Rais Samia kutua Arusha Kwa ziara ya Siku mbili

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
693
1,000
Rais wa jamhuri ya Muungano Tanzania ,Samia Suluhu Hasani anatarajiwa kuanza ziara ya siku mbili katika Mkoa wa Arusha kuanzia oktoba 16 mwaka huu.

Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongela alisema kuwa Rais Samia akiwa Mkoani hapa atatembelea na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuongea na wananchi .

Alisema kuwa Rais Samia atawasili mkoani hapa oktoba 16 mwaka huu jioni na kupokelewa na uongozi wa mkoa.

Alisema oktoba 17 Rais Samia atatembelea Mradi wa Maji uliopo chekereni wilaya ya Arumeru ambao ni sehemu ya Mradi mkubwa wa Maji unaoendelea wenye thamani ya sh, bilioni 520.

Pia siku hiyo atazindua mradi wa hospitali ya wilaya iliyopo Engutoto jijini hapa unayojengwa na fedha za ndani za Halmashauri ya jiji la Arusha.

"Baada ya uzinduzi huo Rais Samia anatarajia kuhutubia umati mkubwa wa wananchi katika uwanda wa mpira wa sheikh Amri aberd "alisema

Mkuu huyo wa mkoa aliongeza kuwa siku inayofuata oktoba 18 ,Rais Samia atazindua kiwanda Cha Nyama Cha Elia Food Overseas LTD kilichopo Namanga wilayani Longido.

Mongela alisema baada ya uzinduzi huo Rais ataelekea Makao makuu ya wilaya ya Longido Kwa ajili ya kuzindua Mradi Mkubwa wa Maji .

"Katika ziara hiyo Rais Samia atahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika uwanja wa kituo Cha mabasi wilayani Longido "Alisema Mongela

Mkuu huyo wa mkoa alitoa Rai Kwa wananchi kujitokeza Kwa wingi kumlaki kiongozi huyo ambaye ameleta miradi mingi mikubwa katika Mkoa wa Arusha.

IMG_20211014_111059_504.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom