Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,498
- 9,279
Ni ukweli usiopingika, mchango wa mwanamke una nafasi muhimu katika uchumi, siasa, na mustakabali wa Taifa ukizingatia nafasi ya ulezi na ujenzi wa uchumi, inapotokea mwanamke ananyanyaswa ni wazi mfumo wake wa uwakilishi unaingia dosari - Samia
Ziangalieni familia zenye mizozo ambako wanawake wanafanyiwa sivyo, family inakuwa haiko 'stable' na hata makuzi ya watoto yanaathirika
Hata sehemu za kazi unaweza kumuona mwanamke mwenzio kaingia kazini asubuhi uso haukunjuki vizuri ukimuambia moja anakujibu tatu ukimuita chemba ukimuuliza tatizo limetoka nyumbani, kwahiyo unayanyaswaji unafanya wanawake wasi-perform vizuri
Afadhali wanaume akikereka huko ana njia zingine za kupita akafurahi na akarudi kazini ametulia, lakini sisi hatuna, ni nyumbani kazini, kazini nyumbani, so handle with care sisi ni assets muhimu
Endapo sisi kama jamii tutafanikiwa kubadili mazoea na firka potofu ama zilizopitwa na wakati naamini kwa kiasi kikubwa tutatokomeza mila na desturi kandamizi kwa mwanamke na watoto.
Historia inaonesha na kuthibitisha nafasi ya Mwanamke ni kujenga umoja, amani na mshikamano katika jamii. Ikitikoea Mwanamke ametengwa na kunyanyaswa hata ushiriki wake katika hayo utakuwa hafifu na hatimaye kufanya ufanisi wake kupungua.