Rais Samia kafanya alichofanya Mzee Mohammed Kissoky miaka ya 70 Bukoba

Kutoka kwa Nguli la Artifical Intel
Yahya Msangi
Wakati wa zile RTC palitokea uhaba wa bidhaa mbalimbali mkiani Kagera (Bukoba enzi zile). Mkuu wa Mkoa Mzee Kissoky (mungu amrehemu) akaitisha kikao cha kamati ya mgao. Alitaarifiwa na mwenzie wa Mwanza Mzee Al Nur meli iliyobeba mgao wa Bukoba (MV Victoria) imepata hitilafu na lazima baadhi ya bidhaa zitupwe ziwani.

Mzee Mohamed Kissoky ikabidi aitishe kikao ili uamuzi uchukuliwe haraka kunusuru meli, abiria na baadhi ya mgao. Mara tu kikao kuanza ikatoka hoja kuwa unga wa mahindi ambao ulikuwa sehemu kuubwa ya mgao ndio utupwe.

Hoja ikawa kuwa ugali sio chakula muhimu Bukoba. Lakini kipindi hicho njaa ilikuwa kali mno kiasi kwamba watu wengi hawakuchagua chakula! Na kila mtu mkoani alijua njaa ilifanya wahaya, wanyambo, wahangaza na wenzao waache kudharau ugali.

Mtoa hoja akahitimisha hoja kwa kusema kati ya bidhaa ambazo kamwe zisitupwe ni bia na vileo! Kwa mtizamo wake ni kuwa watu wa Bukoba hukosa utulivu na uvumilivu wakikosa Pombe! Éti pombe hutuliza watu kuliko ugali hasa kipindi cha bidhaa adimu.

Aliyetoa wazo lile bado yupo na waliomuunga mkono baadhi wapo wengine weshatangulia mbele ya haki. Sisi wengine pamoja na mzee Kissoky tulipinga

Tukieleza umuhimu wa ugali kipindi cha njaa na uwezekano wa kuja kuibua chupa za pombe baadae kwa kutumia wapigambizi. Kura kupigwa tukashindwa! Ila RC akatumia turufu yake.

Hii inaonyesha jinsi watu wachache wanavyoweza kupotosha umma kwa manufaa yao. Jamaa wale watoa hoja wengi walikuwa wafanyabiashara wa bar! Kuadimika kwa beer kuliwaathiri kiuchumi. Sasa wakageuza hitaji lao kuwa ndio hitaji la wengi

Kisa kile cha Bukoba miaka ya 70 hakina tofauti na suala la Katiba na Tume miaka hii. Wachache wanataka kufanya hitaji lao ndio hitaji la watanzania woote milioni 60

Ningependa kuwapa wapinzani wetu testi ndogo tu hâta wa la 7 kama msukuma atajua majibu:

1. Nani aliwahi kwenda likizo kijijini na zawadi ya katiba? Yaani mamaako akupokee usimpe vitenge, sukari, mafuta au hela umpe nakala ya katiba? Umwambie "Hebu soma uone katiba ilivyo mbaya"?

2. Unadhani mama yako angepokea nini kati ya katiba na kitenge?

3. Ufike kwenu wakuulize vipi maisha ya mjini uwajibu "Tume bado ni ile ile haijabadilika"! Unadhani watakuona una akili? Usiwaambie kuhusu umepata ajira au umejenga nyumba au kama unajua lini serikali itawapatia maji ya bomba uwaambie kuhusu tume?

4. Hayati JPM alikuwa akipita watu wanamueleza shida na mahitaji yao. Ni lini mlisikia hata mtu mmoja akimwambia shida yake au ya kijijini kwao ni katiba na tume mpya?

Wapinzani jikiteni kwenye hoja na mahitaji ya wananchi wapiga kura! Hitaji la tume na katiba mpya ni lenu ninyi wachache mno! Halina tofauti na hitaji la wenye bar enzi zile pale bukoba.

Kama alichofanya Mzee Kissoky kupuuza hoja ya kutuma unga na kuokoa beer ndivyo mama samia kafanya leo bungeni. Katupilia mbali hoja ya katiba na tume! Kajikita kwenye mahitaji ya wengi!

Mama kamatia hapohapo!
Kama sio kimpumu basi atakuwa amekunywa rubisi iliyokojolewa na popo
 
Based on Maslow's theory of hierarchy needs.
Dai la katiba ni ESTEEM stage.hii ni stage ambayo society inakuwa imejitambua zaidi. Kwa hiyo katiba mpya ni dai la jamii nzima.
Jk alitufikisha ESTEEM stage. Alituvusha stage zote za chini almost 60% ya WaTZ.
JPM aliturudisha chini zaidi level ya PHYSIOLOGICAL NEEDS almost 50% ya waTZ.maendeleo ya vitu.
Mama SSH anatupandisha tena level za juu.
PHYSIOLOGICAL NEEDS ndo kuboresha maisha ya wa TZ(kutoa ajira, demokrasia,Uhuru wa vyombo vya habari ETC).Maendeleo ya watu.

ref
images.png
 
Back
Top Bottom