Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,488
- 13,608
Ninamuelewa sana Rais Samia anaposema kuwa yeye na Hayati JPM walikuwa kitu kimoja. Kwamba ni maamuzi ya Hayati yaliyompa yeye nafasi ya kuwa mgombea mwenza.
Kwamba yeye na Hayati walihangaika majukwaani na wakapigwa na jua pamoja mwaka 2015 ili waingie ikulu, hivyo haupo uwezekano wa wao wawili kutenganishwa kiuongozi.
Baada ya kifo cha JPM wanaibuka watu na kumpaisha mpaka makamu wake anaonekana sio sehemu ya ufanisi wake wote wa kazi. Ni lazima Rais Samia akwazike kila anapoona anadharauliwa wakati ipo sehemu ya jasho lake katika hiyo heshima anayopewa kiongozi aliyetangulia mbele za haki.
Na Rais kusema kwamba yeye na Hayati ni kitu kimoja haina maana kwamba hata kama yalifanyika makosa basi yafumbiwe tu macho eti kwa kigezo cha kutoichafua kazi nzuri iliyofanyika.
Rais wa sasa afanye kazi kwa kutazama nini kinaweza kufanyika leo na kesho, afanye kazi kwa kutegemea nini haswa washauri wake wanasema.
Aitengeneze Tanzania akiwa na mitazamo kwamba zile dakika moja za watu kusimama kwa ajili ya kumkumbuka Hayati JPM zinapomalizika na watu kuwa wameshakaa vitini mwao, kila kinachofuatia kinasimamiwa na maamuzi yake mwenyewe, ambayo yatamhukumu yeye kama yeye mwaka 2025.
Yeye kuwa kitu kimoja na mtangulizi aliyelala usingizi wa milele hakumaanishi kuwa walichokifanya pamoja hakikuwa na udhaifu na wala hakistahili kurekebishwa pale inapobidi. Wakosoaji (critics) hawakwepeki, waliwakosoa mitume kina Mohamed na Yesu Kristo sembuse wanasiasa wanaoingia ikulu kwa kupigiwa kura!.
Ameongelea ATCL kutakiwa kuwa na wabunifu watakaokuja na mitazamo ya kibiashara zaidi, na utekelezaji wake uanze mara moja. Mashirika yote yenye kutakiwa kupeleka gawio hazina na yawe na aina ya watendaji wabunifu wenye kufanya kazi bila ya presha za kisiasa.
Kuna fursa nyingi tu ukanda ule wa mikoa ya Kigoma, Rukwa, Katavi, ukanda wote ule kwa kuambaa usawa wa ziwa Tanganyika ni fursa tupu za kiuchumi. Ni mikoa yenye utajiri mwingi lakini bado haijaanza kuchangamka. Uwekezaji unapolegezewa masharti yake, serikali ije na mpango mkakati wa kiuchumi wenye kuonyesha namna mikoa ile inavyoweza kuinuka.
Ajikite katika kuangalia namna ambayo bandari inayopanuliwa kule Mtwara itakavyoweza kulitumia vyema soko la Malawi na Zambia. Namna ambavyo bandari ya Tanga inaweza kuwa na mzigo wa uhakika, siku zijazo ambazo pengine corona itakuwa imepatiwa ufumbuzi.
Rais Samia afanye kazi pasipo kuwafikiria wale wote wanaomlinganisha na Hayati. Hawezi kufanana na Hayati na hana sababu ya kuwa mtumwa wa mitazamo au maoni ya wenye kumlinganisha nae. Awe na nafsi huru kila anapoingia ofisini asubuhi, anapofanya kazi mchana kutwa na jioni wakati anaondoka.
Binadamu hajawahi kuridhika tangu aanze kuishi juu ya ardhi na hatakuja kuridhika. Na hatakuja kuzaliwa mwanaume au mwanamke mwenye kipawa cha kumridhisha kila anayemzunguka.