Rais Samia: Kesi ikishatupwa na Tume ya Utumishi wa Umma isiletwe kwangu

Kanzastone

JF-Expert Member
Jan 14, 2021
244
500
Siku ya kuwaapisha ma-Katibu Wakuu wa Mikoa siku ya tarehe 2 June 2021 Ikulu ya Chamwino Mh. Rais alitamka kwamba atashangaa Mtumishi wa Umma kumuona anakata Rufaa kwake kama Rais pale inapotokea Tume ya Utumishi wa Umma inatupilia mbali kesi ya mtumishi.

Nilipoyasikia maneno hayo kutoka kwenye kinywa cha Mh. Rais nilipigwa na butwaa! Nikajiuliza kuwa hivi kuna shida gani inayowakumba watawala wa nchii hii kiasi cha kwamba hawajui maana ya haki na upatikanaji wake? Nikajiuliza kuwa aaaaaaa na Samia tena ambae tunaona ni tumaini letu!

Pia nikajiuliza kuwa:

1. Hivi Mh. Rais hajui madudu yanayofanyika na Tume ya Utumishi wa Umma dhidi ya kesi zinazopelekwa pale Tume?

2. Hivi Mh. Rais hajui kuwa Tume ya Utumishi inahujumu haki ya watumishi kwa kuungana na waajiri wasiokuwa na maadili?

3. Hivi Mh. Rais hakumbuki kuwa watu wameilalamikia sana hii Tume juu kupora haki ya watumishi wanaopeleka rufaa zao pale Tume

4. Hivi Mh. Rais hajui kuwa yeye ndo mwenye mandate ya watumishi na taasisi zake zoote kisheria?

5. Hivi Mh. Rais hajui kwamba kwa maneno aliyoyatoa siku ile tena mbele ya watendaji wake ana pre-empty baadhi ya kazi ya uchambuzi wa hizo rufaa zilizokwishafanywa na watendaji wake Mh. Rais?

6. Hivi Mh. Rais hajui kuwa kwa maneno aliyoyatoa siku ile anaondoa maana na umuhimu wa dhana ya checks and balances kwenye utendaji? Ni sawa na kusema kuwa uamuzi uliofanywa na mahakama za chini haina haja ya kuukatia rufaa kwenye mahakama za juu!

Mwisho, najua Mh. Rais alipotoka tu katika hili, washauri wa Mh. Rais wajitahidi kumshauri Rais ili kuondoa kutokea kwa sintofahamu katika jamii hivyo kuondoa matumaini waliyokuwa nayo watumishi.

Asante.
 
TASK FORCE

JF-Expert Member
Apr 7, 2017
2,481
2,000
Bila katiba mpya tutapata shida haswa kwa hawa watawala wa CCM, dawa yao ni kuwaendea kwa waganga wa kienyeji mnamalizana bila lawama.
aliekudanganya mzanzibar au mcha Mungu anarogeka hakutakii mema
 
zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
1,127
2,000
Bado tuendelee kuwasisitizia watu ambao hamtaki kuelewa hata sijui mtu awaambieje!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawezi kufanya mambo nje ya watu na vyombo vinavyomzunguka. Sasa mnataka Rais afanye maamuzi gani tofauti na yale aliyoshauriwa na vyombo vilivyopo kikatiba ili vimshauri?

Halafu, uzi huu unadhihirisha inconsistencies katika kufikiri kwa baadhi ya watu. Rais JPM alipigwa sana mawe kwa sababu sometimes alijiongeza nje ya kile alichokuwa akishauriwa na wanaomzunguka. Nyie mliona hafai kwa haiba yake hiyo mkamwita dikteta. Mama Samia ana haiba tofauti anataka kubaki kwenye ile misingi ya katiba na ndani ya mipaka yake. Bado hamtaki tena afanye hivyo. Nyie mnataka nini basi?
 
OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
35,171
2,000
Kwani sheria na taratibu zinasemaje? Watumishi walikuwa wanakata rufaa kwa rais kwa utashi wao au ndio utaratibu?
 
crocodile

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,504
2,000
Ingependeza kama ungetupa mfano mmoja tu wa nchi inayojitambua ambayo ukishindwa kupata haki kwenye Mahakama unaenda kwa Rais.
 
mathsjery

JF-Expert Member
Sep 26, 2015
1,895
2,000
Kwani sheria inasemaje?

Kisheria watu wanaruhusiwa kukata rufaa kwa rais?
Bado tuendelee kuwasisitizia watu ambao hamtaki kuelewa hata sijui mtu awaambieje!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawezi kufanya mambo nje ya watu na vyombo vinavyomzunguka. Sasa mnataka Rais afanye maamuzi gani tofauti na yale aliyoshauriwa na vyombo vilivyopo kikatiba ili vimshauri?

Halafu, uzi huu unadhihirisha inconsistencies katika kufikiri kwa baadhi ya watu. Rais JPM alipigwa sana mawe kwa sababu sometimes alijiongeza nje ya kile alichokuwa akishauriwa na wanaomzunguka. Nyie mliona hafai kwa haiba yake hiyo mkamwita dikteta. Mama Samia ana haiba tofauti anataka kubaki kwenye ile misingi ya katiba na ndani ya mipaka yake. Bado hamtaki tena afanye hivyo. Nyie mnataka nini basi?
Soma ukurasa wa tano
 
Attachments

  • File size
    1.1 MB
    Views
    13

Haxxan Jr

Member
Jan 28, 2021
18
45
Bila katiba mpya tutapata shida haswa kwa hawa watawala wa CCM, dawa yao ni kuwaendea kwa waganga wa kienyeji mnamalizana bila lawama.

wananchi wengi hawako tayari kuona ccm inatoka madarakani ...it's ok tuwe na wabunge wapinzani lkn sio CCM kutoka madarakani ....tunaitkadi kwamba CCM ndio chama pekee cha kuweza kusimamia muungano na vile vile ni chama kinachoonekana hakina udini ktk macho ya watu km vyama vingine ....watanzania wengi wana hofu na CCM kutoka madarakani ...kwa ufwatiliaji wangu ni megundua hivyo
 
Pslmp

JF-Expert Member
Mar 18, 2021
1,630
2,000
Kifungu cha 25( 1 ) ( d ) cha Sheria ya Utumishi wa Umma pamoja na Kanuni ya 60( 5 ) Kanuni za Utumishi wa Umma vinasema kuwa , mtumishi ambaye hakuridhishwa na maamuzi ya tume ya rufaa anaweza kukata rufaa tena kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano

Rais ndiye mkuu wa watumishi wote na maamuzi yake yatakuwa ni ya mwisho na hakutakuwa na rufaa nyingine tena isipokuwa sasa ukiamua kubadilisha mwelekeo/upepo na kwenda mahakamani.
Haya ndiyo ya msingi kuhusu rufaa ya mtumishi wa umma.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom