Rais Samia kuzindua kitabu cha mkakati wa Sensa

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,050
4,904
Rais Samia Suluhu Hassan Septemba 14 atazindua kitabu cha mkakati wa uelimishaji na uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 jijini Dodoma.

Taarifa hiyo imetolewa leo Septemba 12, 2021 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu shughuli hiyo aliyosema inalenga kuandaa umma na wadau kuhusu sensa ya watu na makazi mwakani.

Mkuu wa Mkoa amesema uzinduzi huo unaokwenda na kauli mbiu ya ‘Sensa kwa maendeleo, jiandae kuhesabiwa’ utafanyika Septemba 14 uwanja wa Jamhuri jijini hapa kuanzia saa 1 asubuhi

Kwa mujibu wa Mtaka, viongozi mbalimbali watahudhuria akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atakayekuwa mwenyeji na Mwenyekiti mwenza kutoka Zanzibar ambaye ni Makamu wa pili wa Rais Hemed Suleiman Abdallah.

Viongozi wengine ni Kamisaa wa sensa Tanzania Bara, Anne Makinda, Kamisaa wa sensa Zanzibar, Balozi Mohamed Haji Hamza, pamoja na Mawaziri, Manaibu Waziri, Makatibu wakuu, Manaibu katibu wakuu na viongozi wa serikali kutoka Mikoa minne.

Mkuu wa Mkoa amesema Viongozi wa serikali kutoka Mikoa minne ya Singida, Iringa, Morogoro na Manyara watashiriki hivyo akaomba wananchi wa wa Dodoma kujitokeza kwa wingi siku hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Daniel Masolwa amesema Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeshaandaa sensa ya majaribio ambayo inahusisha mikoa 13 nchini na kwamba zoezi linakwenda kwa mafanikio makubwa.

Masolwa ametaja lengo la majaribio hayo ni kupima na kuhakiki vitendea kazi kama vitakuwa na changamoto virekebishwe kabla ya kazi yenyewe ambayo alisema inafanywa na umakini na watu wenye mafunzo na weledi.
 
Au ndio utendaji wa tofauti, mwenzake alikuwa anakwenda kukagua miradi na kuangalia value for money, huyu ni kuzindua na kucheza movie, hataki kuumiza kichwa kabisa.
 
Kwani Tanzania imefanya sensa ngapi tangu tupate Uhuru?

Hizi sensa za majaribio ni za nini?

Inamaanisha hafufahamu namna ya kuhesabu watu nchi nzima?

Kwanini fedha za majaribio zisitumike kutengeneza vipeperushi na kampeni kwenye runinga na magazeti?

Wananchi wameelimishwa ipasavyo maana ya sensa ili wajitokeze kwa wingi?

Au ndo upigaji waendelea?
 
Au ndio utendaji wa tofauti, mwenzake alikuwa anakwenda kukagua miradi na kuangalia value for money, huyu ni kuzindua na kucheza movie, hataki kuumiza kichwa kabisa.
Siyo wote wanakuwa na namna moja ya kutenda. Jpm alikuwa anaenjoy sana kwenda kule kwa sababu gats za kwenda nje hana japo alikuwa anatamani ila kingereza ndo kilimpiga chenga. Pili uongozi mzuri ni ule wa kuelekeza surbodinates wafanye siyo wewe kukimbizana na mitaa na vitongoji kisa wakuone eti umependeza.
 
Back
Top Bottom