Rais Samia: Jengo la Kariakoo kulikuwa na mchanga mwingi kuliko nondo na saruji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,984
13,760
Rais Samia kushiriki chakula cha mchana na walioshiriki zoezi la uokoaji kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo leo Januari 30, 2025.


Kuhusu tukio la ghorofa kuporomoka soma hapa: Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Waziri Mkuu aunda Tume ya watu maalumu 21 - Nov 22, 2024

ALBERT CHALAMILA - MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM

"
Wiki lijalo tutaunda kamati maalum itakayotembelea majengo hasa chakavu ya ndani ya jiji na kuweza kushirikiana na wadau na wamiliki wa majengo hayo kuona namna ambavyo tunaweza kushirikiana kupata private sector wanaoweza ku-develop majengo haya tukapata hoteli, kumbi pamoja na mambo mengineyo ambayo tutapata na maeneo mengine makubwa yatakapokuja"

KASSIM MAJALIWA - WAZIRI MKUU WA TANZANIA

"Mheshimiwa Rais ulinielekeza kuunda kamati maalum ya kufanya uchunguzi wa kuporomoka kwa jengo na kufanya ukaguzi wa kina wa majengo mengine yalioko kwenye eneo la Kariakoo

"Napenda kukufahamisha kuwa kamati hiyo, wajumbe wake wote wako hapa ndani na imehitimisha kazi yake na kwa sasa nakamilisha taratibu za kuiwasilisha kwako nikiwa pamoja na timu nyingine iliyoundwa kwa kadri itakavyokupendeza siku yoyote na wakati wowote tunaomba utupangie muda pamoja na kamati kwa ajili ya kufanya mawasilisho mbele yako

MATHILDA ALOYCE NZELA - MHANGA WA JANGA LA KARIAKOO

"Serikali ilitusaidia sana lakini kwa sabau ni mchanga na nguo zilijaa simenti hatuna nguo tena, hatuna chochote sasa hivi tumepoteza kila kitu watoto wako.

Kama mama kwa niaba ya wafanyabiashara wa jengo lililodondoka Kariakoo, tunahitaji msaada wako. Mungu akuguse ututazame hatuna chochote, tumepoteza mitaji, tumepoteza familia, tunaishi kama ombaomba tunaomba utkumbuke"

SAMIA SULUHU HASSAN - RAIS WA TANZANIA

"Jengine ambalo tumepata somo hapa ni usimamizi wa serikali wakati wa ujenzi na kuhakikisha viwango vya ujenzi vinafuatwa. Kwa wake waliloliona jengo ulikuwa unaona kabisa ni mchanga mwingi kuliko nondo na saruji kwenye lile jengo

"Dar es Salaam tuna mradi wa DMDP ambao kati ya fedha za DMDP tumejipanga kujenga Soko jingine kubwa na nzuri kama la Kariakoo maeneo ya Jangwani, kwahiyo ni maoni yetu kwamba baadhi ya Wafanyabishara, Wanangu Wamachinga tutawahamisha tuwapeleke kwenye Soko lile la Jangwani na wakafanye biashara zao kwa nafasi"
 
Mimi si shabiki wa Samia, but this is a good gesture.

It is still just a gesture.

Hatuoni mabadiliko ya kimsingi kuzuia jengo lingine lisianguke.
 
Rais Samia kushiriki chakula cha mchana na walioshiriki zoezi la uokoaji kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo leo Januari 30, 2025.


Kuhusu tukio la ghorofa kuporomoka soma hapa: Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Waziri Mkuu aunda Tume ya watu maalumu 21 - Nov 22, 2024



Hii pesa iliyotumika kwa hicho chakula wangeoreshea miundombinu ya uokoaji kwenye majanga au iongeze vifaa tiba kwa wajawazito wasifukuziwe kwa waume zao wakazalishwe kwa visu na mikasi.
 
Matatizo katika jamii ni fursa ya kutafuta kiki kwa wanasiasa. Ni kwa nini hizo pesa za kununulia hicho chakula kwa watu wote hao zisingetumika kununulia gloves kwenye hospitali za umma kwa ajili ya akina mama kujifungulia badala yake mkuu wa mkoa Chalamila anamwambia yule mama kama hana pesa ya kununulia gloves arudi nyumbani mumewe akamsaidie kujifungua.:mad:
 
Back
Top Bottom