Rais Samia kutoipa kipaumbele ikulu ya Dodoma: Je, kuhamia Chamwino ilikuwa matakwa binafsi ya Hayati Magufuli?

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,730
10,033
Katika hali za sintofahamu juu ya utendaji wa tofauti sana kati ya rais wa sasa na yule aliekuwa mtangulizi wake, kwa muda mchache sana tumeona mengi yakibadilishwa kwa kasi ya kimbunga.

Huku wengine wakihoji vipi mahusiano yao ya awali kati ya rais SSH na JPM kiushirikiano yalikuwaje kwa undani zaidi?

Kwa matukio mengi ya kiserikali hivi yamekuwa yakifanyika katika ofisi ya ikulu ya Dar na ukimya ukitanda kuhusu maendeleo ya Chamwino.

Sasa je, uamuzi ule wa kuhamisha ikulu toka Dar mpaka Dodoma ulifanywa na hayati pekee bila kushirikisha ngazi nyingine iliyo pembeni yake na wengine hawakupendezwa na maamuzi hayo?
 
Kutoka kwenye sorces zisizo na uhakika zilisema kuwa.

Alikimbia kwa sabbu system zilikuwa hacked ...yaliyokuwa yafanyike/kutangazwa tayari yalikuwa yameshafika mitandaoni.

Hoja ya mapepo,Sina uhakika.

Yote kwa yote alitaka kuidhinisha kazi iliyoanzishwa na muasisi Baba wa Taifa kuhamia Dom

Pia Magogoni ni Ikuku ndogo kama zilivyo nyingine mikoani.Nahisi next time atakuwa pale kwa wenzetu wa Kigoma kuapisha wakuu wa wilaya

Kwa upande wa Mama,ni mapema sana tumpe muda.

Yote kwa yote, huwa pia nawaza na kuwazua kuwa endapo akipatikana Raisi wa awamu nyingine nae pia atakuwa anaenda Magogoni?
Hiyo neno mapema umeandika kimahaba tu, sema ukweli wako, wee si kidume?
 
Huwezi kusema ulikuwa mpango binafsi wa JPM huku awamu zote za Serikali zilikuwa zinajua kuwa yawapasa kuhamia Dodoma ila muda na rasimali vilikuwa vikwazo.

Mthubutu akaja kifanya japo nafahamu bila uwepo wa JPM Serikali kuhamia Dodoma lingechukua miaka 100 kuja kutekelezwa.
 
Sasa je, uamuzi ule wa kuhamisha ikulu toka Dar mpaka Dodoma ulifanywa na hayati pekee bila kushirikisha ngazi nyingine iliyo pembeni yake na wengine hawakupendezwa na maamuzi hayo?
Kuna jamaa aliwahi kuona mkia wa mbwa ulipo, kisha akaniuliza, Mbwa anananihii kwa kupitia wapi?
 
Ujenzi wa Ikulu Mpya Jijini Dodoma ulikuwa ni moja ya muendelezo tu wa matumizi mabaya ya fedha za umma uliofanywa na marehemu! Ile Ikulu ya zamani ilikuwa inatosha kabisa.

Yaani ni sawa tu na ule ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa kule Chato! Wananchi wanataabika, mzee alikuwa anatapanya tu kodi zao kwa kujenga white elephant projects.
 
Huwezi kusema ulikuwa mpango binafsi wa JPM huku awamu zote za Serikali zilikuwa zinajua kuwa yawapasa kuhamia Dodoma ila muda na rasimali vilikuwa vikwazo..!!

Mthubutu akaja kifanya japo nafahamu bila uwepo wa JPM Serikali kuhamia Dodoma lingechukua miaka 100 kuja kutekelezwa.
Mkuu watu wanamtuhumu Jiwe kuwa yale yalikuwa ni maamuzi yake binafsi kwani aliwahi kutamka hadharani kuwa " Ufisadi mkubwa ndani ya Serikali uliofanywa na Watendaji Wakuu wakiwemo Watangulizi wake wengi waliwekeza ndani ya Jiji la Dsm especialy kwenye majengo. Na majengo yale walipangishiwa Mashirika mbali mbali ya Kimataifa na Idara pamoja na Taasisi mbali mbali za Serikali. Sasa naiondoa Serikali yangu na kuipeleka Dom kama ilivyoasisiwa na Nyerere. Kisha nione haya majengo ya Mafisadi watayafanyia nn". Full kuwakomoa.

Ninachokiona mimi ni kwamba Serikali haiamini ktk "Uchawi" lkn Serikali hiyo hiyo Watendaji wake ni Binadamu wenye Imani tofauti tofauti. Mshana Jr atakuwa kanielewa.
 
Katika hali za sintofahamu juu ya utendaji wa tofauti sana kati ya rais wa sasa na yule aliekuwa mtangulizi wake, kwa muda mchache sana tumeona mengi yakibadilishwa kwa kasi ya kimbunga.

Huku wengine wakihoji vipi mahusiano yao ya awali kati ya rais SSH na JPM kiushirikiano yalikuwaje kwa undani zaidi?

Kwa matukio mengi ya kiserikali hivi yamekuwa yakifanyika katika ofisi ya ikulu ya Dar na ukimya ukitanda kuhusu maendeleo ya Chamwino.

Sasa je, uamuzi ule wa kuhamisha ikulu toka Dar mpaka Dodoma ulifanywa na hayati pekee bila kushirikisha ngazi nyingine iliyo pembeni yake na wengine hawakupendezwa na maamuzi hayo?
Mbona hiyo ipo tokea Nyerere,hayo sio matakwa ya Magufuli ila Magufuli alikuwa anatekeleza matakwa ya Nyerere.
 
Katika hali za sintofahamu juu ya utendaji wa tofauti sana kati ya rais wa sasa na yule aliekuwa mtangulizi wake, kwa muda mchache sana tumeona mengi yakibadilishwa kwa kasi ya kimbunga.

Huku wengine wakihoji vipi mahusiano yao ya awali kati ya rais SSH na JPM kiushirikiano yalikuwaje kwa undani zaidi?

Kwa matukio mengi ya kiserikali hivi yamekuwa yakifanyika katika ofisi ya ikulu ya Dar na ukimya ukitanda kuhusu maendeleo ya Chamwino.

Sasa je, uamuzi ule wa kuhamisha ikulu toka Dar mpaka Dodoma ulifanywa na hayati pekee bila kushirikisha ngazi nyingine iliyo pembeni yake na wengine hawakupendezwa na maamuzi hayo?
huyu mama anakoelekea hata haeleweki, anaongea sana utendaji ZERO......

yani yeye ni dsm, zenji, dsm zenji sijui kama anaelewa anachokifanya!
 
Back
Top Bottom