Rais Samia kumbuka haya na uyatafakari

Omutontozi

Senior Member
Nov 12, 2021
122
213
Nakusalimu mama!

Kwanza nakukumbusha methali isemayo "Ushikwapo Shikamana" Tangu lilipotokea janga la msiba wa Magufuli, katiba ilikutaka wewe ndo uwe Rais wetu lkn mazingira ya wewe kuwa rais hayakuwa mepesi, tunamshukuru mungu uliapishwa na kushika madaraka. Baada ya kuapishwa wana CCM wenzio hawakuwa tiyari kuona unakuwa rais, walitawaliwa na fikra dhaifu za mfumo dume hivyo ulikuwa umezungukwa na wanafiki.

Wananchi waliokuunga mkono kwenye kila hatua uliyopiga ni wafuasi wa upinzani hasa Chadema kwa kutumia kauli mbiu ya "MAMA ANAUPIGA MWINGI" walifanya hivo wakiamini wametoka kwenye minyororo ya Magufuli na wahuni waliokabidhiwa madaraka hivyo wakaona wewe ni mtu sahihi kuwaponya.

Kumbuka

Janga la corona wana-CCM wenzako walikupinga waziwazi, CHADEMA wakaungana na wewe kwa hatua ulizozichukua

Wana-CCM walishaaminishwa mwanamke hawezi kuongoza nchi, hivyo wengi walikupinga na bado wanakupinga lakini Chadema walikuunga mkono wakisema "UNAUPIGA MWINGI" hili unaweza usilijue kama sio mfatiliaji wa mitandao

Kumbuka wapinzani hasa CHADEMA walishakubali utendaji wako kuliko CCM wenzio wanakuona umepata urais kwa bahati nasibu na wanasema pengine ulihusika kummaliza Magufuli.

Nachotaka ujue ni kwamba wapiga kura wako 2025 wengi wangekuwa vyama vya upinzani kama usingegeuka na kuanza kuwafunga minyororo ile ile aliyokuwa akiwafunga Magufuli.

Zawadi pekee uliyowazawadia wapinzani baada ya kukuunga mkono katika magumu yote ni KUMPA MBOWE KESI HATARI YA UGAIDI. Mh. hii haitaleta afya katika utawala wako

Mungu akubariki, akuwezeshe kukumbuka fadhira za wapinzani.

Je, ile ahadi ya kukutana na wapinzani nani alikuzuia? Au muda bado? Huoni kwamba ni wadau muhimu kuleta utulivu katika serikali yako?
 
Kwenye hili la kumwekea Mbowe kesi za kusingizia Mama ameharibu Ile safari nzuri aliyoanza nayo. Nashauri aachane na hilo tendo la KISHETANI
Kwa Sisi Wakristo tunaamini kuwa kila jambo lina kusudi/maana toka kwa Muumba wetu. Kuna jambo linakwenda kutokea Tanz.
 
Back
Top Bottom