Rais Samia kabla ya kubadili Wakuu wa Mikoa/Wilaya na Wakurugenzi mulika hili chaka

Oct 13, 2018
35
259
Na Thadei Ole Mushi.
_______________________________

January mwaka (2020) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof Palamagamba Kabudi alisema bila juhudi za Rais John Magufuli, fursa za kufundisha lugha ya Kiswahili Afrika Kusini ingetupita… “Fursa hiyo ingepita si kwasababu nyingine yoyote ile, uzembe wetu wenyewe”

Aliyasema haya katika hafla ya kuapishwa kwa mabalozi wapya akiwemo Dkt. Benson Bana. Hii ni fursa Moja kati ya nyingi ambazo taifa hupoteza kutokana na uzembe wetu wenyewe. Anachokiongea Kabudi hapa kinamaanisha (Mabalozi) wetu hawaifanyi kazi yao ipasavyo huko njee ya nchi.

Mwezi wa tano Mwaka huu wakati Rais wetu Dr JPM akiwaapisha kina Moleli Kama Naibu Waziri pale Dodoma alisema kuwa Balozi wa Kenya Nchini amefanya Mambo makubwa Sana. Rais alifikia mahali akachombeza kuwa anatamani angelikuwa Mtanzania ampatie kazi ya kufanya. Hii ni kwasababu alisimamia vizuri Sana maslahi ya Taifa lake kuhusu mgogoro uliotaka kuibuka katika mipaka yetu katika kipindi cha Korona.

HEBU TWENDE SAWA HAPA.

Tuachane na hiyo fursa ya Kiswahili aliyoiokoa Mh Rais kule Africa kusini, mwaka 2018 wakati tunakimbizana na wanajeshi kubeba Korosho kule Mtwara na Lindi kwa kukosa soko, Ghana ilikuwa ishauza njee ya nchi yao Korosho za dola Milioni 455.75 Nigeria ikifuatia kwa kuuza Korosho za Dola milioni 190.97 Senegal ikiwa inafuatia nk, wakati huo tuambie ni Balozi gani aliweza kufanikisha hata dili la dola laki mbili la Korosho?..

Mwaka Jana tulipata shida pia ya soko la Pamba lilikuwa haliendi vizuri. Si kwamba Pamba ilikuwa haiuzwi huko nje, kuna mataifa yaliyoongoza kwa kusafirisha Pamba njee ya mipaka yao na kupata fedha ya maana, mwaka 2019 China, India, Marekani, Italy, Benin, Ivory Coast nk ni mojawapo ya nchi zilizoingiza fedha nyingi kutokana na kusafirisha Pamba.

NATAKA KUSEMA NINI

Wakati mabalozi wa mataifa mengine wakihaha na kukamilisha dili mbalimbali kwa manufaa ya mataifa yao kwa Tanzania mwaka 2019 mabalozi wetu badala ya Ku deal na vitu sensitive vya nchi walikuja nchini kuja kutalii kwenye miradi inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano.

Kuna jambo la kujifunza hapa hasa kwa mabalozi wetu ambao wanatuwakilisha kwenye mataifa mengine. Wanafanya kazi gani huko? Ni dili ngapi nchi yetu inapoteza kwa mabalozi wetu hawa kutokuwa makin? Pamoja na kulinda diplomatic immunity wana majukumu mengine hasa ya kutafuta wawekezeji na fursa kwa watanzania. Wana jukumu pia la kutafuta masoko kwa bidhaa zetu hasa mazao nk.

Tatizo lipo pale pale, tumewapa retired officers kwenda kutuwakilisha kama mabalozi. Kinachotokea wanakuna vipara na matumbo yao tu huko njee na kunywa wisky . Tufike mahali idara zetu ziwapime kwa Impact wanayoiletea nchi si kwa kiingereza wanachokiongea. Hizi balozi ni za kufumua ziendane na mabadiliko ya dunia na hasa ya nchi yetu. Tuna fursa nyingi sana zinatupita...

Kwao Ubalozi ni zawadi si majukumu, ni mahali pa kwenda kumalizia uzee wao nk.

USHAURI.

Ubalozi usiwe tena ni eneo la kuwapa makada wa ccm waliokosa vyeo ndani ya nchi maeneo ya kuongoza. Kama kweli tunataka kukimbia na kasi ya Dunia hapa tuwekeze kwa wataalamu haswa na watu wenye maono. Ni eneo nyeti sana ambalo kama tukilitumia vizuri linaweza kutupandishia thamani mazao yetu haswa. Linaweza Kuongeza Ajira nchini, linaweza kuboost viwanda vyetu Sana.

