Rais Samia, kota zote zilizobaki ni uchafu, ziondoke!

nashicha

JF-Expert Member
May 29, 2021
279
517
Mh leo umepata kufungua na kukabidhi nyumba mpya na nzuri za Magomeni nakuomba kwa kauli yako uwape nguvu za kisheria Wakurugenzi kuondoa kota zote hasa za ILALA MCHINIKINI zimekuwa ni uchafu kwa mwonekano wa Jiji letu, hasa mbele ya ofisi za Mkuu wa mkoa.

Kungeweza kujengwa Parking nzuri na ofisi ya mkuu wa Wilaya lakini kota zimekuwa Kama jalala pamoja na kuwaondoa Wamachinga Hizo kota hapo ndio zimekuwa maficho ya uchafu na biashara.

Ni bora kujengwe nyumba nzuri hao wakaazi wapewe na ziweze kuchukua idadi ya familia nyingi zaidi maana maeneo ni makubwa, lakini mabanda yaliyopo yamekuwa uchafu mkuu wa mkoa ombea kibali upate hata mahali pakuegesha magari maana ofisi yako imebanwa Sana na vilevile utalipendezesha jiji nawasilisha.
 
Back
Top Bottom