Rais Samia kukomba Wawekezaji na Wafanyabiashara wakubwa wa Kimarekani kuja kuwekeza Tanzania

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,071
9,476
Ndugu zangu, Rais Samia Ni zaidi ya kiongozi, Ni zaidi ya Mwanasiasa,Ni zaidi ya mwanadiplomasia,Ni zaidi ya jasusi wa kiuchumi,Ni zaidi ya komandoo wa Vita ya kiuchumi, Rais Mama Samia Ni mchanganyiko wa hivyo vyote,Ni mjumuiko wa hayo yote, Ni muunganiko wa hayo yote, Ndani yake utayaona hayo yote,Ni Rais kweli kweliii,Ni Rais anayejuwa maana ya kiapo Cha Urais alicho apa, Anajuwa yupo hapo kwa ajili ya Tanzania na Watanzania,Anajuwa Nini anafanya, Nini anatakiwa afanye kwa ajili ya Taifa hili.

Rais Samia anajuwa kuzivuta fursa popote pale katika uso wa Dunia kwa ajili ya watanzania,Anajuwa kunasa mitandao ya kifursa kwa ajili yetu, Ndio maana tunaona ndani ya muda mfupi wa uongozi wake namna wawekezaji na watalii walivyo miminika na kutiririka hapa nchini, h ii yote ni kutokana na jitihada za kidiplomasia zilizofanywa na Rais Samia. Hii yote Ni kutokana na ushawishi alionao Rais Samia kitaifa na kimataifa,Hii yote ni kutokana na namna Rais Samia anavyokubalika na kuungwa mkono na watu mbalimbali,hii yote ni kutokana na heshima kubwa aliyojijengea na kulijengea Taifa letu katika Sura ya kimataifa ambayo imeifanya Tanzania kuaminika na kuwa chaguo namba moja la wawekezaji na watalii.

Sasa Rais Samia yupo Marekani kwa mualiko maalumu wa Rais Wa Marekani Joe Biden, Watanzania tutarajie mengi kutoka kwa Rais wetu,kitakuwa ni kishindo Cha mafuriko ya fursa nchini, Naamini anakwenda kuvuta wawekezaji na wafanyabiashara Wakubwa, Tutegemee na kutarajia fursa mbalimbali za kiuchumi kutiririkia nchini mwetu. Wapo viongozi wengi huko wa mataifa mengine,Lakini simuoni wa kushindana na Rais Samia kifursa,simuoni wa kuwakomba wawekezaji Zaid ya Rais Samia, simuoni wakumzidi ushawishi Rais Samia na Tanzania yetu,Tanzania Ni kubwa, Rais Samia Ni Maarufu na mashuhuri, huyu Ni Mama wa shoka,lazima vyombo vya habari vya kimataifa vitamani kufanya Naye mazungumzo ya masuala mbalimbali, lazima wawekezaji watamani kuonana na Rais Samia.

Rais wetu Mpendwa Ni Nyota iwakayo inayoweza kuwaongoza wavuvi Ziwani,Tanzania yetu lazima ing'ae ,lazima ivune fursa,lazima tunufaike na ziara hii ya Rais wetu, Lazima itikise na kutetemesha,lazima inase mabillioni ya kiuwekezaji kuja kwetu, lazima tupate madollar ya Kimarekani kupitia uwekezaji,lazima Tunufaike.

Ndugu zangu watanzania Rais wetu yupo kazini,sote tunamuona namna anavyoipambania nchi yetu,Tumuunge mkono na kumtia moyo,Tumpe Faraja na kumwombea Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia watanzania,Hakika tutafurahi wenyewe Kama ambavyo Tumeona Taifa likipiga Hatua mbele za kimaendeleo ndani ya muda mfupi katika kila Secta.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.:0742-676627
 
Ni vigumu mno. Hakuna mwekezaji atakuja kuwekeza pahala ambapo kuna sera zinazobadilika kulingana ni nani rais. Yaani tungejifunza kwa waarabu au wachina ingekuwa poa sana. Waarabu au wachina hawana ujinga wa eti demokrasia, wao lete uwekeze ila lazima tugawane faida. Ila bongo eti madini wanasomba mkisema mbane walipe kodi eti miga kumbe kuna wajinga fulani wana 10% na wamewekeza singapore kwenye real estate etc
 