Eneo hili lisiwe ni la kuwapa watu waliostaafu kwenye majeshi na maeneo mengine. Mtu aliyestaafu akapumzike Labda kama ana kitu cha kipekee sana. Tupeleke watu fresh kabisa kichwani kwenye maeneo haya. Tuwekeze kwenye Ujasusi wa Kiuchumi kwenye hizi ofisi zetu, tupeleke watu wenye uwezo wa kufanya negotiations na kunusa fursa na kuwazidi maarifa mataifa mengine huko njee.

Tuwe na evaluation form kila baada ya mwaka kupima nani ameweza Ku meet mahitaji yetu. Tuwe na vigezo vya upimaji, tunataka balozi afanye nini?

Kama eneo hili litaendeleza utamaduni wa Kale kuhusu kuwapa makada na wastaafu bado tutakuwa na safari ndefu sana.... Ndio maana Kenya aliweza kutupiga hapo S.A.....

Kama mabalozi wetu wakiweza kufanya lobbying tu kwa asilimia 60 hakuna zao ambalo litakosa soko na Bei nzuri.

Ole Mushi
0712702602

FB_IMG_1618415637599.jpg
 
Mkuu umeongea mambo ya msingi sana. Kongole sana.

Niliwahi andika kuhusu "uchama" na "uwenzetu" unavyoua fursa za maendeleo nchini Tanzania.

Kuanzia kwa viongozi wa chini kabisa mpaka wa juu,ni kupeana nafasi kwa namna hiyo.

Mh. Rais SSH tunakuomba uliangalie hili ili kila kiongozi alete tija katika nafasi yake.

Na kuliangalia kwenyewe ni kuacha kuteua kwa "uchama" au "uwenzetu", bali tuteue kwa weledi,utaifa,ubunifu,uthubutu.
 
Viongozi wetu hawawezi kuelewa chochote kuhusu ulioyashauri kamwe!! Wanapofanya teuzi wanayajua sana sema uchama na mwenzetu imeshaiua nchi.

Imagine Dr. Benson Bana aliteuliwa kua balozi...Ernest Mangu aliteuliwa kua Balozi kisa tu atulizwe baada ya kuondolewa U IGP. Modestus Kapilimba.

Bado hatujui watu wa kuwateua kutuwakilisha kwenye sekta nyeti kama ubalozi.

Swali: Je, Said Bakhresa hawezi kuteuliwa kua balozi?
 
Kweli kabisa, mtu akishastaafu ni vema aachwe tu akapumzike kuliko kumpa mzigo mwngne kama huo ambao unahitaji akili iliyochangamka sana
 
Lazima tujue biashara haifanyiki kutegemea ushawishi wa balozi peke yake. Kuna mambo mengi sana yanachangia nchi na nchi kufanya biashara.

Lazima kujiuliza kwa nini kipindi cha JK mazao yetu yalikuwa na masoko na ghafla.

Ni kweli mabalozi wana sehemu yao lakini ukweli ni kuwa sera, diplomasia, kodi, ubora wa mazao, upatikanaji (wingi) na bei vinachangia kwa kiasi kikubwa sana katika biashara.

Kwasasa tujikite kwenye kurekebisha sheria na sera zetu kama Rais alivyoagiza badala ya kuanza kulaumu na kutetea kundi flani ambalo kwa kiasi kikubwa lilichangia kudhorotesha biashara nchini.
 
Hivi kwani hizi nafasi na zingine kama hizi haziwezi kutangazwa watu wakafanya application kama kazi zingine tu. Hata uwaziri, wabunge hawawezi kufanya application ya nafasi hizo na Rais kuangalia vigezo na masharti na appraisal letters.

Maana inawezekana kabisa asilimia kubwa ya hawa watu wanaoteuliwa sio tu hawana uwezo wa kazi hizo bali hata interest na kazi zenyewe hana ni basi tu wanafanya kwa kujilazimisha.
 
Kumbe Dr. Benson Bana ameteuliwa kuwa Balozi! Balozi wa wapi sijui!! Mzee aliutamani sana uteuzi. Ahueni alikumbukwa dakika za majeruhi.
 
Wacha wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wapigwe tochi, unawalinda ili iweje?

Samia akibadili wakuu wa wilaya na Wakurugenzi haizuii kufanya yote hayo uliyoyashauri.

Je, hao wakuu wa wilaya na Wakurugenzi "Makada" wamekutuma uwasemee maana tumbo joto?
 
Back
Top Bottom