Rais Samia kuhudhuria na kuhutubia Baraza Kuu la 76 la Umoja wa Mataifa Jijini New York

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kwenda New York Nchini Marekani kesho Septemba 18, 2021 kuhudhuria Mkutano wa 76 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, akitarajiwa kuhutubia Baraza hilo Septemba 23

Vilevile, atahudhuria Mikutano ya kilele ya kujadili masuala ya mabadiliko ya tabianchi, usalama wa chakula na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)

1D436B32-59AF-40F7-BDC3-4DEBD85DBC8E.jpeg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kuondoka kesho Septemba 18, 2021 Tanzania kuelekea New York Marekani kuhudhuria Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Yaani Baraza Kuu la umoja wa mataifa UN, wakubwa wote wa dunia watakaa kimya kumsikiliza mama huyu jasiri akihutubia UN kwa mara ya kwanza Tangu 2015 mara ya mwisho kwa raisi kutoka Tz kufanya hivo.

Kila la heri our beloved president.

Nini maoni yako kuhusu ziara hiyo?

D10036EE-FB60-48D9-B4F4-4E376D55F0B6.jpeg
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom