Rais Samia hongera sana kwa kuruhusu bidhaa za Kenya kuanza kuingia Tanzania

Ninacho jua mimi kila nchi ina sera ya kulinda soko la ndani, kiasi fulani ina achia bidhaa za nje kiasi flani una linda soko la ndani, Sasa wacha mama afungue bila mipango dhabiti baada ya 2 years viwanda vyote vitakufa na ajira zitakufa then tutakua soko la nchi jiran, hata ulaya hawa soko lisolo na kikomo kama mama yenu anavyotaka
Ajira zenyewe ziko wapi za kusem zitakufa?
 
..Mahindi.

..Tanzania ina-supply kiasi kidogo sana cha mahindi ambayo K inaagiza toka nje.

..wakulima wa mahindi wa Tanzania wanatakiwa waongeze uzalishaji kwasababu kuna mahitaji makubwa Kenya.
Sio hizo..nataka jua bidhaa zetu zilizoongezwa thamani kule tunauza zaidi kama nini?
 
Manufacturing industry ya tz ipo nyuma tunakubali, imelindwa takribani miaka 60 lkn haikui, je tuilinde mpaka lini? Goals na strategies za kukuza industry tz tangia Uhuru zipo ktk mfumo wa short, medium na long plan lkn tafiti zinaonyesha hatujafanikiwa walau hata kwa 30% kulinganisha na kenya , je tuendelee mpaka lini kuwa watu wa plan hewa?
You can not plan business growth with policy uncertainty,policies should be competitively and harmonized
 
Sio hizo..nataka jua bidhaa zetu zilizoongezwa thamani kule tunauza zaidi kama nini?
Mzee mjinga huyo, anakuambia watz tutauza mahindi, mahaba yake ya siasa yameshampa upofu. Kuilinda manufacturing industry ya Tz ni jukuma la serikali, unavyoiletea ushindani wakati bado haijasimama sawa maana yake unataka kuiua. Tayari tuna soko kubwa la SADC , kwa nini ulete ushindani usio na afya ili kuwafurahisha tu wakenya.

Kwa akili hizi hizi basi aruhusu na watanzania bara wakamiliki ardhi Zenji, tuone kama after 5 yrs wazenji watakuwa na ardhi, tuna kiongozi vision less na hopeless kabisa.
 
Ardhi ya Zenji na yenyewe iachwe wazi tuone huo ushindani anaotaka kuipa manufacturing industry ya Tz , tuwape pia ndugu zake wazenji halafu tuone in 10 yrs kama watakuwa na ardhi kiasi gani .
 
Aondoe na ushuru kwenye bidhaa za maziwa kutoka nje ili wenye viwanda vya maziwa wakina ASAS, na wewnzie.....wajute na wakipate cha mtema kuni...... maana hawa wenye viwanda vya maziwa walikuwa ni mawakala wa mwendazake wametuchelewesha sana
Nyie ndo mnaulizia wenzenu wamechaguliwa kwenda form five kwenda wapi
 
Kwani tanzania hakuna viwanda vya juice na ngano vinavyoweza kuuza Kenya? Acheni hizo sera zenu za kizamani!

Sasa akina AZAM wataweza na wao kuuza juice zao na ngano Kenya. Bidhaa za AZAM zina ubora wa kushindana na kuzidi hata za Kenya.
nani kakwambia walikuwa hawauzi? nani kakwambia kenya walikuwa hawaleti? nikwambie tuu ili kulinda viwanda vya ndani hasa kwa bidhaa zinazo zalishwa nchini hasa juice, ngano maziwa n.k

Serikali iliweka ongezeko la ushuru kwa bidhaa zote kutoka nje sio kutoka kenya tuuu.... kwahiyo ni bidhaa za mataifa yote... pamoja na hayo bado kenya wameendelea kuuza bidhaa nyingi.