Ni vigumu mno. Hakuna mwekezaji atakuja kuwekeza pahala ambapo kuna sera zinazobadilika kulingana ni nani rais. Yaani tungejifunza kwa waarabu au wachina ingekuwa poa sana. Waarabu au wachina hawana ujinga wa eti demokrasia, wao lete uwekeze ila lazima tugawane faida. Ila bongo eti madini wanasomba mkisema mbane walipe kodi eti miga kumbe kuna wajinga fulani wana 10% na wamewemeza singapore etc
Chini ya uongozi wa Rais Samia Naamini Hakuna muwekezaji atakaye juta kuwekeza Tanzania
 
Huyu hapa
20221214_194418.jpg
 
Nakuhakikishia kama hatujakuwa na msimamo ni ngumu sana kupata wawekezaji wa maana. Dkt Magufuli alikuwa mtu sahihi sana. We angalia Egypt inapiga hatua kwa sababu ya Rais wao mjeshi
Kinachowavutia wawekezaji Ni Sera nzuri na Bora za uwekezaji, mahusiano mazuri na wawekezaji ,siyo wanakuja kuwekeza halafu wewe unaanza kuwatisha,kuwatukana,kuwanyanyasa,usalama Wao kuwa mdogo.

Tanzania tuna amani na usalama wa kutosha ndio sababu mwekezaji yeyote atakayekuja Tanzania anakuwa na uhakika na uwekezaji wake kutokana na Hali y usalama kuwa nzuri na ya uhakika, lakini pia Ni katika wakati huu wa Rais Samia wawekezaji wanajuwa na kuwa na uhakika na usalama wa mitaji yao,hakuna anayewatishia Wala kuwatukana Wala kuwanyanyasa Wala kuwasumbua.

Kinachoangaliwa Ni wao wafuate Sheria zetu na kutimiza masharti ya kiuwekezaji,lakini pia kuona Tanzania inanufaika na uwekezaji wa aina yoyote Ile unaokuja nchini kwetu kwa kuhakikisha Kama nchi tunapata Kodi na fursa za kiuchumi ikiwepo uzalishaji wa ajira kwetu vijana.

Ikumbukwe pia kuwa nchi zote zinahitaji wawekezaji,hivyo wakiona katika nchi yako mitaji yao IPO hatarini kupotea kutokana na mazungirat mabaya ya uwekezaji lazima wahamishie mitaji yao na kwenda au kupeleka kuwekeza nchi zingine zenye mazingira mazuri na salamaaà
 
uwekezaji Tanzania ni mgumu sana kutokana na matatizo tuliyonayo;
i)Umeme usioaminika
ii) Matatizo ya maji
iii) kodi ambazo hazieleweki
iv) Rushwa
v) Uaminifu kwa watu ni mdogo sana
Kuna jamaa mmoja alikuwa nchi fulani southern Africa. akauza vitu vyake vyote ili akawekeze Tanzania. Jamaa mwenyewe aikuwa Muitaliano. Cha moto alikiona maana alifilisika na kuishia kurudi Italy akiwa maskini. Sasa hivi anaishi kwa pension. Kuwekeza Tanzania risk ni kubwa sana. Ni watu kama wahindi na wachina waliozoea kutoa rushwa ndiyo wanaweza kuja lakini kwa mzungu hapo sijui.
 
Ndugu zangu, Rais Samia Ni zaidi ya kiongozi, Ni zaidi ya Mwanasiasa,Ni zaidi ya mwanadiplomasia,Ni zaidi ya jasusi wa kiuchumi,Ni zaidi ya komandoo wa Vita ya kiuchumi, Rais Mama Samia Ni mchanganyiko wa hivyo vyote,Ni mjumuiko wa hayo yote, Ni muunganiko wa hayo yote, Ndani yake utayaona hayo yote,Ni Rais kweli kweliii,Ni Rais anayejuwa maana ya kiapo Cha Urais alicho apa, Anajuwa yupo hapo kwa ajili ya Tanzania na Watanzania,Anajuwa Nini anafanya, Nini anatakiwa afanye kwa ajili ya Taifa hili.

Rais Samia anajuwa kuzivuta fursa popote pale katika uso wa Dunia kwa ajili ya watanzania,Anajuwa kunasa mitandao ya kifursa kwa ajili yetu, Ndio maana tunaona ndani ya muda mfupi wa uongozi wake namna wawekezaji na watalii walivyo miminika na kutiririka hapa nchini, h ii yote ni kutokana na jitihada za kidiplomasia zilizofanywa na Rais Samia. Hii yote Ni kutokana na ushawishi alionao Rais Samia kitaifa na kimataifa,Hii yote ni kutokana na namna Rais Samia anavyokubalika na kuungwa mkono na watu mbalimbali,hii yote ni kutokana na heshima kubwa aliyojijengea na kulijengea Taifa letu katika Sura ya kimataifa ambayo imeifanya Tanzania kuaminika na kuwa chaguo namba moja la wawekezaji na watalii.

Sasa Rais Samia yupo Marekani kwa mualiko maalumu wa Rais Wa Marekani Joe Biden, Watanzania tutarajie mengi kutoka kwa Rais wetu,kitakuwa ni kishindo Cha mafuriko ya fursa nchini, Naamini anakwenda kuvuta wawekezaji na wafanyabiashara Wakubwa, Tutegemee na kutarajia fursa mbalimbali za kiuchumi kutiririkia nchini mwetu. Wapo viongozi wengi huko wa mataifa mengine,Lakini simuoni wa kushindana na Rais Samia kifursa,simuoni wa kuwakomba wawekezaji Zaid ya Rais Samia, simuoni wakumzidi ushawishi Rais Samia na Tanzania yetu,Tanzania Ni kubwa, Rais Samia Ni Maarufu na mashuhuri, huyu Ni Mama wa shoka,lazima vyombo vya habari vya kimataifa vitamani kufanya Naye mazungumzo ya masuala mbalimbali, lazima wawekezaji watamani kuonana na Rais Samia.

Rais wetu Mpendwa Ni Nyota iwakayo inayoweza kuwaongoza wavuvi Ziwani,Tanzania yetu lazima ing'ae ,lazima ivune fursa,lazima tunufaike na ziara hii ya Rais wetu, Lazima itikise na kutetemesha,lazima inase mabillioni ya kiuwekezaji kuja kwetu, lazima tupate madollar ya Kimarekani kupitia uwekezaji,lazima Tunufaike.

Ndugu zangu watanzania Rais wetu yupo kazini,sote tunamuona namna anavyoipambania nchi yetu,Tumuunge mkono na kumtia moyo,Tumpe Faraja na kumwombea Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia watanzania,Hakika tutafurahi wenyewe Kama ambavyo Tumeona Taifa likipiga Hatua mbele za kimaendeleo ndani ya muda mfupi katika kila Secta.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.:0742-676627
Wanakuja na majenereta yao ya umeme? Au na matenk yao ya maji
 
uwekezaji Tanzania ni mgumu sana kutokana na matatizo tuliyonayo;
i)Umeme usioaminika
ii) Matatizo ya maji
iii) kodi ambazo hazieleweki
iv) Rushwa
v) Uaminifu kwa watu ni mdogo sana
Kuna jamaa mmoja alikuwa nchi fulani southern Africa. akauza vitu vyake vyote ili akawekeze Tanzania. Jamaa mwenyewe aikuwa Muitaliano. Cha moto alikiona maana alifilisika na kuishia kurudi Italy akiwa maskini. Sasa hivi anaishi kwa pension. Kuwekeza Tanzania risk ni kubwa sana. Ni watu kama wahindi na wachina waliozoea kutoa rushwa ndiyo wanaweza kuja lakini kwa mzungu hapo sijui.
Nashukuru kwa mchango wako,lakini ningependaa kukuhakikishia kuwa Rais Samia amedhamiria kulinda Taswira nzuri ya Taifa letu mbeele ya macho ya wawekezaji kwa kuondoa changamoto zote zinazokuwa ni kikwazo kwa wawekezaji na uwekezaji
 
uwekezaji Tanzania ni mgumu sana kutokana na matatizo tuliyonayo;
i)Umeme usioaminika
ii) Matatizo ya maji
iii) kodi ambazo hazieleweki
iv) Rushwa
v) Uaminifu kwa watu ni mdogo sana
Kuna jamaa mmoja alikuwa nchi fulani southern Africa. akauza vitu vyake vyote ili akawekeze Tanzania. Jamaa mwenyewe aikuwa Muitaliano. Cha moto alikiona maana alifilisika na kuishia kurudi Italy akiwa maskini. Sasa hivi anaishi kwa pension. Kuwekeza Tanzania risk ni kubwa sana. Ni watu kama wahindi na wachina waliozoea kutoa rushwa ndiyo wanaweza kuja lakini kwa mzungu hapo sijui.
Kabla mwekezaji kutoka nje kuja kuwekeza Tanzania anauliza wale wengine ambao walishawekeza na majibu ya wale ndio yatawezesha wawekezaji wengi kuja au kutokuja.Hivi kuna mahali kuna matandao unaonyesha experience ya wawekezaji Tanzania ikoje??
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom