Rais Samia: Kiwanda cha tumbaku Morogoro kitafufuliwa mwaka 2023

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuna mwekezaji amejitokeza ili kukifufua kiwanda cha tumbaku kilichopo Morogoro ambapo amesema kufufua kiwanda hicho kutakuza uhitaji wa soko la tumbaku na kuwataka wakulima wa tumbaku kuendelea na kilimo hicho.

Ameyasema hayo mkoani Tabora akizindua Barabara ya Tabora, Koga, Mpanda. Bei ya Tumbaku imeonekana kushuka tangu mwaka 2018 kwa takwimu za kutoka Benki Kuu ya Tanzania. Inawezekana ufufuaji wa kiwanda hicho ikawa chachu ya kuongeza bei na hali ya masiaha kwa vijana ambao wamekuwa wakinufaika na uwepo wa kiwanda hicho.

1652869526737.png
 
Bei ya Chai ya Tanzania nayo inazidi kushuka kwenye soko la dunia.
 
Back
Top Bottom