Kanzastone
JF-Expert Member
- Jan 14, 2021
- 244
- 355
Siku ya kuwaapisha ma-Katibu Wakuu wa Mikoa siku ya tarehe 2 June 2021 Ikulu ya Chamwino Mh. Rais alitamka kwamba atashangaa Mtumishi wa Umma kumuona anakata Rufaa kwake kama Rais pale inapotokea Tume ya Utumishi wa Umma inatupilia mbali kesi ya mtumishi.
Nilipoyasikia maneno hayo kutoka kwenye kinywa cha Mh. Rais nilipigwa na butwaa! Nikajiuliza kuwa hivi kuna shida gani inayowakumba watawala wa nchii hii kiasi cha kwamba hawajui maana ya haki na upatikanaji wake? Nikajiuliza kuwa aaaaaaa na Samia tena ambae tunaona ni tumaini letu!
Pia nikajiuliza kuwa:
1. Hivi Mh. Rais hajui madudu yanayofanyika na Tume ya Utumishi wa Umma dhidi ya kesi zinazopelekwa pale Tume?
2. Hivi Mh. Rais hajui kuwa Tume ya Utumishi inahujumu haki ya watumishi kwa kuungana na waajiri wasiokuwa na maadili?
3. Hivi Mh. Rais hakumbuki kuwa watu wameilalamikia sana hii Tume juu kupora haki ya watumishi wanaopeleka rufaa zao pale Tume
4. Hivi Mh. Rais hajui kuwa yeye ndo mwenye mandate ya watumishi na taasisi zake zoote kisheria?
5. Hivi Mh. Rais hajui kwamba kwa maneno aliyoyatoa siku ile tena mbele ya watendaji wake ana pre-empty baadhi ya kazi ya uchambuzi wa hizo rufaa zilizokwishafanywa na watendaji wake Mh. Rais?
6. Hivi Mh. Rais hajui kuwa kwa maneno aliyoyatoa siku ile anaondoa maana na umuhimu wa dhana ya checks and balances kwenye utendaji? Ni sawa na kusema kuwa uamuzi uliofanywa na mahakama za chini haina haja ya kuukatia rufaa kwenye mahakama za juu!
Mwisho, najua Mh. Rais alipotoka tu katika hili, washauri wa Mh. Rais wajitahidi kumshauri Rais ili kuondoa kutokea kwa sintofahamu katika jamii hivyo kuondoa matumaini waliyokuwa nayo watumishi.
Asante.