Rais Samia: Kwa wale mliokuwa na mashaka, mwanamke huyu ataweza kuwa Rais wa Tanzania? Nataka niwaambie aliesimama hapa ni Rais wa JMT

Admin1988

JF-Expert Member
Mar 30, 2017
1,603
1,835
Wakuu,

Wale mlio kuwa na wasi wasi amesema, "Kwa wale mliokuwa na Mashaka, mwanamke huyu ataweza kuwa rais wa Tanzania! Nataka niwaambie Alie simama hapa ni Rais wa JAMHURI ya MUUNGANO wa TANZANIA" ~ Mh Samia Hasan Suluhu.

Mjadala umefungwa tuchape kazi. Kwa manufaa ya watanzania wote.

====

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka Watu wote wenye mashaka ikiwa yeye anaweza kuwa Rais, kuwa na uhakika naye kwasababu yeye ndiye Rais ambaye maumbile yake ni mwanamke.

Akitoa salamu zake kwenye shughuli ya kuaga Mwili wa Hayati Dkt. John Magufuli, Rais Samia amesema kutangaza kifo cha Rais Magufuli haikuwa rahisi, Kifo hiki hatukutarajia na Magufuli alikuwa kipenzi cha wengi

Amesema Tanzania ipo katika mikono salama kwasababu yeye na Rais wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi wataendeleza alipoishia Rais Magufuli na wataifikisha Nchi pale ilipokusudiwa kufika. Awataka Watanzania kutafakari mema na dira ya Magufuli pamoja na kuijenga Tanzania.

 
Back
Top Bottom