Rais Samia kuanza upya siyo vibaya, kwa Wakuu wa Wilaya/Mikoa si Sabaya peke yake, wapo wengi waliovunja haki za binadamu

Tumbiliwaulaya

JF-Expert Member
Nov 22, 2020
280
435
Mama kwa heshima na taadhima,kwanza nikushukuru kwa hatua uliyoichukua dhidi ya mkuu wa wilaya ya Hai mheshimiwa Sabaya, na kwa kuwa la Sabaya umesema lichunguzwe maoni yangu kuhusu yeye ninayaweka kando.

Ila mama nikumbushe kitu kimoja, umefungua mlango ambao haukupaswa kufunguliwa,ila tu kama una dhati ya kweli toka moyoni mwako.

Kwanini nayasema haya? nayasema haya kwa kuwa si Sabaya tu bali baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa katika kipindi hiki cha miaka mitano iliyopita wamehusika kikamirifu katika uvunjaji ulio kithiri wa haki za binaamu.

Umefungua mlango pale ulipoamua kuitika na kulifanyia kazi suala la Sabaya,kuanzia sasa utajua mengi toka kwa wana wa nchi hata kwa wale ambao mambo yao yalikuwa yamesitilika sasa yatakuwa wazi,walio umia ni wengi na wakaamua kukaa kimya kwani walijua hata wakilia hakuna atakae wapokea msiba wao na kwa kuwa umeitika na ukafungua mlango sasa tarajia wageni wengi wenye vilio na mateso watataka uzisikie hadithi zao za mateso waliyo pitia,na hata wale walio kwisha mpelekea Mungu misiba yao sasa watairejesha ili uwafute machozi.

ILI UFUPISHE MANENO TIMUA WOTE UANZE UPYA.
 
Back
Top Bottom