Rais Samia, kuna dalili zote za kuwa na mafuta ziwa Tanganyika na Nyasa

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,141
18,769
Moderators wa JF mnazingua sana. Mmebadilisha kichwa cha thread na kutoka nje kabisa ya topic. Lengo haikuwa kusema kuna dalili za mafuta, bali kuweka mkazo kwamba lazima tuharakishe ku-utilize hii resource kwa kuwa kuna kasi ya kuacha kutumia mafuta duniani. Kwa nini mnafix vitu ambavyo havina tatizo, na kuishia kuharibu? Ndio maana kuna wakati niliacha kabisa kuandika thread kwa ajili ya mambo yenu kama haya


Raisi Samia, kuna dalili zote za kuwa na mafuta ziwa Tanganyika na Nyasa. Tusipoyachimba ndani ya miaka kumi ijayo hayatakuwa na faida tena kwetu

Raisi Samia, nadhani una taarifa kwamba kuna kila dalili za mafuta ndani ya Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa. Hakuna maendeleo yaliyofanyika kuchimba mafuta katika maeneo haya kutokana na vikwazo viwili;
  1. Upande wa ziwa Tanganyika kuna kikwazo cha waasi wa DRC. Si rahisi kuendeleza mradi wa mafuta ziwani Tanganyika ikiwa waasi hawa wa DRC hawajaondolewa kabisa. Na mafuta haya yataendelezwa kwa ushirikiano kati ya Tanzania na DRC, ndio maana Tanzania ilikuwa tayari kupeleka jeshi DRC kusaidia kuondosha waasi ili tuchimbe haya mafuta kwa ushirikiano na DRC. Inaonekana zoezi la kuondoa waasi limekwama, na hiki kimekuwa kikwazo.
  2. Upande wa ziwa Nyasa kuna mafuta. Lakini pindi ilipoonekana Ziwa Nyasa lina mafuta tuliingia katika mgogoro wa mpaka kati yetu na Malawi. Wakijua rasilimali ya mafuta iloiyomo ziwani, Malawi walianza kudai ziwa Nyasa lote liko upande wa Malawi na ndio maana wao wanalitambua kama Ziwa Malawi. Nilipendekeza humu JF kwamba tuachane na suala la mgororo wa mpaka na jirani zetu Malawi tukubaliane nao kwamba rasilimali yoyote ya mafuta ndani ya ziwa tutagawana 50/50 bila kujali iko upande gani. Sijui kama nilisikilizwa.
Sasa kuna tatizo. Kutokana na tatizo la mabadiliko ya mazingira (climate change), mataifa makubwa duniani yameweka mkakati wa kuacha kutumia mafuta kwa ajili ya magari na mitambo. Norway kwa mfano, wanasema kufikia 2050 wataacha kabisa shughuli za kuchimba mafuta. Uingereza wanasema watapiga marufuku magari ya kutumia diesel kufikia 2025 nadhani. Japan, Germany na hata China, wote wanasema ndani ya miaka 15 ijayo wanataka kutoka kwenye kutumia mafuta kwenye magari na kuingia kwenye magari ya umeme (from internal combustion engines to electric vehicles)

Sasa hii inamaanisha nini kwa nchi kama Tanzania ambazo hadi sasa zimekalia tu uchumi wa mafuta bila kuuendeleza? Ina maana ndani ya miaka 20 ijayo, mafuta yatakuwa si mali kitu. Hata ukigundua una mafuta mengi kama bahari ya Hindi, hayatakusaidia tena kwa kuwa dunia imeanza kuondoka toka tekinolojia ya mafuta kwenda teknolojia ya umeme!

Hivyo basi, kama kweli tunataka kufaidika na rasilimali ya mafuta tuliyonayo, ni lazima iendelezwe ndani ya kipindi cha miaka kumi ijayo. La sivyo haya mafuta yatakuwa na rasilimali isiyohitajika tena duniani, na ndani ya kipindi cha miaka kumi ijayo tutaanza kushuhudia kuporomoka kwa bei ya mafuta kadiri magari ya umeme yanavyoingia sokoni. Leo hii hata Lamborghini wamesema wataacha kutengeneza gari za mafuta!

Kwa hiyo kaza mwendo tuweke mkakati wa kuchimba mafuta Lake Tanganyika na Nyasa. Tatua changamoto zinazokabili maeneo haya. Waambie TPDC waache ku-weka areas with the highest oil potential for last. Ikiwezekana, wafanye mkupuo mmoja wa kugawa vitalu vya kufanya oil and gas exploration kwa nchi nzima, time is of essence, waache mwendo wa bata.

Tukiweza kuchimba mafuta ndani ya miaka kumi ijayo, yatachangia sana kuinua uchumi wetu, tutakuwa na barabara za rami hadi vijijini! Tukichelewa, haya mafuta hayatatusaidia, yatakuwa obsolete resource!

