Rais Samia, kana una nia ya dhati dhidi ya uovu, wengine hawa hapa wanaoshutumiwa kwa uhuni, ufisadi na dhulma

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
822
1,000
INAMPASA MMOJA AFE KWA AJILI YA WENGI? HAPANA WAFE WOTE WENYE DHAMBI. (JE, OLE SABAYA AMETOLEWA SADAKA?)

Tunashukuru kwa hatua uliyoichukua dhidi ya Sa baya. Huyu alikuwa na makando kando mengi nyakati za utawala wa Hayati John Pombe Magufuli(Dhulma, Matumizi mabaya ya Uongozi, Ufisadi n.k)

Lakini hakuwa peke yake. na wengine hawa hapa tunaomba wafanyiwe uchunguzi huru na wa haki. Either washtakiwe au wasafishwe. Mimi naanza na huyu wa kwanza.

1. Christian Makonda
Tuhuma zake ni pamoja na Kuchukua Rushwa, Kutumia mamlaka Vibaya, Kuhusishwa na Utekaji na Mauaji. Tunaomba ufanyike uchunguzi huru ili asafishwe kijana wa watu au ahukumiwe maana isije tu kuwa Chadema walikuwa wanamchukia na kuamua kumpakazia mambo hayo sababu ya utendaji kazi wake akiwa Mkuu wa Mkoa na baada ya kutokuwa Mkuu wa Mkoa wameridhika mpaka siku tena akija pata Cheo au Uongozi ndo waanze kulalamika. Tunaomba jambo hili ulifanyie kazi.

Wito wangu
Naomba watanzania wenzangu either tutaje watuhumiwa wengine au tutaje wanaotakiwa kusafishwa kutokana na yale ambayo walitendwa na kunenwa. Mimi nimeanza na huyo wewe Mtanzania mwenzangu unaweza ongezea wengine.
 

Magna Carta

JF-Expert Member
Jul 14, 2014
4,080
2,000
Mtu Asiyejulikana hata wewe unadhamiri chafu, Kama unazo tuhuma za Makonda na unao ushahidi weka wazi na kaa ukikumbuka Serikali inayo macho makubwa ya kuona.
 

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
681
1,000
Mtu Asiyejulikana hata wewe unadhamiri chafu, Kama unazo tuhuma za Makonda na unao ushahidi weka wazi na kaa ukikumbuka Serikali inayo macho makubwa ya kuona.
USA wao kupitia CIA hawakukurupuka kumtuhumu na kumblacklist kuingia kwao. Kama CIA walishamuona huyu asiyejulikana anahitajika aseme nini?.. Hapa ni serikali chunguzeni tuhuma za CIA . Period
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
15,734
2,000
Mtu Asiyejulikana hata wewe unadhamiri chafu, Kama unazo tuhuma za Makonda na unao ushahidi weka wazi na kaa ukikumbuka Serikali inayo macho makubwa ya kuona.
hana dhamana ya kuweka wazi yeye kama mtu binafsi vyombo vya uchunguzi vina dhima hiyo
 

King Bill

JF-Expert Member
Feb 8, 2021
685
1,000
Makonda hakutuhumiwa na CHADEMA tu, alituhumiwa na watanzania wote wapenda haki,kwa kuwa vitendo vyake na kauli zake zilisadifu hulka yake na kuthibitisha uovu na uhuni wake.
 

Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
2,024
2,000
Me mwenyewe sioni kama happy anamakandokando kama hao mbwiga wengine
Hapi labda sababu ya uchawa uliopitiliza, hana tofauti na Mwigulu, Kingwagwala, Kabudi, Kasesela, Gambo and the likes, but mambo ya ujambazi, uporaji, utapeli na matabia ya kishenzi kama Sabaya or Makonda hao watu hawana!

Na hata kama wanaiba basi hawaibi kifalafala! Haiwezekani mshahara wa RC mil 5 kwa mwezi then mtu ndani ya miezi 6 tu kazini ananunua gari la mil.300, na hana biashara yeyote!! And still Magu alikuwa anajisifu anapambana na mafisadi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom