Pre GE2025 Rais Samia kwa Mabalozi: Hatupo hapa kuelekezwa nini cha kufanya kwenye nchi yetu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Sep 2, 2024
1,561
4,025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan hivi karibuni amejibu kuhusu matamko yaliyotolewa na balozi mbalimbali hapa nchini Tanzania kufuatia kifo cha Kada wa CHADEMA, Ali Kibao.

Mara baada ya Ali Kibao kupatikana akiwa amefariki huko Ununio, Dar Es Salaam balozi za nchi mbalimbali kama Marekani, Ufaransa na Umoja Wa Ulaya yaani EU walijitokeza kukemea kitendo hicho na kuitaka serikali ya Tanzania kufanya uchunguzi wa haraka.

Soma Pia:
Rais Samia: Mauaji ya Kibao hayakubaliki. Uchunguzi umeanzishwa

Leo akiwa anatoa hotuba kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi La Polisi, mkuu huyo wa nchi amedokeza kuwa hayuko tayari kuelekezwa nini cha kufanya na kwamba Tanzania ina katiba na miongozo yake na kwamba sisi tunajua nini cha kufanya.

Source: Mwananchi
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan hivi karibuni amejibu kuhusu matamko yaliyotolewa na balozi mbalimbali hapa nchini Tanzania kufuatia kifo cha Kada wa CHADEMA, Ali Kibao.

Mara baada ya Ali Kibao kupatikana akiwa amefariki huko Ununio, Dar Es Salaam balozi za nchi mbalimbali kama Marekani, Ufaransa na Umoja Wa Ulaya yaani EU walijitokeza kukemea kitendo hicho na kuitaka serikali ya Tanzania kufanya uchunguzi wa haraka.

Leo akiwa anatoa hotuba kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi La Polisi, mkuu huyo wa nchi amedokeza kuwa hayuko tayari kuelekezwa nini cha kufanya.
Ngoja walete karibu USS Theodore Roosevelt (CVN-71) ndiyo utajua hujui
 
Back
Top Bottom