TaiPei
JF-Expert Member
- Aug 4, 2022
- 391
- 322
Mama nakusalimu kwa jina la JMT,
Mimi ni muumini sana "Satstification & appreciation"
Nafahamu kwa kutumia vyombo vyako unafahamu taarifa zote za uchapakazi na Uhodari wa DED wetu, DC na DAS wetu, DSO wetu katika Wilaya hii,
Majuzi wakati unawaapisha wakuu wapya wa mikoa ulimmwagia sifa lukuki Dada yetu Mkurugenzi wa Malinyi Mhe Joanfaith John kwa uchapakazi wake uliotukuka ambao nchi nzima imekubaliana na wewe kuhusu binti yule kuwa ni mtu wakutiliwa mfano kwa Uchapakazi anaouonesha,
Mhe Rais wangu, hebu usipite Mbarali bila kuwapongeza na kuwatia moyo hawa viongozi wetu kwa mambo makubwa wanayofanya.
Wacha nitaje machache tu niliyoyaona:
1. Wanafanya kazi kwa Upendo na Ushirikiano wa kiwango cha juu Sana,
2. Wanafanya vizuri Sana katika ukusanyaji wa Mapato mkoa mzima wa Mbeya,
3. Mbarali,Ndio Wilaya pekee hapa Tanzania iliyosajili mifugo yake kielektroniki kwa kiwango kikubwa ili kutekeleza sera yako ya kuongeza uuzwaji wa nyama na mifugo nje ya nchi,
4. Kusimamia vizuri kilimo cha Mpunga na mazao mengine,
5. Kusimamia vizuri miradi ya Ujenzi ikiwemo hii VETA utakayoizindua leo,
6. Kusimamia swala la Elimu bure kwa watoto wetu wote,
#MBEYA TUNAKUPENDA SANA MHE RAIS NADHANI UMEJIONEA MWENYEWE MAPOKEZI YETU
<<<<<<<<<<<<<>>>>>>>>>>>>>>>
Pitia pia hii ziara ya Waziri wa Kilimo Mbarali Hussein Bashe,
Hili ni Shamba la Mpunga Mbarali ( Skimu ya Umwagiliaji )
Waziri Bashe akitua na helkopta ya Jeshi Mbarali kuhamasisha kilimo cha Umwagiliaji,
Mkuu wa mkoa Mbeya akiwa na Mawaziri wa Kilimo katika uhamasishaji wa kilimo cha Umwagiliaji Mbarali
#Hongera Sana wanaMbarali,