Rais Samia kuwa makini, una upinzani ndani ya CCM yako

Analijua hilo...hata Urais walitaka wamruke....CCM si watu...leo hii wanamkana mwendazake kana kwamba hakuwa jamaa yao...hawa watu siyo kabisa
 
Kwanza nikupongeza sana kwa kuupiga mwingi mpaka unaotea. Kwa wale waliokaa Tabora wanajua hadithi ya mcheza maarufu wa mpira wa miguu kutokea mkoani humu YUNGE MWANA NSALI huyu inasemakana alikuwa anauwezo wa kupiga faulo akikonga mwamba inaenda kufunga upande wao.

Mama unapigiwa kila aina ya hadithi na simulizi na huku vifijo vikiwa kwako.

Tunaambiwa unaupiga mwingi sijui upi huo maana upinzani haupo Bungeni na mtaani umeurudisha tunduni utulie kwanza maana unalima shamba hawa ndsge upinzani wanaweza kupekua mbegu na kuzila na shamba letu UCHUMI likanyauka.

Kuna maneno yanapita eti wengi ndani ya mfumo walikuwa hawataki uwe kiongozi mkuu mara baada ya kiongozi wetu mpendwa(sio kwa wote) JPM afariki dunia yanasemwa mengi hatimaye umechukua utawala na uongozi. Kama kweli yapo kwanini unaendelea kufanya makosa na unakibali kuchonganishwa na Rai wako?

Kuna haja gani kila kitu kikitoka serikalini kwako Wananchi wanakipinga? Kulikuwa na ulazima gani wa kufanya kazi na Nchemba ama Ndugulile hawa mliwafukuza katika ile Awamu ya Tano kuna kipi kinakufanya uwaamini hawa. 2025 si mbali ni mola kutupa pumzi ya kutosha tunaingia katika patashika ya uchaguzi mkuu.

Nakuhakikishia mimi ukiendelea kukumbatia Wagombea wenzio ndani ya serikali yako tegemea Wazalendo wanyonge watakupa salaam zao.

Tunakwenda kufanya uchaguzi wa kizazi kipya kinachotumia mitandao inakuwaje sehemu waliozaliwa wanaijua wewe una ruhusu ichezewe.

Mtoe Nchemba mpe hata wizara nyingine tofauti na hiyo wizara ya Fedha huyu Nchemba kumbuka 2015 mlisumbuana nae kiasi cha kuchafua utalii wa ndani kwa kupaka mawe majina yake.

Kama una mapenzi na Watanzania angalia watu wa kufanya nao kazi ndani yako humo una vifutu na Kobiko wametulia tu wanachofanya wanakuchonganisha na raia.

Unaupiga mwingi usije kuwa kama YUNGE.

Kitakacho muokoa Rais Samia ndani ya CCM ni chama Cha mapinduzi mwaka 2025, kuprint fomu moja tu ya mgombea wao. Vinginevyo kuna mtifuano mkubwa ndani ya chama, ambapo kupata zile asilimia zao 99.9% itakuwa ni miujiza.​

 
Bora mama kuliko yule muuaji !!! Watz wenye akili wanamkubali mama samia ila wapumbavu kutoka kanda ileeee wanamchikia
Kwa akili yako unajidanganya wote wanao mpinga ni wakanda ile,basi wewe ndio mpumbavu wa dunia,halfu usilazimishe tumkubali wtz wote, kama wewe ni mnufaika kaa kimya, nyie ndio mnasababisha tuletewe makodi ya hovyo hovyo.
 
Haya makundi yameibuka lini mbona mwendazake aliyasiginia mbali chama kikawa kimoja? Mama ataendelea na awamu ya pili, isiwe kama yule spika aliyeongoza muhula mmoja
 
Hizi nafasi zenye msamaha wa kodi zinagombaniwa. Suluhisho ni wote tulipe kodi kwa maendeleo ya nchi yetu.
 
Back
Top Bottom