Rais Samia hongera sana kwa kuruhusu bidhaa za Kenya kuanza kuingia Tanzania

dev senior

JF-Expert Member
Aug 12, 2012
402
500
Unajaribu kumuelekeza lakini kagoma kuelewa. Maamuzi ya mama kwenye baadhi ya mambo yanatupeleka shimoni. Viwanda vya TZ ni dhaifu ni lazima tuvilinde
 
Blac kid

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
6,370
2,000
Ni kama tumekalilishwa na 'industrial model' kama ndo development strategy yetu pekee. hii model ya viwanda ilishashidikana kwa miaka 60 sasa, tukubaliane na 'comparative advantage' stýle kwetu na kwa majilani wetu.

protectionism ijazaa matunda, kwanini tusiwekeze kwenye kilimo na ufugaji ambako tuna advantage kubwa kuliko Kenya na nchi jirani sio lazima tuendelee kwa kupitia viwanda or industrial model. Agricultural madel itatufa sanaa tutegeneze green zone ya kilimo cha export.

na tulime kwa kimkakati (market focused) kwanini mahidi, mbaazi maharage tu, wakati karrati vitugu swaumu tangawizi pilipili huleta more foreign exchange kuliko mahindi.

Nchi kama Brazil Denmark Colombia Portugal hawana viwanda ila nitajiri tuache kukalilishwa tupanue mawazo yetu. Naona mama kasha ona hilo na sio mhafidhina kama mtangulizi wake. Big up SSH.
Ni kweli mkuu tusiishi kwa mazoea, ngoja tuendelee kuwaelimisha watz wenzetu wafute fikra mfu vichwani mwao.
 
Blac kid

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
6,370
2,000
Unajaribu kumuelekeza lakini kagoma kuelewa. Maamuzi ya mama kwenye baadhi ya mambo yanatupeleka shimoni. Viwanda vya TZ ni dhaifu ni lazima tuvilinde
Tuvilinde mpaka lini babu? Tumevilinda kwa miaka 60 lkn havikui, je tuendelee kuwapa mamilioni ya wananchi bidhaa duni miaka elf10 kisa kulinda ajira elf10?
 
dev senior

JF-Expert Member
Aug 12, 2012
402
500
Brazil hakuna viwanda??? Hizi data umetoa wapi. Manufacturing sector ya Brazil ni ya tatu kwa ubora kwa upande wa amerika, wapo nyuma ya USA na Canada
 
Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
9,100
2,000
mibidhaa feki ya China imetapakaa mtaani tena kwa bei ghali, ajabu wabongo mnalazimisha serikali imkazie Kenya kwa vijisababu uchwara.
Baadhi ya Watanzania mko so obsessed na Wachina mtu unaweza kufikiri labda tuliwahi kutawaliwa na Wachina!!
 
Bunsen Burner

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
613
1,000
China hakuna duty free na Tz, bidhaa za China zinaingia kwa kodi Tz, sasa kwa nini unataka bidhaa za Kenya ziingie Tz bila kodi? Narudia ni Rais mjinga tu anayekubali kuua manufacturing industry ya nchi yake ili aweze kuuza mahindi Kenya.

Kuruhusu bidhaa kuingia hovyo Tz ndio changamoto ya wafanyabiashara au watanzania, kwa kuruhusu hivi ameua ajira ngapi za viwandani Tz, SSH ni Rais wa watanzania sio Kenya, atulize akili aache kukurupuka kukubali tu ovyo ovyo chochote anacho ombwa na hao wakenya.
Wewe Tz, si na wewe uuze basi finished products ulizonazoKenyq kwani umekatazwa?? Tatizo labda bidhaa zako najua hazitapata soko au kuweza kushindana kwa kuwa substandards... ...sasa kwa changamoto hiyo, basi kwa nini ndo isiwe chachu ikufanye uweze kuimprove hizo final products zako ili kuweza shindana na kuingia ktk soko la kimataifa.... jamani dunia sasa imekuwa 'global village'... hakuna namna na tumechelewa sana. Kazi iendelee.
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
57,606
2,000
Naunga mkono hoja
Bidhaa za ndani nyingi magumashi
Kwenye ubora
Hizo juice,maziwa nk tunazouziwa humu ubora uko chini kabisa

Ova
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
57,606
2,000
Wewe Tz, si na wewe uuze basi finished products ulizonazoKenyq kwani umekatazwa?? Tatizo labda bidhaa zako najua hazitapata soko au kuweza kushindana kwa kuwa substandards... ...sasa kwa changamoto hiyo, basi kwa nini ndo isiwe chachu ikufanye uweze kuimprove hizo final products zako ili kuweza shindana na kuingia ktk soko la kimataifa.... jamani dunia sasa imekuwa 'global village'... hakuna namna na tumechelewa sana. Kazi iendelee.
Wapeleke a.energy au m.energy huko wakauze

Ova
 
Lob

JF-Expert Member
Jul 24, 2017
803
1,000
Mama Samia popote ulipo nakupa hongera Sana kwa hatua hii uliyofikia.