Lakini kwa upande mwingine viwanda vyetu vya juice, maziwa na ngano nchini vimechangamka sana na vimefanya sana biashara.
Lakini kama Samia ameona ni ruksa tuuu kuingiza bila sharti basi lakini ukweli ni kwamba wenye viwanda wataisoma namba
 
mibidhaa feki ya China imetapakaa mtaani tena kwa bei ghali, ajabu wabongo mnalazimisha serikali imkazie Kenya kwa vijisababu uchwara.
Yaani hawa jamaa wamezoea kutulazimisha kununua bidhaa feki nchini zikiwa substandards , tena kwa bei ya juu wakijua hatuna namna... wacha wafundishwe kuwa siku zote ' mteja ni mfalme' na mteja mwisho wa siku utafuta value for money.....
 
nani kakwambia walikuwa hawauzi? nani kakwambia kenya walikuwa hawaleti? nikwambie tuu ili kulinda viwanda vya ndani hasa kwa bidhaa zinazo zalishwa nchini hasa juice,ngano maziwa n.k...
Mkuu wataisoma namba kivipi? This is fear of unknown. Umekiri kuwa tz tunauza Kenya na Kenya wanauza tz, ila bidhaa zinatozwa Kodi pande zote. Swali kama kutakuwa na free duty pande zote kipi kitaifanya tz ishindwe kuendelea kuuza Kenya kama iliweza kuuza wakati wa Kodi?
 
Mzee mjinga huyo, anakuambia watz tutauza mahindi, mahaba yake ya siasa yameshampa upofu. Kuilinda manufacturing industry ya Tz ni jukuma la serikali, unavyoiletea ushindani wakati bado haijasimama sawa maana yake unataka kuiua. Tayari tuna soko kubwa la SADC , kwa nini ulete ushindani usio na afya ili kuwafurahisha tu wakenya.

Kwa akili hizi hizi basi aruhusu na watanzania bara wakamiliki ardhi Zenji, tuone kama after 5 yrs wazenji watakuwa na ardhi, tuna kiongozi vision less na hopeless kabisa.
We jamaa ni primitive Sana sekta ya kilimo inayotoa 70% ya ajira unaidharau, umekomaa na sekta ya viwanda ambayo imechangia % ndogo ya ajira nchini, kwani tukikaza na agricultural products hatutengenezi ajira? Kwani tukikomaa na kuuza bidhaa za mashambani hatutengenezi pato la nchi? Watz tumelogwa na nani? Wacha hizo bidhaa za Kenya zije ili viwanda vya tz wapanue akili za ubunifu.
 
Mkate wa Kenya ukiutafuna mh! yam yam....hadi unajiukiza ngano yao ya Islael au wapi, sabuni protex ukiogea, juisi ya matunda ndio usiseme, kalamu ya BIC unaandika kwa raha, dawa ya viatu KIWI nimetumia nikiwa mtoto hadi nazeeka sasa haijwahi kuwa na mpinzani, sabuni ya unga ukmuagiza mtoto dukani anasema Mangi nipe OMO, ! Kenya nyie!!!....
Watanzania kuna kitu tusipokubali kusema tutakuwa watumwa hadi kizasi cha 17, tumeendekeza KUBEBWA, yanateuana eti kisa baba yake alikuwa RAS zamani, kisa ni wa dini yetu,
 
Mzee mjinga huyo, anakuambia watz tutauza mahindi, mahaba yake ya siasa yameshampa upofu. Kuilinda manufacturing industry ya Tz ni jukuma la serikali, unavyoiletea ushindani wakati bado haijasimama sawa maana yake unataka kuiua. Tayari tuna soko kubwa la SADC , kwa nini ulete ushindani usio na afya ili kuwafurahisha tu wakenya.

Kwa akili hizi hizi basi aruhusu na watanzania bara wakamiliki ardhi Zenji, tuone kama after 5 yrs wazenji watakuwa na ardhi, tuna kiongozi vision less na hopeless kabisa.
Kilimo ndo kimetoa ajira nyingi nchini kuliko kitu chochote,so kama masoko yapo ya uhakika hii ni biashara nzuri..au watu wakiuza mazao hawapati fedha na kuboresha hali zao za maisha?..unakalia kulilia vitu vidogo vya sijui ajira viwandani..ajira hizo ni kiasi gani?

