Rais Samia kuwa mgeni rasmi Mkutano wa Vyama vya Siasa - Desemba 16

Mbowe wasipomwachia tareh 14 Dec basi nitajua kuwa mama kajiandaa kushindwa.
THE LOST
Dogo hiyo ilikuwa Kesi Ndogo ndani ya Kesi Kubwa. Hii Kesi Ndogo ilikuwa kujua kama washtakiwa waliteswa wakiwa mikononi mwa Polisi ama la. Baada ya hukumu ya tarehe 14/12/2021, kesi inarudi Mahakama Kuu ambako kuna Kesi ya Ugaidi ambapo mtuhumiwa ni Mbowe na wenzake. Ushanfahamu?
 

Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa vyama vya siasa pamoja na wadau mbalimbali wa siasa.​


Mkutano huo ambao awali ulitakiwa kufanyika Oktoba 21, mwaka huu lakini ukahairishwa, imeelezwa kuwa utafanyika Desemba 16 na 17, mwaka huu jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Desemba 4, 2021 Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya siasa, Juma Ally Khatib amesema mkutano huo utatanguliwa na semina kwa wajumbe wa baraza la vyama vya siasa kuhusu historia na majukumu ya baraza hilo, ambayo itafanyika Desemba 15.

Khatib amebainisha kuwa mkutano huo utakuwa na mada tatu zinazohusu masuala ya kisheria, demokrasia, siasa, uchumi na maadili ya kitaifa, yanayohusiana na demokrasia ya vyama vingi vya siasa.

"Baraza la vyama vya Siasa linatumia fursa hii, kushauri vyama vya siasa vyote vyenye usajili kamili, kuhudhuria mkutano huo, kwani ni fursa adhimu ya kubadiishana mawazo kuhusu mambo yanayotuhusu. Siasa ni ushawishi na ushawishi hufanikiwa kapitia njia ya mijadiliano," amesema Khatib.

Naye mwanasiasa Mkongwe na Mjumbe wa baraza la vyama vya siasa, John Cheyo ametoa wito kwa watanzania pamoja na serikali kuendelea kudumisha Uhuru na umoja.

"Nawaomba vijana na Watanzania tuipende nchi yetu na tumlaani mtu yoyote anayedhihaki nchi. Pia naiomba serikali iendelee kudumisha uhuru na umoja katika Taifa letu kupitia baraza la vyama vya siasa... wale wanasiasa wanaohamasisha vitu vya ajabu huwezi kupata kwa njia hiyo unayoitaka, hata Mwalimu Nyerere aliipata nchi hii kwa njia ya mazungumzo," amesema Cheyo.

Mwenyekiti wa kamati ya maadili na mahusiano wa baraza hilo, Doyo Hassan Doyo amesema baraza hilo liko kisheria hivyo linauwezo wa kutatua na kuondoa matatizo ambayo yanavikabili vyama vya siasa.

"Kwahiyo nitoe wito mwanasiasa yeyote atakayekiuka taratibu na sheria, tutamuwajibisha kwa mujibu wa sheria na kanuni ambazo tumejiwekea. Hivyo tunatoa wito viongozi wasiwe maneno ya maudhi kwa wengine, viongozi wa nchi pamoja na usalama wa Taifa," amesema Doyo.
Covid 19 watawakilisha ccm B
 
Ni mkutano wa kipuuzi kabisa.
Hauna maana wala mantiki.

Hivi kulikuwa na ulazima wa kumualika Samia kuwa mgeni rasmi?
Ni vipi Samia awe mgeni rasmi wakati yeye ni mdau wa kawaida kwenye huo mkutano?
Mama Samia ni mwenyekiti wa CCM, chama ambacho ni sehemu ya ushiriki wa mkutano wa vyama vya siasa, sasa kualikwa kama mgeni rasmi ni ili kuja kuwaasa nini wakati yeye mwenyewe anapaswa kuwa mjumbe wa mkutano huo ili kuaaswa?
 
05 December 2021

Mjadala ,Vikwazo vya Kimataifa muhimu

Mbinyo wa Jumuiya yaz Kimataifa ni dawa mujarabu kwa tawala dhalimu, ulifanikiwa kuibana Serikali ya Kibaguzi South Africa, imeweza kuibana Zimbabwe...


 

TOKA MAKTABA 2019​

Tanzania Yaitaka Dunia Kuiondolea Vikwazo vya Kiuchumi Zimbabwe Bila Masharti​




Na Mwandishi wetu,
Tanzania imelaani vikali vikwazo ilivyowekewa nchi ya Zimbabwe na kuitaka dunia kuiondolea nchi hiyo vikwazo hivyo bila masharti kwani haviaathiri tu Zimbabwe bali huathiri pia nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)
Kauli ya kulaani vikwazo hivyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati alipokuwa akiwasilisha mada katika kongamano maalum kuhusu “vikwazo vya kiuchumi na hatma ya Afrika: Uzoefu wa Zimbabwe” leo Jijini Dar es Salaam.

Prof. Kabudi alisema kuwa kitendo cha dunia kuiwekea vikwazo nchi ya Zimbabwe, hakuiathiri tu Zimbabwe bali hata nchi wanachama wa SADC.

“Tulikubaliana katika mkutano wetu wa mwezi Augosti kuwa leo tarehe 25/10/2019 kuiambia dunia kuiondolea Zimbabwe vikwazo vya kiuchumi ilivyoviwekea bila masharti..…leo siyo siku ya kuomba wala kukumbushana bali leo ni siku ya kuiambia dunia rasmi iiondolea Zimbabwe vikwazo vya kuichumi” Alisema Prof. Kabudi

Waziri Kabudi aliongeza kuwa “vikwazo ilivyowekewa Zimbabwe ni batili na kama Marekani na Umoja wa Ulaya wana hoja ya msingi wapeleke azimio katika baraza kuu la umoja wa mataifa na ndiyo maana katika mkutano wa SADC tuliazimia kulaani vikali Zimbabwe kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na kuitaka dunia kuiondelea Zimbabwe vikwazo hivyo bila masharti,”.
 
Toka Maktaba :
01 August 2019

U.S. blacklists Zimbabwe officials over human rights abuse​


File photo : Brigadier-General Anselem Sanyatwe was the tactical commander.

(Reuters) - The United States on Wednesday imposed sanctions on Zimbabwe's state security minister and its ambassador to Tanzania, the U.S. Treasury Department said, accusing them of human rights abuses, including directing an attack on peaceful protesters.

Owen Ncube, Zimbabwe's state security minister, was blacklisted over accusations that he ordered security services to abduct and mistreat members of the opposition group, the Treasury Department said in a statement.

The Treasury Department said it imposed sanctions on Anselem Sanyatwe, Zimbabwe's ambassador to Tanzania, accusing him of directing security forces to attack protesters during demonstrations after the 2018 elections, when he was commander of the National Army's Presidential Guard Brigade

Read more : U.S. blacklists Zimbabwe officials over human rights abuse

Read more : Anselem Sanyatwe Biography: Wife, Career, August 1 Shootings -Pindula, Local Knowledge
 
https://www.nytimes.com › sanction...
Sanctions Were Crucial to the Defeat of Apartheid - NYTimes.com

19 Nov 2013 — When the Comprehensive Anti-Apartheid Act of 1986 imposed economic sanctions against the apartheid regime of South Africa (over.....



Read More :

SANCTIONS AGAINST SOUTH AFRICA​

The charismatic Anglican bishop, Desmond Tutu, rallied western support with his call for a boycott of South Africa, primarily through economic sanctions. The administration of Ronald Reagan opposed formal sanctions, preferring to exert quiet pressure to speed up reform. But the demand for sanctions could not be quieted, and in 1986 Congress overrode a presidential veto to ban the importation of South African goods and prohibit American business investments in South Africa.

While some critics believe the sanctions were more symbolic than anything else, others claim that they did contribute to rapid political change in South Africa. In 1990 President F.W. de Klerk released Nelson Mandela after twenty-seven years of imprisonment, opened negotiations with the ANC and scrapped most of the apartheid laws. In 1992 a strong majority of the country's white population voted to endorse de Klerk's dismantling of apartheid and the extension of political rights to the black majority. When this happened, President Bush lifted the economic sanctions, claiming that the purpose of the bill had been successfully carried out.

For further reading: Margaret P. Doxey, Economic Sanctions and International Enforcement (1980); Richard A. Falk, Samuel S. Kim and Saul H. Mendlovitz, eds., The United Nations and a Just World Order (1991).


SANCTIONS AGAINST SOUTH AFRICA​

Title I -- Policy of the United States with Respect to Ending Apartheid

Policy Toward the Government of South Africa

Sec. 101. (a) United States policy toward the Government of South Africa shall be designed to bring about reforms in that system of government that will lead to the establishment....... READ more source :
 
https://www.latimes.com › archives
ANC Chief Calls On Nations to Pressure Pretoria With Stiffer ...


2 Dec 1987 — ... called on Tuesday for intensified sanctions against South Africa to ... But Julius K. Nyerere, one of Africa's elder statesmen as the ...

“There will come a time when the South African racist regime and its military will accept that such a racist government is no longer possible,” Nyerere told the conference. “They will then accept that negotiations must take place with the people’s leaders.”

Source : ANC Chief Calls On Nations to Pressure Pretoria With Stiffer Sanctions
 
Ni vizuri chadema wakashiriki huu mkutano, jukwaa zuri la kutoa changamoto
Wasingekuwepo John Cheyo na Shibuda sawa. Hayo maajenti wa shetani kijani yatatumika kuvuruga agenda ya kikao. Hakuna sababu ya kupoteza muda kwa kikao kisichokuwa na tija.
 
Hapa naona Rais SSH wanamsumbua tu kumwalika kwenye miavuli ya Vyama vya Siasa ambayo haina nguvu yoyote..
Mwavuli huu bila CHADEMA, ACT-Wazalendo,NCCR Mageuzi hausaidii kitu kwani hauna ushawishi wowote..
Aagize kesi ya Mwenyekiti Mbowe ifutwe kwanza halafu mengine yaendelee..
 
Back
Top Bottom