Rais Samia kama binadamu ana mapungufu ila ana sifa zote za kuwa Kiongozi wa Nchi yetu

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Hakuna binadamu aliyekamikika, hivyo hata Mama Samia hajakamilika. Ila kiuongozi nitakuwa wa mwisho kukosoa na kusema Hana sifa ya kuwa Rais wa Nchi.

Urais wa Nchi unaongozwa na sifa Moja kuu, Rais ni Mzazi Kwa Taifa bila kujali ana umri Gani. Mama anasimama kama mzazi kwetu.

Jambo la pili Rais anapaswa kuwa mtu anayekubali kwamba hajui kila kitu ila anaweza kusimamia kila Jambo linalopaswa kusimamiwa. Mhe. Rais hajui kila kitu ila anaweza akasimamia Yale tuliyomkabidhi asimamie.

Jambo la tatu, akikosea anaweza akarekebisha makosa endapo yanarekebishika. Mhe Rais ni mwepesi kurekebisha pale anapopata fact kwamba Kuna mapungufu, aliwahi kuacha baadhi ya wateule wake baada yakusikia wananchi wakilalamika, Leo amerekebisha utata uliokuwa kwenye hotuba yake. Huu ndio uzazi na Uarais siyo kukomaa ukijitapa kwamba hakuna makosa

Anaweza akasemehe na wakati mwingine akapuuza, amempuuza Ndugai, Polepole n wengine. Hakutaka kushindana nao Wala kuwaonyesha yeye ana ñguvu Gani ameacha mamlaka ziangaike nao.

Anakasirika kama mwanadamu, anakwazika lakini hatoki adharani kuonyesha amekwazika. Kwa kuwa wanaomkwaza ni watu wazima anawaita nakuwakanya au kuwasikiliza ndani majirani wasijue. Tulishaanza kuona Taifa likiongozwa Kwa hasira za papo Kwa papo Leo hasira zinaelekea kwenye kalamu bila kudhalilishana. Pongezi

Mwisho; anaamini kwamba anaweza kupotoshwa na walio chini yake Kwa maslahi Yao na anapobaini anarudi nyuma kuyatizama maamuzi yake nakurekebisha pale alipopotoshwa. Tulimsikia kwenye mkutano wa vyama vya siasa,alikiri kwamba maridhiano ni muhimu na akaagiza waliopo chini yake wamshauri namna nzuri yakuliponya Taifa

Hizi sifa wanazo watu wachache sana, hata huko upinzani hakuna watu wenye sifa hizi sema awajapata madaraka mngejionea rangi zao halisi.

Kuhusu maendeleo; ukiwa na Kiongozi anayetenda haki na anayemcha Mungu ni zaidi ya majengo na mareli. Ukiwa na hofu hata utajiri hauna maana. Ameanza kurejesha confidence yetu soon ataendelea kufungua milango tujiletee maendeleo maana hakuna Rais anayeleta maendeleo, maendeleo yanaletwa na watu Kwa kufanya KAZI. Akiendelea mmoja mmoja kati yetu basi Taifa limesonga mbele.

Hongera Mama Samia, unayo nafasi yakurekebisha machache mabaya yanayokuchafua hasa ya kisiasa then utafanya mazuri mengi. Fungua moyo na tangaza msamaha kwa waliokukosea uanze ukurasa mpaya, samehe uliorithi kutoka kwa utawala uliopita. Ponya taifa manunguniko yakiisha taifa litapata baraka na umoja wetu utaonekana. Nikuombe sana sana usirithi ukatili maana ujazaliwa katili, usiumizwe na wapinzani wanaosema adharani, umizwa na wanaokusema gizani ambao umewateua wewe. Hao wa ndani wanaokwambia funga huyu fungua huyu ni wabaya kuliko wanaokubeza adharani.

Nikutakie mwaka mpya 2022, nipo nawewe bega kwa bega kwenye yale tu yenye maslahi kwa taifa na siyo maslahi ya chama.
 
Ila tatizo alisema mwenyewe kuwa raisi hakosei. Na pia tatizo kubwa zaidi ni makosa haya yamekua kwenye hotuba zote.

Mfano akiwa kwenye mkutano wa COP26 alisema geothermal ni moja ya chanzo Cha nishati nchini, kitu ambacho sio kweli.

Kuna shida kubwa kwa wanaoandika hotuba na wanaompa taarifa, lakini pia yeye anapaswa kuwa fit kujua na kusoma mambo mengi ili fedheha hizi ndogondogo inakua rahisi kuepuka
 
Hakuna binadamu aliyekamikika, hivyo hata Mama Samia ajakamilika. Ila kiuongozi ntakuwa wa mwisho kukosoa na kusema Hana sifa ya kuwa Rais wa Nchi...
Naunga mkono hoja
Hivyo hata hili la milioni na bilioni, ni kosa la kawaida sana tusilifanye nongwa!.

P
 
Kwani Ndugu zitto ambae ni Ndugu katika Imani na Rais yeye anasemaje? Maana Rais akiwa muislamu zitto hakosoi lolote anageuka kua chawa na Rais akiwa mkristo zitto huchambua hoja kwa hoja kiuchumi na hukosoa kweli kweli.
 
Dah...Kwaheri CCM, ...ndo basi tena.
Magu alikirusha Kwenye Reli baada ya Mkwere Kukiherereza...! Ilifika mahala Ukivaa Sare Ya CCM Unazomewa..!! Ile Hali naanza Kuiona Soon!!
 
