Rais Samia kuhudhuria birthday ya Sugu, ni harakati za kumvimbia Spika Tulia?

sheiza

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
7,564
11,478
Katika hali isiyo ya kawaida, jana imeshuhudiwa mheshimiwa rais akiwa mgeni rasmi kwenye birthday ya ndugu mr 2 au sugu au 2proud au Jongwe.

Hii imeibua maswali lukuki hasa ikichukuliwa na muda ambao hiyo shughuli ilikuwa inafanyika na ni tukio la kwanza la aina yake.

Lakini kiundani zaidi inaonekana ni kama mpango wa kumzima dr Tulia asionyeshe cheche zake za uspika awapo bungeni.

Ikumbukwe mara ya mwisho bunge kupitia spika lilitoa amri kwa serikali kuja na hatua za msingi ambazo inachukua kuhusiana na sakata la kupanda mafuta na ikatoa deadline hali iliyopelekea mh rais kuitisha kikao usiku wa manane ili waziri wa nishati akatoe tamko kwa niaba ya serikali kama alivyoamriwa.

Pia ikumbukwe siku aliyoapishwa dr Tulia kama spika hakusita kumtaja hayati Magu kama mtu aliyechangia yeye kufika hapo jambo lililoonekana halikumpendeza sana mama.

Sasa je harakati hizi za kuhudhuria hadi sherehe za usiku za sugu ni harakati za kumzima dr Tulia na kutaka kumuonyesha kuwa wana uwezo wa kummaliza jimboni na pengine awe spika wa kipindi kimoja?

Muda utasema.
 
SSH na Tulia wako vizuri kabisa, natabiri jimbo la Mbeya mjini kugawanywa kabla ya uchaguzi 2025.

Hakuna haja ya kugawa jimbo la Mbeya Kwani SUGU ndio amekwisha aga siasa anataka kurudi kwenye music , ameona vijana wanavyovuta mpunga mrefu amevutika!

Mbowe nae kama ana akili huu ndiyo wakati wake wa kuachana na siasa ajishuhulishe na biashara zake kama mtaji amekwisha pata!!!i
 
Good analysis. Politically YES inawezekana. Strategically NO inategemea na Uelekeo wa TULIA katika SIASA za URAIS coz nafikiri issue sio Ubunge. Issue ni URAIS
 
Punguza ujinga, Samia ndio mwenyekiti wa ccm, amewakata manguli kama Andrew Chenge akampitishia Tulia peke yake.

Umbea haukupendezi mtoto wa kiume, unadhani Ndugai alipenda kujiuzuru? Ndio sembuse huyu digidigi Tulia atamsumbuwa Rais kwa lipi? Unaweza kuleta jeuri kwa mwenyekiti wako?
 
Mwenyekiti ni Kikwete ,Samia ni boya tu!!! Maamuzi yote yanafanyika kabla ya mkutano na cha kushangaza kwenye mikutano ya Kamati kuu , Halmashauri kuu Kikwete ni mstaafu sio mjumbe lakini hakosi!!! CCm bila kumfunga kengele VascoDagama atakiyumbisha chama chenu kama anavyoiyumbisha serikali kuhusu Katiba mpya!!!
 
Katika hali isiyo ya kawaida, jana imeshuhudiwa mheshimiwa rais akiwa mgeni rasmi kwenye birthday ya ndugu mr 2 au sugu au 2proud au Jongwe.

Hii imeibua maswali lukuki hasa ikichukuliwa na muda ambao hiyo shughuli ilikuwa inafanyika na ni tukio la kwanza la aina yake.

Lakini kiundani zaidi inaonekana ni kama mpango wa kumzima dr Tulia asionyeshe cheche zake za uspika awapo bungeni.

Ikumbukwe mara ya mwisho bunge kupitia spika lilitoa amri kwa serikali kuja na hatua za msingi ambazo inachukua kuhusiana na sakata la kupanda mafuta na ikatoa deadline hali iliyopelekea mh rais kuitisha kikao usiku wa manane ili waziri wa nishati akatoe tamko kwa niaba ya serikali kama alivyoamriwa.

Pia ikumbukwe siku aliyoapishwa dr Tulia kama spika hakusita kumtaja hayati Magu kama mtu aliyechangia yeye kufika hapo jambo lililoonekana halikumpendeza sana mama.

Sasa je harakati hizi za kuhudhuria hadi sherehe za usiku za sugu ni harakati za kumzima dr Tulia na kutaka kumuonyesha kuwa wana uwezo wa kummaliza jimboni na pengine awe spika wa kipindi kimoja?

Muda utasema.
jamaa unaona mbali sana wewe!
 
Back
Top Bottom