Mimi naweza kuwa tofauti na wengine kwenye kuliangalia hili suala. Bidhaa nyingi za ndani hazina ubora kabisa hivyo kuanza kuruhusu bidhaa za Kenya kuanza kuingia ni hatua kubwa na ambayo itawaamsha usingizini wafanyabiashara wa bongo kuanza kutengeneza bidhaa kwa ubora mkubwa sana.

Mfano hadi Sasa bidhaa kama juices, unga wa ngano n.k zimesharuhusiwa kuingia Tena bila inspection fee, maana yake ni kuwa hivyo vitu huku tutavipata kwa Bei ndogo na hivyo kufanya bidhaa zinazozalishwa nchini nazo kupungua Bei na hatimaye kupunguza inflation.

Hii ni hatua nzuri Sana Mama Samia, wenye viwanda ni wakati wao Sasa wa kunoa vichwa na kutengeneza bidhaa Bora ili kupambana na hizo za wakenya.

Hii ni survival of the fittest, wataoweza kupambana na bidhaa za Kenya wapambane na wataoshindwa basi ruksa kufunga hivyo viwanda.

Miaka mingi tumelia ubora wa bidhaa za ndani , Sasa Mama kaja kafungua nchi hivyo hii ichukuliwe Kama challenge kwenye nyie wenye viwanda ambao mlikuwa mnazalisha juice zisizo na ubora au mnazalisha unga kwa bei kubwa.

Kongole Mama Samia, kazi iendelee.

Mama ana akili Kubwa baada ya 2030 nchi itakua ya kwanza kwa maendeleo Africa, aendelee kujenga team ya kumshauri na kusimamia utendaji achukue wataalamu kutoka Nje hasa singapore na USA watamsaidia sana.
 
Lob

JF-Expert Member
Jul 24, 2017
803
1,000
sabuni ya jamaa gani? kiufupi, viwanda vingi vya kenya vinamilikiwa na wazungu ambao wanatengeneza bidhaa zenye ubora. havimilikiwi na wahindi kama hapa bongo. fungulia tu milango ili tufanye biashara na ndio tutajifunza ushindani.
Uko sahihi, ushindani ndio utatupa maendeleo, wamejifungia miaka 60 na bado masikini
 
Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
1,663
2,000
Faida ni kubwa kuliko hasara, faida kuu mojawapo ni tunaenda kumpa mwananchi bidhaa bora na kwa bei nafuu, hasara kuu ni viwanda legelege vinaenda kufa hivyo kutishia ajira kadhaaa za wananzengo, hii nimeongea kwa ufupi zaidi.
una hoja ya kijinga sana mkuu, sisi tunawauzia raw materials alafu wao wanatuuzia finished products.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
13,359
2,000
Mama Samia popote ulipo nakupa hongera Sana kwa hatua hii uliyofikia.

Mimi naweza kuwa tofauti na wengine kwenye kuliangalia hili suala. Bidhaa nyingi za ndani hazina ubora kabisa hivyo kuanza kuruhusu bidhaa za Kenya kuanza kuingia ni hatua kubwa na ambayo itawaamsha usingizini wafanyabiashara wa bongo kuanza kutengeneza bidhaa kwa ubora mkubwa sana.

Mfano hadi Sasa bidhaa kama juices, unga wa ngano n.k zimesharuhusiwa kuingia Tena bila inspection fee, maana yake ni kuwa hivyo vitu huku tutavipata kwa Bei ndogo na hivyo kufanya bidhaa zinazozalishwa nchini nazo kupungua Bei na hatimaye kupunguza inflation.

Hii ni hatua nzuri Sana Mama Samia, wenye viwanda ni wakati wao Sasa wa kunoa vichwa na kutengeneza bidhaa Bora ili kupambana na hizo za wakenya.

Hii ni survival of the fittest, wataoweza kupambana na bidhaa za Kenya wapambane na wataoshindwa basi ruksa kufunga hivyo viwanda.

Miaka mingi tumelia ubora wa bidhaa za ndani , Sasa Mama kaja kafungua nchi hivyo hii ichukuliwe Kama challenge kwenye nyie wenye viwanda ambao mlikuwa mnazalisha juice zisizo na ubora au mnazalisha unga kwa bei kubwa.

Kongole Mama Samia, kazi iendelee.

Mama si malaika. Yapo yake ya fyongo na mengi ya kheri.

Kujipambanua kwake kutokea kwa mwendazake mama katukosha sana!
 