Huyu mama sifa zote kuu za urais hana.
Rais anapaswa kuwa na Upeo, maono na ushawishi. Yeye mwenyewe anajua sifa za kupewa urais hana isipokuwa bahati (kudra) ndio imempa urais baada ya bosi wake kufa ghafla. Kwa sasa anaamini anaweza kuendelea kuwa rais kwa sababu ya jinsia yake ya kike.

Pale tumepigwa kwa 100%.
 
Dah...Kwaheri CCM, ...ndo basi tena.
Magu alikirusha Kwenye Reli baada ya Mkwere Kukiherereza...! Ilifika mahala Ukivaa Sare Ya CCM Unazomewa..!! Ile Hali naanza Kuiona Soon!!
Kuweka kumbukumbu sawa Magu ndio aliiua kabisa CCM, na kuzalisha genge lake uchwara la kidikteta na kihuni kwa mwamvuli wa kijani.

Wewe ulishawahi kuona wapi wanaCCM wanashangilia katiba ibadilishwe ili rais aliyepo madarakani aendelee kukaa madarakani milele?

Toka lini CCM ikapitisha wagombea wa udiwani na ubunge bila kuzingatia mchuano wa kura za maoni?

Toka lini CCM ikakosa watu wa kuongoza CCM na serikali mpaka kwenda kununua wapinzani ili kuja kupewa vyeo?

Toka lini majambazi yaliyookotwa mtaani yalipewa nafasi za ukuu wa wilaya na mikoa kwa mwavuli wa CCM?
 
Ila tatizo alisema mwenyewe kuwa raisi hakosei. Na pia tatizo kubwa zaidi ni makosa haya yamekua kwenye hotuba zote.
Mfano akiwa kwenye mkutano wa COP26 alisema geothermal ni moja ya chanzo Cha nishati nchini, kitu ambacho sio kweli.
Kuna shida kubwa kwa wanaoandika hotuba na wanaompa taarifa, lakini pia yeye anapaswa kuwa fit kujua na kusoma mambo mengi ili fedheha hizi ndogondogo inakua rahisi kuepuka
Atabadilika Chief, kumbuka hajawahi kugombea hii nafasi
 
Mjomba! Una umri gan? Binafsi nilimchagua Magufuli 2015 sio sababu ya chama ila trust juu yake! CCM 2015 ilikuwa inapumulia machine.
CCM haijawahi kupumulia mashine, Ni vile Kikwete alikuwa mjinga sana ikaonekana chama chote ni cha wajinga
 
Dah...Kwaheri CCM, ...ndo basi tena.
Magu alikirusha Kwenye Reli baada ya Mkwere Kukiherereza...! Ilifika mahala Ukivaa Sare Ya CCM Unazomewa..!! Ile Hali naanza Kuiona Soon!!
Kikwete alikuwa dhaifu, hakuna mtu anaweza kuizomea CCM ya Samia
 
acha kumpa sifa asokua nazo huyo bi tozo, huyu maza alimuita nonsense waziri wake hadharani, huyu maza juzi hapa kamjibu ndugai alafu we unasema kampuuza, huyu maza aliudanganya ulimwengu kuhusu mbowe kupitia BBC alafu juzi kwenye mkutano wa siasa anasema mbowe awe na heshima, huyu maza ni katili kama alivyokua mtangulizi wake tu.
 
Imefika mahali kuchagua tuchague mtu, sio chama kama wanavyo tushawishi, kiukweli mtu akichaguliwa anakuwa na nguvu kuliko chama na chama hakiwezi kumdhibiti kamwe.

Kwa roho ya Magu, hatukupaswa kumchagua, sio kumchagua tu akupaswa agombee nafasi ya Urais, kwani akipitishwa tu na CCM, vyombo, taasisi zote zinahakikisha lazima aapishwe!
 
acha kumpa sifa asokua nazo huyo bi tozo, huyu maza alimuita nonsense waziri wake hadharani, huyu maza juzi hapa kamjibu ndugai alafu we unasema kampuuza, huyu maza aliudanganya ulimwengu kuhusu mbowe kupitia BBC alafu juzi kwenye mkutano wa siasa anasema mbowe awe na heshima, huyu maza ni katili kama alivyokua mtangulizi wake tu.
Hama Nchi mwizi wewe
 
Naunga mkono hoja
Hivyo hata hili la milioni na bilioni, ni kosa la kawaida sana tusilifanye nongwa!.

P
Big no hilo ni kosa kubwa sn, hotuba ya Rais inapitia kwenye mikono mingi sn kabla ya kumfikia yeye, tatizo watu wake wameshajua siyo mfuatiliaji wala hafanyi tafiti kabla kujiridhisha na alicholetewa
 
Imefika mahali kuchagua tuchague mtu, sio chama kama wanavyo tushawishi, kiukweli mtu akichaguliwa anakuwa na nguvu kuliko chama na chama hakiwezi kumdhibiti kamwe. Kwa roho ya Magu, hatukupaswa kumchagua, sio kumchagua tu akupaswa agombee nafasi ya Urais, kwani akipitishwa tu na CCM, vyombo, taasisi zote zinahakikisha lazima aapishwe!
Huyo alikuwa ni zaidi ya katili
 
Back
Top Bottom