Rais Samia, Katiba Mpya ndio suluhu ya matatizo ya Watanzania

Iwe ni kuwa na bunge lenye meno na ambalo litakuwa wajibu wa kuiwajibisha serikali lazima watanzania tukomae tupate katiba mpya.

Iwe ni kudhibiti wanasiasa waovu ambao walishageuza nchi yetu kama shamba la bibi kuvuna na kuiba mali za umma. Tunahitaji katiba mpya.

Kulinda na kutetea haki za kila mtanzania dhidi ya maovu ya udhalimu wa wakora wa kisiasa na wanaoua, kutesa na kuletea maumivu watanzania. Tunahitaji katiba mpya.

Katiba mpya itafutwe kwa kila namna, iwe kwa maandamano, makongamano, elimu na kuhamasisha watanzania wote bila kujali itikadi zao.

Katiba mpya ndio suluhu la matatizo ya taifa letu. Tupate katiba ambayo itaruhusu raisi, spika, waziri , Igp na kiongozi yoyote kushitakiwa kama akifanya kosa.
Siku ya mwisho kila goti litapigwa , mmekwishaanza kujianika , Mamluki wakubwa nyie .

Wewe tulikuonya mapema sana lakini ulitoa mapovu yenye matusi , kiko wapi sasa ?
 
Kenya walipambania Katiba Mpya wakapoteeza feedha nyingi sana kwa hilo zoezi, matokeo yake mambo ni yale yale, ufisadi ni ule ule.

Katiba mpyaa sio solution ya matatizo ya mtanzania. Siku watu wotee tukibadili mindset basi taifa litasonga.
Kenya unataka kuilinganisha na utopolo gani hapa EA?
 
Usijidanganye mkuu, Katiba mpya kenya imeleta mabadiliko makubwa. Kwamba ufisadi ni uleule sio kweli. Hukusikia Dci wa Kenya alifungwa kwa kudharau mahakama? Lini umesikia scandal za ufisadi Kenya kama miaka ya utawala wa Moi.
Kaangalie walivyogawana fedha za Covid kisha rudi hapa. Mambo Kenya yapo vile vile, utofauti upo kwenye namna tu viongozi wakubwa wanavyopatikana.
 
Kenya walipambania Katiba Mpya wakapoteeza feedha nyingi sana kwa hilo zoezi, matokeo yake mambo ni yale yale, ufisadi ni ule ule.

Katiba mpyaa sio solution ya matatizo ya mtanzania. Siku watu wotee tukibadili mindset basi taifa litasonga.
Wewe jitafakari zaidi. Huna tofauti kifikra kama yule mtu anaeamini kuwa raia kwakibadili mindset zao basi hakuna haja ya kuwa na Polisi wala Mahakama.
 
Wewe jitafakari zaidi. Huna tofauti kifikra kama yule mtu anaeamini kuwa raia kwakibadili mindset zao basi hakuna haja ya kuwa na Polisi wala Mahakama.
Upo sawia kabisa....huoni finland wanafikiria magereza ni ya kazi gani, simply because hakuna wafungwa. Mkibadili mindset mnapata maendeleo, sio katiba
 
Pumbavu mkubwa achana na mimi.
Huku kwetu watu huwa huwa hawamshambulii mtu individual Bali hushambulia hoja aliyoitoa.

Jifunze kujenga hoja wachangiaji watakuelewa. Viwanda vya matusi kejeli na mipasho waachie wenyewe Kule ulikotoka.
 
Mwalimu Nyerere alipigania Uhuru wa nchi yetu na kufanikiwa tukamwita Baba wa Taifa.
Mama akifanikisha kupatikana katiba inayotokana na mapendekezo yaliyowasilishwa na iliyokuwa Tume ya kukusanya maoni chini ya Warioba napendekeza tumuuite Mama wa Taifa.
Au mnasemaje ndugu zangu?
 
Iwe ni kuwa na bunge lenye meno na ambalo litakuwa wajibu wa kuiwajibisha serikali lazima watanzania tukomae tupate katiba mpya.

Iwe ni kudhibiti wanasiasa waovu ambao walishageuza nchi yetu kama shamba la bibi kuvuna na kuiba mali za umma. Tunahitaji katiba mpya.

Kulinda na kutetea haki za kila mtanzania dhidi ya maovu ya udhalimu wa wakora wa kisiasa na wanaoua, kutesa na kuletea maumivu watanzania. Tunahitaji katiba mpya.

Katiba mpya itafutwe kwa kila namna, iwe kwa maandamano, makongamano, elimu na kuhamasisha watanzania wote bila kujali itikadi zao.

Katiba mpya ndio suluhu la matatizo ya taifa letu. Tupate katiba ambayo itaruhusu raisi, spika, waziri , Igp na kiongozi yoyote kushitakiwa kama akifanya kosa.
Kama na humo mwenu mmeanza kuelewa maana ya "KATBA MPYA YA WANANCHI". Basi kumbe karibu patapambuzuka
 
Rais Samia Suluhu Hassan kwanza nakupongeza sana kwa hatua mbalimbali unazochukua baada ya kuondokewa na Magufuli Mhe. Rais kama lilivyo jina lako wewe ndio Suluhu ya suala la Katiba mpya.

Haya yote unayohangaika nayo kuyaweka sawa ni kutokana na Mwendazake kuona mapungufu yaliyopo kwenye katiba iliyopo ndio ikawa rahisi kwake kuyafanya aliyoyafanya. Nadhani hata wewe utakumbuka hayati Baba wa Taifa aliwahi kusema Katiba hii ilimpata rais dikteta atawaonea wananchi na hilo limetimia kwa Mwendazake.

Rais samia "legacy" yako pekee sio kujenga zahanati au kupandisha mishahara bali ni kuwapatia wananchi katiba mpya nakuhakikishia rais samia utakumbukwa kwa miaka hata 50 ijayo rais mstaafu Jakaya Kikwete pamoja na kuwa hakufanikiwa kutupatia katiba mpya lakini vizazi vinamkumbuka kwa uthubutu wake wa kuanzisha mchakato kwani alisema katiba iliyopo ina miaka 50 na mambo mengi yamebadilika.

Mungu ambariki sana.
kabla hata mwaka mmoja haujaisha, Rais Samia ameitupilia mbali Katiba ya Wananchi (aka Katiba ya Warioba), sasa anataka kuja na katiba yake ya mchongo anayoijua yeye mwenyewe:

Back
Top Bottom