Rais Samia, kwanini kwenye hotuba yako UN umeshindwa kuinadi Tanzania?

Ule mkutano haukuwa kwa ajili ya kunadi nchi wala kuelezea matatizo binafsi ya nchi bali global agenda..

Kuna majukwaa mengi ya hivyo Kama Davos nk
Wewe nafikir umekuwa Brain washed na elimu fake ya wazungu kiasi kwamba hata unashindwa kujitambua. Ungejua thamani yako katika ulimwengu huu, nadhani usinge sema maneno kama hayo. Shame on you!

Msikilize Rais Tscheked wa DRC alivyotoa speech yake kwenye jukwaa hilo hilo ambalo wewe unadai kuwa "halikuwa jukwa la kuelezea matatizo binafsi ya nchi bali global agenda".

Kitu kingine naomba huko mbele jaribu kutofautisha mkutano ambao ulifanyika miongoni mwao na jukwaa la kujieleza.
Kama unashindwa kutofautisha haya basi rudi tena darasani ukaanze upya. Nafikiri mtu mweupe amekughiribu sana akili kiasi kwamba hata unatia aibu.

Nafikiri Rais Samia Suluhu Hassan huko aliko, ata kuwa anajitathmini mwenyewe nafikiri, kwa makosa aliyo yafanya. Amepewa nafasi ya kujieleza; Anacho kifanya ni kuelezea theme ileile ambayo ambayo mda wote wamekuwa wakiiongelea kwenye mkutano wao na ambayo inajulikana ulimwengu mzima na vile vile kutangaza biashara za vaccines za akina Bill Gates na matajiri wengine wakubwa. Huko ni kutojielewa! Anisamehe kwa hilo.

Wazungu wanawafurahia Marais kama hawa ambao hawawapi matatizo na amabo wanawasaidia kuwaneemesha kwa kuwatangazia biashara zao. Ni ahibu!

Ningekuwa mimi Rais Samia nafikiri ningemtupilia mbali mtumishi aliye iandaa hiyo speech na kufanya Rais wetu ahaibike mbele ya watu wake na waafrika wenzetu kwa ujumla. Mtumishi huyo inaonyesha bado hajajua ulimwengu wa leo unaendaji. Na nini sisi tunatakiwa tufanye ili tuondokane na upuuzi wa kuwa wstumwa wao wa kiuchumi. Huyo mtumishi bado yuko kwenye fikra za kikoloni. Hajapevuka bado na ni hatari kwa taifa letu.

Rais wa nchi yenye rasilimali kubwa na wasomi wa ma-PhD kibao kama Tanzania, sikuona umuhimu wa kwenda kuwapigia magoti wazungu kuwaomba watupe chanjo. Si tununue tu kwa hela zetu kama tunazihitaji.
Kulikuwa kuna haja gani ya kwenda kusalim amri kwa binadam ambao wana fikra za kinyama na ambao hawatujali sisi wala kututhamini sisi kama binadam wenzao?

Nchi gani tajiri ulimwengu huu inaamini kweli katika demokrasia na hakibza binadam? Rais alitakiwa kwanza ajiulize mwenyewe, hiyo demokrasia na haki za binadama anazo zipigia kelele kwenye majukwaa ya kimataifa, nani anafaidika nayo? Ninge mwomba Rais wetu afanye uchunguzi wa nani anafaidika na hiyo demokrasia na haki za binadam ambazo hizo nchi za kibeberu zina propagate.

Kuna nchi ambayo manigger wanauwa na kuswekwa jela kama kuku kama Amerika duniani? Kuna nchi mabepari wamezidi kuwa matajiri wa kupindukia huku wakiwaumiza wananchi wao kwa mishahara midogo na conditions mbaya za kufanya kazi kama Amerika?

Ulaya nako, kama hii nchi ninayo ishi ya Ujerumani, wafanyakazi wengi kwenye makampuni yao hasa makampuni ya magari na mashine wamekuwa watumwa tu. Mishahara yao haiwatoshelezi kukidhi mahitaji yao kama ya kununua magari mapya na furnitures, ili waweze ku-afford hivyo vitu, inabidi wachukue mikopo. Kwa namna hiyo hawana budi kuenyeka mpaka wanazeeka.

Haya yote yanasababishwa na ujinga wao. Wanarizika na hela ndogo ya bure wanayo pata kutoka serikalini wakiwa jobless. Nao pia hawajitambui kuwa wanaumia.
 
utaongea nn pale kumbuka zamani kulikua na balozi pia
Kwani sasa hivi hatuna balozi kwenye baraza la UN? Of course tunaye, ila asikiki kama zamani Salim Ahmed Salim alikuwa.

Swala sio kwamba tuna balozi au hatuna, swala hapa la kulizungumzia ni inakuwaje Rais wa nchi kama Tanzania, nchi ambayo toka kuanzishwa kwake imekuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru wa Afrika na kuwa na kiongozi aliyeiva na siasa ya Mwalim Nyerere anakwenda UN kusalim amri na kuanza kupigia debe kushamiri kwa ubepari ambao sasa umekuwa ni ubeberu duniani? Kweli ni kitu cha ajabu sana na cha kusikitisha.

Nina uhakika mtu kama Hamphrey Polepole, Bashiru Alli, Lukuvi na Prof. Kabudi ndiyo kabisaa wasinge toa speech kama hiyo iliyo tolewa na Rais wetu jukwaani. Haya ni majemedari ya CCM yanayo jitambua. Wamepikwa na kuiva na misingi ya mwasisi wetu kuto surrender!
 
Nina uhakika mtu kama Hamphrey Polepole, Bashiru Alli, Lukuvi na Prof. Kabudi ndiyo kabisaa wasinge toa speech kama hiyo iliyo tolewa na Rais wetu jukwaani. Haya ni majemedari wa CCM wanao jitambua. Wamepikwa na misingi ya mwasisi wetu kuto surrender!
Bado kama serikali tunahoja yakujibu kilichotokea Dodoma kwalisu kijibiwe

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Siasa za Rais Mstaafu Kikwete ningekuomba achana nazo. Hazitakufikisha mbali. Na wala Rais Kikwete hataingia kwenye records ya watanzania kuwa ni Rais ambaye amefanya mambo makubwa kwa watanzania na nchi yake. Rais Kikwete alijali sana kukutana na wazungu juu kwa juu, kitu ambacho kili wa-cost watanzania maisha yao.

Mama usionyeshe tabia ya kumkana Hayati Rais Magufuli, wewe yaendeleze yake na fanya yako mengine mapya. Tabia ya kumkana Hayati Magufuli inaweza ikaku-cost. Watanzania wengi bado wanampenda sana Magufuli.
 
Bado kama serikali tunahoja yakujibu kilichotokea Dodoma kwalisu kijibiwe

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
Hivi Lissu ni nani kwa watanzania? Huoni kama yeye ni mwuuza nchi? Mtu yeyote anaye shirikiana na mabeberu kutaka madaraka kwa hali na mali, unategemea ntu kama huyo atakuwa na uwezo wa kujitutumua mbele ya wawekezaji wake? Thubutuu! Hataweza fanya chochote zaidi ya kuamua vitu kuwa favour mabwana zake.

Amwangalie Malema jinsi anavyo endesha upizani Afrika ya Kusini. Hivyo ndivyo wazalendo wanavyo takiwa kufanya. Na sio chuki ya kutaka kushika Dola kwa nguvu za mabeberu. Haita work. Na mimi sitakubali.
 
Kwani sasa hivi hatuna balozi kwenye baraza la UN? Of course tunaye, ila asikiki kama zamani Salim Ahmed Salim alikuwa.

Swala sio kwamba tuna balozi au hatuna, swala hapa la kulizungumzia ni inakuwaje Rais wa nchi kama Tanzania, nchi ambayo toka kuanzishwa kwake imekuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru wa Afrika na kuwa na kiongozi aliyeiva na siasa ya Mwalim Nyerere anakwenda UN kusalim amri na kuanza kupigia debe kushamiri kwa ubepari ambao sasa umekuwa ni ubeberu duniani? Kweli ni kitu cha ajabu sana na cha kusikitisha.

Nina uhakika mtu kama Hamphrey Polepole, Bashiru Alli, Lukuvi na Prof. Kabudi ndiyo kabisaa wasinge toa speech kama hiyo iliyo tolewa na Rais wetu jukwaani. Haya ni majemedari ya CCM yanayo jitambua. Wamepikwa na kuiva na misingi ya mwasisi wetu kuto surrender!
Ningependa kuongeza kitu kidogo kuhusu mabeberu. Amerika na baadhi ya nchi za Europe ziko kwenye stage ya kufa. Hizo nchi zinatapatapa. Kuiacha system yao ya unyonyaji ili kubadilisha mfumo kwa ajili ya kuokoa jahazi, hiyo hisani hawataweza kuitoa. Wako radhi tuangamie wote.