Angalia pia:

Suluhisho la mgogoro na Malawi ni hili; sio suala la ziwa wala mpaka

Suala la uwepo wa mafuta katika ziwa Nyasa na kusababisha mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi limeishia wapi?

Katika awamu hii chini ya Rais mpya Malawi, Magufuli atumie fursa hii kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania
 

Denmark says it will stop new oil and gas extraction from the North Sea​


By Laura Sanders with AP • Updated: 04/12/2020

Denmark says it is putting an end to the fossil fuel era by stopping all new oil and gas exploration in the North Sea.
It has cancelled its latest licencing round - a process which grants firms permission to search for and extract oil and gas.

Fossil fuel extraction will stop by 2050.
 
1621414857755.png

Read more: 2030 ban of new petrol and diesel cars: what will it mean for you? – Which? News - Which?
 
Kwa huu mwendo wetu wa kijinga kuingia mikataba ya miaka 99 na wawekezaji! basi tuchukulie tu kwamba extraction ya mafuta kwetu haina tija.
Yaani uwepo wa mafuta nchini mwetu ni sawa na kumiriki tenga la samaki waliooza!
 
Ulimwengu wa 3 bado watatumia sana mafuta. Kwani kuna shida gani tukizalisha mafuta tutumie wenyewe.
Na hayo magari ya kutumia mafuta mtatengeneza wenyewe? Na spare zake?

Na kuchimba mafuta kwa ajili ya soko la ndani ya nchi peke yake is not economical
 
Kwahiyo mpaka lami itatengenezwa kwa kutumia umeme

Biashara ya mafuta ni kubwa sababu ya magari na vyombo vya usafiri, by that time biashara itakuwa ndogo kama matumizi yenyewe yatakuwa Lami na sijui Mbolea.
 
Hapo ziwa Nyasa umeongea utopolo tu, sheria za kimataifa zinasema, mnapotenganishwa na chanzo cha maji, basi mpaka unapita kati kati, na hilo huwa halina mjadala.
Watu kama wewe ndio mnaoturudisha nyuma. Mnagombea mbuzi, hamumpeleki malishoni kutokana na ugomvi wenu hadi anakufa.
 
Kwa huu mwendo wetu wa kijinga kuingia mikataba ya miaka 99 na wawekezaji! basi tuchukulie tu kwamba extraction ya mafuta kwetu haina tija.
Yaani uwepo wa mafuta nchini mwetu ni sawa na kumiriki tenga la samaki waliooza!
Kwahiyo hiyo ndio condition kwa wawekezaji wote?
 
Watu kama wewe ndio mnaoturudisha nyuma. Mnagombea mbuzi, hamumpeleki malishoni kutokana na ugomvi wenu hadi anakufa.
Uki-give in katika suala moja, basi na wengine wote wanapata picha kwamba huyu tukimtikisa huwa ana-give in, na hapo wote wataanza kukusumbua, hadi Kenya atasema mlima Kilimanjaro ni wake, na ataleta mikataba yake ya kikoloni anayoijua yeye, lazima uwe na principles.
 
Uki-give in katika suala moja, basi na wengine wote wanapata picha kwamba huyu tukimtikisa huwa ana-give in, na hapo wote wataanza kukusumbua, hadi Kenya atasema mlima Kilimanjaro ni wake, na ataleta mikataba yake ya kikoloni anayoijua yeye, lazima uwe na principles.
Hiyo ndio ilikuwa philosophy ya Magufuli ambayo Samia anajaribu kurekebisha kwa kuwa ilituharibia nchi sana!
 
Mafuta yatatumika kuendesha Mitambo y kuzalisha umeme, Mfano Generators, kwahiyo usijali msee
Hio Mali haina expire date
Unadhani gharama za kuchimba na kuendesha visima vya mafuta ni kama vile visima vya maji mlivyochimbia huko kijijini kwenu?

Yaani lojiki unayoleta ni sawa na kusema hakuna tatzizo, tutatengeneza Dreamliner zetu zitumike kama daladala Dar es Salaam
 
Hoja ya waasi wa DRC kuwa sababu ya kutochimba mafuta ziwa Tanganyika haina mashiko, mbona Total wame-exprole gas Ziwa Tanganyika upande wa DRC? Labda ziko sababu nyingine.

Vv
 
Na hayo magari ya kutumia mafuta mtatengeneza wenyewe? Na spare zake?

Na kuchimba mafuta kwa ajili ya soko la ndani ya nchi peke yake is not economical
Ndio maana mleta hoja anasema yachimbwe haraka , ikiwezekana ndani ya miaka 10.

Vv
 
Back
Top Bottom