Micho

JF-Expert Member
Apr 12, 2009
309
250
sioni kama ni shida kwasabaabu ata sisi tutauza bidhaa za aina hiyohiyo kwao.
Bei ndugu..bidhaa zetu ziko juu na ubora bado kidogo..Kenya watazalisha zaidi kuliko sisi...kwahio uchumi wao utakuwa kwa kasi zaidi wakati sisi tunajikongoja...tulianza kupiga hatua ila na wasiwasi tunarudi nyuma...unless vinavyokuja kwetu vipigwe kodi kubwa kuprotect soko la vitu vyetu..

Kwa mfano

Mo alikuwa yuko protected na product zake km margarine yake ilikuwa bei ya chini ila ni ngumu kidogo..na prestige ya Kenya ubora mzuri laini ila bei juu sana..sasa wanavyoruhusiwa bei ya prestige ikiwa sawa au chini kidogo au juu kidogo ya Mo margarine watu watanunua prestige maana ni laini na affordable na bidhaa ya Mo itabaki dukani muda mrefu mwishoe hatazalisha na Kenya watazidi kufyatua na kuuza and they will live happily ever after...

Sasa kuhusu Mo margarine kuuzwa Kenya...kuna shaka kidogo..km hapa Tanzania watu walikuwa wanaichukua sababu mbadala wake ni bei juu...inatakiwa kule Kenya itumike mbinu ya ziada ili itoboe...
 
Blac kid

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
6,370
2,000
una hoja ya kijinga sana mkuu, sisi tunawauzia raw materials alafu wao wanatuuzia finished products.
Mwendakuzimu angemaliza miaka 10 angefanikiwa kutengeneza 90% ya mazezeta nchini, we ukiuza raw material hupati kipato? Kwa akili zako nchi haiwezi kukuza GDP kwa kuuza raw material? Hebu weka facts hapa kilimo na viwanda ni sekta gani imechangia pato kubwa la taifa kuliko nyenzake?
 
chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
1,145
2,000
Bei ndugu..bidhaa zetu ziko juu na ubora bado kidogo..Kenya watazalisha zaidi kuliko sisi...kwahio uchumi wao utakuwa kwa kasi zaidi wakati sisi tunajikongoja...tulianza kupiga hatua ila na wasiwasi tunarudi nyuma...unless vinavyokuja kwetu vipigwe kodi kubwa kuprotect soko la vitu vyetu..

Kwa mfano

Mo alikuwa yuko protected na product zake km margarine yake ilikuwa bei ya chini ila ni ngumu kidogo..na prestige ya Kenya ubora mzuri laini ila bei juu sana..sasa wanavyoruhusiwa bei ya prestige ikiwa sawa au chini kidogo au juu kidogo ya Mo margarine watu watanunua prestige maana ni laini na affordable na bidhaa ya Mo itabaki dukani muda mrefu mwishoe hatazalisha na Kenya watazidi kufyatua na kuuza and they will live happily ever after...

Sasa kuhusu Mo margarine kuuzwa Kenya...kuna shaka kidogo..km hapa Tanzania watu walikuwa wanaichukua sababu mbadala wake ni bei juu...inatakiwa kule Kenya itumike mbinu ya ziada ili itoboe...
mimi kama raia wa kawaida nisiyemiliki kiwanda chochote, ninachohitaji maishani mwangu ni maisha rahisi, bidhaa rahisi n .k, ziwe zimetoka kenya, china au kokote nahitaji kurahisishiwa maisha basi. hayo mauchumi sijui manini mtajuana hukohuko.
 
chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
1,145
2,000
Uko sahihi, ushindani ndio utatupa maendeleo, wamejifungia miaka 60 na bado masikini
wamejifungia kina nani? mimi ninayeongea ni mtz, na unatutukana kwamba sisi ni masikini. binafsi ni middle class na nina maisha mazuri kulikwa asilimia kubwa sana ya Wakenya, hivyo usiseme tz masikini, sema africa yote ikijumuisha na nchi yako ya kenya ni masikini wa kutupwa.
 
Lob

JF-Expert Member
Jul 24, 2017
803
1,000
Una maisha mazuri ukilinganisha na ya nani? unaweza ukaishi na familia yako muda gani bila kufanya kazi/biashara, Kipato chako kwa Mwaka ni kiasi gani?
 
Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
1,663
2,000
Mwendakuzimu angemaliza miaka 10 angefanikiwa kutengeneza 90% ya mazezeta nchini, we ukiuza raw material hupati kipato? Kwa akili zako nchi haiwezi kukuza GDP kwa kuuza raw material? Hebu weka facts hapa kilimo na viwanda ni sekta gani imechangia pato kubwa la taifa kuliko nyenzake?
akili yako ndogo mkuu, wala hupaswi kuzozana na mimi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom