Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,702
- 71,013
Kama mbunge halali analipwa zaidi ya shilingi milioni 13.8 kwa mwezi basi wale wabunge 19 wa Ndugai ambao hawana chama chochote kilicho waidhinisha kuingia bungeni bali kwa ubabe na kiburi cha Ndugai huku akilindwa na marehemu Magufuli watakuwa wanalipwa takribani bilioni 3.4 kwa mwaka bila kuhesabu posho za vikao.
Pesa hizo za umma ni wizi mkubwa wa wazi kabisa ila wenye baraka za bunge na rais aliyepita. Je, nawe una bariki wizi kama huo? Au Utaufumbia macho kwa vile hao ni wabunge wanawake na kinachofanyika ni kuikomoa Chadema?
Angalia usiingie kwenye kapu la lawama kama za mtangulizi wako aliyekuwa na kiburi cha uzima.
Wizi huu unatofauti gani na watumishi hewa? Nguvu ya kukemea mengine utaipata wapi kama mengine utayafunika wakati kila mwenye akili anayaona?
Wewe sio yule!