Rais Samia kushusha zaidi bei ya mafuta mwishoni mwa Desemba 2021

Kumbe alitupandishia makusudi tu sahivi anataka kuishusha, tumeshapigika mno
 
Baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuondoa Tshs 102 katika kila lita ya mafuta msimamo wa bei ya mafuta uliopo nchini bado haumpi usingizi mama huyu kwani bei ya mafuta ndio huamua gharama za maisha ya watoto hawa wa masikini ama zipande au zishuke au zisalie zilivyo.

Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutumia Shirika la mafuta nchini yaani TPDC ( Tanzania Petroleum Development Corporation ) sasa tutaagiza mafuta moja kwa moja toka Visimani hii ikiwa ni baada ya Waziri wa nishati Mhe January Makamba kufanya ziara ya kiserikali kwenye nchi zinazochimba mafuta za Saudi Arabia, Algeria na UAE.

Nia ya Serikali ya awamu ya Sita nikuhakikisha kila Mtanzania anaishi maisha yake kwa gharama ndogo iwezekanavyo ili awe na ziada kwaajili ya maendeleo yake ya kimwili, kiroho na maendeleo ya vitu hakika tumempata Rais mwenye Uchungu wa kweli wa maisha ya watu wake ambao wengi wao ni watu wa kipato cha chini sana.

Tanzania kwa mwaka inaagiza wastani wa Jumla ya lita za mafuta 3.5BL kwa kutumia makampuni binafsi kwa mtindo wa Bulk Procurement System ( BPS ) yaani kwa malundomalundo mtindo ambao uliwapa faida zaidi wawekezaji na kuumiza zaidi walaji wa mwisho alichokifanya Rais Samia sasa ni kupindua meza.

Wamiliki hao wa Visima vya Mafuta wameonesha nia pia ya kujenga Visima bandia vya mafuta hapa nchini kwaajili ya kuhifadhi mafuta yao na kuzisambazia nchi zote za maziwa makuu hakika Tanzania tunakwenda vizuri sana.

Tanzania ni salama sana na Samia
 
Kwa speed hii ya Rais Samia, Tanzania huenda ikaibua mabilionea wapya 100 miaka miwili ijayo,Tufanye kazi kwa bidii zaidi
 
Team JF,


MERRY CHRISTMAS AND HAPPY NEW YEAR 2022.

#TUENDELEE KUMUUNGA MKONO RAIS WETU,
 
Miradi yote iliyoachwa na Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli Rais Samia Suluhu Hassan anaitekeleza kwa 100%

Sihiyo tu tayari mingine mipya inaendelea na Ujenzi,

Tunawajibu wa kumwombea Mama huyu,
 
Back
Top Bottom