua anatoka watu wanapiga kama kawa!
 
Hongera

Sana mama wa Taifa kwa kujali majirani zetu uwe na safari njema na uchape kazi ikiwezekana ukae huko huko kama mwaka mmoja au miwili umsaidie kiongozi huyo mpya Raisi wa Zambia mbinu za uongozi,sisi tutavumilia tu hadi hapo utakaporudi. Sawa!
 
Ni mwendawazimu aliepoa.Huwezi kwenda Zambia kwa mbwembwe zote hizo kwenda kushiriki kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani wakati huku nyumbani kwako unawadhibiti wapinzani na kuhakikisha kuwa wanakiona cha mtemakuni.
 
Kada wa CCM mzee Mgaya anasema CCM wako Zambia kwenye hafla ya kumwapisha Rais mpya kama chama tawala na wamesindikizwa na washirika wao kwa upande wa Zanzibar ACT wazalendo.

Tukio hili liko mubashara Channel ten.

Updates;
 
Ujinga ni kuhisi chama tawala kitaongea na chama pinzani cha nchi nyingine, the political immaturity ya watanzania na wapinzani ni below sea level
 
Back
Top Bottom