Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,693
- 36,080
Habari!
Kwakweli kama mtumishi ambaye sijapanda daraja tangu niajiriwe, siujui mshahara mpya nakaribia mwaka wa sita sasa hapa matumaini yanayeyuka. Naanza kufikiri nje ya duara.
Hata hayo madaraja mapya sijui kama nami nitakuwa mmoja wapo. Maana idadi ya wanaostahili kupanda madaraja ni wengi kuliko idadi tuliyotajiwa.
Pia kuna mambo mawili:
1. Kuahidiwa/kutajiwa jambo
2. Kutendewa.
Hapa kuna watu watanawa lakini hawatakula.
Ok, twende kwenye hoja.
Kama uchumi umeyumba tangaza kupunguza mshahara wako pamoja na mshahara wa viongozi waandamizi bila kuwasahau wabunge.
Hii itasaidia kumpunguzia mlipa kodi mwananchi mzigo mkubwa.
Uchumi utakapokaa sawa mtaendelea na utaratibu wenu wa kulipana mamilioni huku mkiendelea kulipana allowances kedekede.
Sisi watumishi na wananchi wanyonge hatuna shaka na nyie viongozi, tunajua umuhimu wenu katika taifa hili.