Rais Samia umekosea tena; haupo kwa ajili ya kuongoza wanawake, bali kuongoza Watanzania wa jinsia zote

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,962
Mama Samia Leo nimeona umekosea tena Jambo ambalo umekuwa ukilikosea toka mwanzo.

Ma Samia wewe ni Rais wa JMT, hivyo jinsia, ukabila, dini au rangi uliyo nayo haina uhusiano na urais wako.

Leo umesisitiza kuwabeba wanawake kwa kuwa hapo zamani wanaume walibebwa Sana kwenye siasa, hivyo sasa hivi ni wakati wa wanawake.

Mama Samia ameenda mbali kwa kusema, wanawake watamchagua Rais mwanamke 2025 na mtarudi tena hapo mlipo leo kupongezana.

Hilo halipo sawa, hutachaguliwa sababu ni mwanamke Bali utachaguliwa sababu ni Rais na kiongozi mzuri.

Haupo kwa ajili ya kuongoza wanawake, Bali upo kwa ajili ya kuongoza jinsia zote.

Hata serikali yote wakijaa wanawake hakuna shida endapo tu Wana uwezo wa kuongoza na sio eti kwa sababu ya kubalance gender.

Mama Samia katika kila hotuba umekuwa ukitoa statement ambazo ni controversial.

Itakuwaje wanaume nao wakakomaa na kusema wanataka kumsimamisha Rais mwanaume?

Una muda wa kurekebisha hayo
 
Back
Top Bottom