Rais Samia kukutana na Vyama vya Siasa Januari 3, 2022

kalacha mateo

Senior Member
Sep 27, 2021
118
237
Kauli ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu juu ya vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara aliyoitoa Desemba 2021.

Januari 3, 2023 atazungumza na viongozi vya vyama vya siasa juu ya hali na mwelekeo wa hali ya kisiasa nchini.
 
View attachment 2466771

Ujinga tu. Mwelekeo gani?. Maongezi mengi bila vitendo. Kuwafanya Viongozi wa upinzani Kama watoto. Kila siku vikao halafu mambo yapo vilevile.
 
Hivi hapo mwanzoni mbona mikutano ya kisiasa ilifanyika na nchi ilienda vizuri tu. Iweje Leo masharti na vikao vingi?. Kuna Nini?. Kama hawataki mikutano ya siasa waseme tuendeleee hivi hivi waje waruhusu wenyewe.

Yani Samiah anaturudisha mwaka 1992 na kipindi Cha 1995 kwenda 2005 wakati wa mkapa. Kulazimisha watu wote kuongea Yale ambayo Rais anataka . Angalia Leo watangazaji wamekuwa monitored haswa. Mfano Gerald Hando.
 
Yeye hana kosa maana amekuta utaratibu umeharibiwa kwaiyo hata kwa tulipofikia amefanya kazi kubwa sana katika suala la democrasia na amefanikiwa kuirejesha democrasia iliyokuwa imepotea kwa muda mrefu
 
..hata tofauti na kiongozi anayepiga marufuku kuendesha magari kwasababu kuna ajali za barabarani.

..vyama viruhusiwe kufanya mikutano. Atakayevunja sheria wakati wa mikutano hiyo achukuliwe hatua.

..mihadhara ya kukashifiana madhehebu ya dini ni hatari kwa jamii lakini imeruhusiwa.
 
Yeye hana kosa maana amekuta utaratibu umeharibiwa kwaiyo hata kwa tulipofikia amefanya kazi kubwa sana katika suala la democrasia na amefanikiwa kuirejesha democrasia iliyokuwa imepotea kwa muda mrefu
Hivi, rais kuvunja katiba sio kosa? Vyama vya siasa vipo kikatibq ya nchi na shughuli zake pamoja na taratibu na miongozo ya Sheria hiyo ya vyama vingi vya siasa nchini ipo na imeundiwa na chombo Cha kisheria Cha kuvilea yaani msajili wa vyama vya siasa.
Inakuwaje mtu mmoja kutoka chama Cha siasa chenye haki sawa na vingine kwa mujibu wa Sheria ya vyama vingi azuie vyama vingine kufanya kazi za siasa ikiwa ni pamoja na mikutano ya hadhara halafu mnamsifia?
Hii siyo sawa na hastahili kusifiwa badala yake aambiwe ukweli kuwa anakiuka katiba ya nchi Jambo ambalo ni kosa mbele ya Sheria.
Kama anaona sawa Basi apeleke mswada bungeni waifute Sheria ya vyama vingi.
 
Naamini atasema;

Aliyezuia mikutano Amefariki, tuheshimu maelekezo ya hayati!!!

Natania tu, 2022 Si 2023. Mambo ni moto.!!!!
 
Njama za kuiweka CCM

Wanapoteza mida tu yule Makamu wao amalizie mizunguko, kwa uhalisia, kumaliza Kampeni.

Pamoja na kujizatiti kwao-CCM- kwa kuongeza sanduku lao la fweza

Tunaenda kuona CCM pwaaa 2025.

Tusubiri misamiati
 
Kauli ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu juu ya vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara aliyoitoa Desemba 2021.

Januari 3, 2023 atazungumza na viongozi vya vyama vya siasa juu ya hali na mwelekeo wa hali ya kisiasa nchini.
View attachment 2466771
Hapa Tanzania vyama vya siasa ni viwili tu au vitatu tu. Ni Chadema, CCM na angalau Act. Vingine vinaangukia kwenye kundi la pili hapo juu
 
..hata tofauti na kiongozi anayepiga marufuku kuendesha magari kwasababu kuna ajali huwa zinatokeo.

..vyama viruhusiwe kufanya mikutano. Atakayevunja sheria wakati wa mikutano hiyo achukuliwe hatua.

..mihadhara ya kukashifiana madhehebu ya dini ni hatari kwa jamii lakini imeruhusiwa.
Mihadhara ya kidini kwa sababu haina maslahi ya ccm🤣🤣
 
Back
Top Bottom