Unawaza kama mtoto wa chekechea.

Bidhaa bora zije hawa wahindi wetu wapate changamoto ya kutengeneza vitu bora ambavyo pia ni free kuuza Kenya..Yes,competition..huku kubebana sana kuna lemaza
 
Upuuzi mtupu, hata USA haikubali bidhaa zote kutoka China na Ulaya, ni jukumu la serikali kulinda viwanda na ajira za watz, SSH hajitambui wala hajui anachotaka hasa ni nini ? Yaani sisi tunapeleke mahindi Kenya halafu wao wanaleta finished products na anachekelea.
1989....
Hakuna aliyesema kuwa tutakubali kila kitu hata sumu kutoka kenya.

Hakuna aliyekukataza usipeleke finished products Kenya kama unazo huko kenya.

Dunia inaenda kuwa kijiji. Hatuwezi jifungia ndani tukiogopa ushindani.
 
China hakuna duty free na Tz, bidhaa za China zinaingia kwa kodi Tz, sasa kwa nini unataka bidhaa za Kenya ziingie Tz bila kodi? Narudia ni Rais mjinga tu anayekubali kuua manufacturing industry ya nchi yake ili aweze kuuza mahindi Kenya.

Kuruhusu bidhaa kuingia hovyo Tz ndio changamoto ya wafanyabiashara au watanzania, kwa kuruhusu hivi ameua ajira ngapi za viwandani Tz, SSH ni Rais wa watanzania sio Kenya, atulize akili aache kukurupuka kukubali tu ovyo ovyo chochote anacho ombwa na hao wakenya.
Kwani huwa ukienda kununua blue band ya kenya dukani unapewa bure? Hivyo vitu tutavinunua dukani na maduka yatalipa kodi maana serikali haitaleta vitu kutoka kenya na kugawa majumbani kwetu bure, maisha yapo juu sana tunahitaji bidhaa zipungue bei Ili watu wengi wamudu kununua.
 
We jamaa ni primitive Sana sekta ya kilimo inayotoa 70% ya ajira unaidharau, umekomaa na sekta ya viwanda ambayo imechangia % ndogo ya ajira nchini, kwani tukikaza na agricultural products hatutengenezi ajira? Kwani tukikomaa na kuuza bidhaa za mashambani hatutengenezi pato la nchi? Watz tumelogwa na nani? Wacha hizo bidhaa za Kenya zije ili viwanda vya tz wapanue akili za ubunifu.
Ni kama tumekalilishwa na 'industrial model' kama ndo development strategy yetu pekee. hii model ya viwanda ilishashidikana kwa miaka 60 sasa, tukubaliane na 'comparative advantage' stýle kwetu na kwa majilani wetu.

protectionism ijazaa matunda, kwanini tusiwekeze kwenye kilimo na ufugaji ambako tuna advantage kubwa kuliko Kenya na nchi jirani sio lazima tuendelee kwa kupitia viwanda or industrial model. Agricultural madel itatufa sanaa tutegeneze green zone ya kilimo cha export.

na tulime kwa kimkakati (market focused) kwanini mahidi, mbaazi maharage tu, wakati karrati vitugu swaumu tangawizi pilipili huleta more foreign exchange kuliko mahindi.

Nchi kama Brazil Denmark Colombia Portugal hawana viwanda ila nitajiri tuache kukalilishwa tupanue mawazo yetu. Naona mama kasha ona hilo na sio mhafidhina kama mtangulizi wake. Big up SSH.
 
Wakenya walianza zamani kuleta bidhaa zao tena wakati sisi bado tumelala fofofo.

Miaka ya sabini zilikuwa zunakuja gari zao zenye bidhaa kila aina na pia madawa ya binadamu.

Walikuwa wanazunguka nchi nzima wakisambaza bidhaa zao

Kweli nimekumbuka mbali sana.

Kila jioni wanaonyesha sinema baada ya kukusanya hela siku nzima

Kama karuhusu ni mwendelezo tu
Wakati wa Jumuia ya Afrika Mashariki iliyovunjwa na Wanasiasa
 
Back
Top Bottom