Amerika inakufa. Inaishi kwa kuwalisha wananchi wake mambo ya uongo kuhusu China na baadhi ya nchi ambazo zinafanya vizuri. Amerika imebaki ni mabavu tu. Lakini kama system imekuwa obsolete!

Sikilizeni wenyewe mazungumzo ya wasema kweli kwenye hii clip.

Siasa za Rais Mstaafu Kikwete ningekuomba achana nazo. Hazitakufikisha mbali. Na wala Rais Kikwete hataingia kwenye records ya watanzania kuwa ni Rais ambaye amefanya mambo makubwa kwa watanzania na nchi yake. Rais Kikwete alijali sana kukutana na wazungu juu kwa juu, kitu ambacho kili wa-cost watanzania maisha yao.

Mama usionyeshe tabia ya kumkana Hayati Rais Magufuli, wewe yaendeleze yake na fanya yako mengine mapya. Tabia ya kumkana Hayati Magufuli inaweza ikaku-cost. Watanzania wengi bado wanampenda sana Magufuli.

Samahani mkuu. Sijajua point yako kwenye kuninukuu huku.
Yaani sijakuelewa unaposema eti Jk hana mambo makubwa aloifanyia nchi hii.
Serious!
Kuunganisha lami mikoa yote kiasi leo hii Dar-Mwanza hulazimiki kupitia nchi jirani, kwako ni jambo dogo!
Kuna Rais tokea tupate Uhuru Ameajiri Kama Kikwete? Ilikuwa ukisomea Ualimu tu hata huhitaji kuomba kazi, ukihitimu ni unapangiwa kituo cha kazi tu. Hili kwako ni dogo!!

Watu walifanya siasa mpaka kumtukana, je yupo Rais amewahi kufikia rekodi yake?

Eti unamshauri Mama aendeleze ya Magufuli, yaani aendelee kutoajiri?
Aendeleze utekaji!?
Aendeleze Ukabila na Ukanda!?
Awe katili kama mtangulizi wake!?
Au asipandishe Mishahara na Madaraja kwa Watumishi kama ilivyokuwa 6yrs ago!?
 
Mbona unacho andika unajisuta mwenyewe? Kwani wakati wa utawala wa Rais Kikwete waziri wake wa ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakati ule alikuwa nani? Si hayati Rais Magufuli? Na hilo azimio la kujenga Barabara kwa fedha zetu za ndani, nani alimshauri Rais marehem Mkapa wakati ule? Si huyo huyo hayati Rais Magufuli?

Bila hayati Magufuli wakati ule, hakuna kitu kingefanyika. Amini ninacho kueleza. Fikiria wewe mwenyewe, kwa mfano, tulidanganywa kuwa meli kubwa ya wachina ambayo ilikiwa ikivua samaki kwenye deep sea yetu, eti imezama, baada ya Rais Magufuli (wakati ule waziri), kuipiga "tanch", yaani kuizuia.

Kitu kama hiki katika uelewa wako wa vitu inawezekana kweli? Na kama inawezekana mbona hakuna maelezo yoyote kuhusu kuzama kwa hiyo meli? Na imezama position gani? Vipi hali ya crue members wa hiyo meli walienda wapi au waliokolewa vipi?

Wewe unafikiri swala kama hili litazimwa vipi bila Rais wa nchi kujua? Of course Rais Kikwete alitia mkono wake kwenye hiyo mada.

Kijana kwa taarifa kama hii na hali ilivyo kuwa kimaisha wakati wa utawala wa Rais Kikwete hata kama ungepata ajira gani na ngapi, ni kazi bure ninakuambia. Hali ya maisha ya kila mtu kufanya anachotaka bila "state control", ni jambo la hatari sana kwa maisha ya watanzania. Tumshukuru Mungu ametuepusha na manaya, inge escalate, sijui sasa tungekuwa tunazungumza nini?

Vyombo vya usalama vilikuwa kwa ajili ya kuwalinda viingozu tu na sio raia wa kawaida kama wewe na mimi.

Ile haikuwa uhuru na wala ajira, bali ilikuwa ni "chaos". Sina haja ya kukueleza mengi, nafikiri utakuwa umesha sahau jinsi serikali yetu ilivyo kuwa ikiendeshwa wakati ule. Watanzania hawakuwa na orientation hata kidogo ya policy ya serikali.

Sitaki kutoa list ya mambo ambayo yalienda vibaya nchini. Nitakuchosha tu. Naomba tujikite kwenye mada yetu.
 
Back
Top Bottom