Rais Samia: Kisiasa tupo vizuri, leo wanangu wamejipanga na Mabango yao nikawaambia nimewaona, nikawapungia Mkono

Rais samia akiwa Washington D.C amesema Tanzania kisiasa tupo Vizuri.

Hali ya Kisiasa Tupo Stable,Hali ya Kisiasa iko Nzuri, tunachukua Hatua za kufanya Vyama vyote vya Siasa vikae Pamoja Kujadili namna ya Kuendesha Siasa zetu Nchini.

"Nimeunda timu ndani ya vyama vya siasa, tumeweka Jeshi la Polisi, viongozi wa dini, taasisi za kijamii, watajadili mambo ambayo wamepanga, kuna chama cha siasa kimoja bado hakijakubali bado naendelea na mazungumzo nao na nawaelewa kwanini hawajakubali" - Rais @SuluhuSamia.

Rais amewaona Vijana wa Marekani walioandamana na Mabango na Fulana wakidai Katiba Mpya na Wabunge wa 19 Wafukuzwe. Amesema ameyaona Mabango na kuyasoma. Ujumbe umefika.

Kuhusu chadema kugomea Vikao vya Baraza la vyama vya siasa, amesema anawaelewa na anaendelea kuzungumza nao ili wajiunge na wenzao.

Ziara ya Rais Samia: Watanzania waishio Marekani waandamana kudai Katiba Mpya

View attachment 2199573
Kwa kweli ile hali tuliyokuwa nayo chini ya Magufuli ilikuwa inatisha. Hata ukifanya jogging, tayari Polisi Hawa hapa. Wale waliovaa fulana za "PRAY FOR LISSU", habari yake waliipata kwa Polisi. He, Mungu amesaidia mama anarejesha mshikamano na utulivu.
 
Back
Top Bottom