Rais Samia kwanini teuzi za Kisiasa hazina longolongo kama za Watendaji? Wanasiasa mnanyanyasa Watendaji kwenye Kuteua

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
1,281
2,020
Mh. Rais Samia Hassan Suluhu,

Ni ukweli usiopingika kuwa watendaji wengi wa Serikalini wananyanyasika sana sana. Mwanasiasa kama Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na hata baadhi ya watendaji wa ngazi za kuteuliwa na Mamlaka ya Raisi kama MaKatibu Wakuu n.k wamekuwa ni watu wasiokuwa na vikwazo vyovyote vya kupanda katika nafasi hizo. Tatizo lipo hasa kwa hawa watendaji wa kati katika Serikali - Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo n.k. Unyanyasaji upo katika namna mbalimbali mojawapo zikiwa ni kama zifuatazo:

1. Kufanyiwa usaili na upekuzi kwa watendaji viongozi serikalini (vetting) - hapa kuna manyanyaso makubwa sana sana kiasi kwamba ningeshauri Mamlaka za Uteuzi pengine ziachane kabisa na mambo ya kushindanisha watu na kuwafanyaia upekuzi. Utaraibu uliop hapa ni nafasi kutangazwa, kisha wahusika wanafanyiwa usaili. Wahusika wanasubiri matokeo lakini matokeo hayo hayatoki na mwisho wa siku nafasi hiyo inajazwa na mtu mwingine kabisa ambaye hata usaili husika hakufanya.

Kuna Taasisi nyingi sana za Serikali ambazo waliofanyiwa usaili tunawafanyia upekuzi kwa muda mrefu sana kiasi kwamba inakuwa kama huo upekuzi ni kuwatafutia watu dosari. Hii ni tofauti kabisa na wale wanaoteuliwa kwenye nafasi za kisiasa. Kwa mfano ni miezi karibia sita sasa tangu Uchaguzi wa mwaka jana ufanyike lakini mpaka sasa wakuu wa mikoa na wilaya wanaelekea kupatikana wote. Hata Wakurugenzi wa Halmshauri wanapatikana soon bila kucheleweshwa. Wakati hao wakipewa nafasi kuna Taasisi za Serikali ambazo wasailiwa walifanya usaili tangu zaidi ya miaka mitatu iliyopita na nafasi zao hazijawahi kujazwa na pia wasailiwa hawajawahi hata kufahamishwa iwapo walifanikiwa au hawakufaikiwa katika usaili huo. Hivi huo upekuzi wa Zaidi ya mika mitatu au minne unakuwa umekusudia kitu gani?

Kwa nini wanasiasa mnawapelekesha hivyo watendaji wa Serikali? Bila kuzitaja nafasi husika na Taasisi ambazo usaili wa watendaji wake umekuwa ni wa muda mrefu ninakuomba Mheshimiwa Rais ujaribu kufuatilia hilo na angalau hata kulikemea kwa kupitia Katibu Mkuu wa Utumishi. Bila kulikemea hili basi linaleta tu mtazamo wa awamu ya tano ambapo watu walikuwa wakiteuliwa kwa kufuata ukabila (angalia baadhi ya Taasisi za maana hapa nchini ambako asimilia 40 ni kutoka kabila Fulani).

2. Utaratibu mwingine ni kupitia kukaimisha watendaji kwa nafasi mbambali katika Taasisi za Seruikali - hapa watendaji wengi wamekuwa wakikaimishwa kwa muda mrefu kuliko miezi sita ile inayotambulika kwenye Kanuni. Pamoja na msisitizo ulioweka wa kupandisha watumishi vyeo bado (kwa utafiti wangu binafsi) Zaidi ya 55% ya watumishi walioshika nafasi mbambali za kukaimu nchini wanaendelea kukaimu.

Nenda Ofisi yeyote ya Halmshauri, Taasisi za Serikali na hata kwenye mawizara utakuwa watumishi wanaendelea tu kukaimu nafasi wakati kwa nyie wanasiasa na wale wanaouteuliwa na Raisi ukiangalia hata wakuu wa wilaya, wa mikoa, maDED n.k waliokuwa wanakaimu haizidi hata asilimia tatu ndiyo wanaokaimu na wengi wao hukaimu kwa muda mfupi sana na nafasi zao kujazwa.

Sasa kama hawa nafasi zao zinajazwa faster kwa nini watendaji wengine wa Serikali wanaendelea tu kukaimu? Wanasiasa tafadhali wafikirieni basi na watendaji wengine - msijipendelee wenyewe tu? Ona mfano yule Mtendaji wa OSHA mama amekaimu yule kwa sasa inawezekana hata miaka mitano imeshafika lakini hakuna kuteuliwa na usishangae akatolewa pale analetwa Sukuma Gang.

Mwisho Mheshimiwa SSH nakuomba na kukushauri angalua utamke neno kwa jambo hili ili lifanyiwe kazi kuwapunguzia manyanyaso Watendaji wa Serikali ambao siasa zimewakalia kooni.
 
Bila kuwa na utawala wa majimbo/mikoa hayo matatizo yatudumu milele
 
Back
Top Bottom