Rais Samia, hongera kwa uenyekiti CCM. Tafadhali funga mipaka na India

kerubi afunikaye

JF-Expert Member
May 20, 2013
1,183
1,057
Nafahamu Rais wetu uko busy Dodoma na masuala ya kichama.

Hongera kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM.

Sitaki kuingia sana huko na sina maneno mengi kuhusu siasa.

Nakuomba ufunge mipaka kati ya Tanzania na India kwa muda hadi pale hali ya corona itakapotulia kule kwa wenzetu.

Wanatia huruma sana na kila nchi inahangaika ili linalotokea India lisitokee kwake,na Tanzania si exception.

Tuna mwingiliano mkubwa na India, hivyo ni muhimu tuchukue tahadhari kubwa sana.

Akili za kiasili zinaniambia hatutaweza kuhimili third wave katika nchi yetu. Hivyo naomba sana serikali yetu itumie njia madhubuti kuzuia maambukizi kama yale.

Huyu mdudu anazidi kufanya mutation na kila anavyobadilika ndivyo anavyozidi kuifungua kinga ya miili yetu,hivyo tusitambe sana kwamba tuna kinga nzuri maana hatujui kwa undani nini kinaendelea kuhusu covid 19 virus na mutation gani itakuja kuwa janga letu.

Kwa sababu mimi ni muumini wa wale wasiotaka kurukia masuala ya chanjo kwa haraka(tujipe muda wa kutosha kujirishisha),hivyo naomba sana tujitahidi kudhibiti mipaka yetu na taratibu nyingine za kujikinga ndani ya jamii ziwe enforced kwa nguvu kubwa ili tuwe salama kuanzia sasa hadi pale tutakapojiridhisha kuhusu chanjo.

Ni hayo tu.
 
Maza ana mambo mengi ya msingi ya kufanya, hawezi kuanza kuhangaika na vijimafua visivyoweza kuua hata kifaranga cha kuku.
 
Nafahamu Rais wetu uko busy Dodoma na masuala ya kichama.

Hongera kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa ccm.

Sitaki kuingia sana huko na sina maneno mengi kuhusu siasa.

Nakuomba ufunge mipaka kati ya Tanzania na India kwa muda hadi pale hali ya corona itakapotulia kule kwa wenzetu.

Wanatia huruma sana na kila nchi inahangaika ili linalotokea India lisitokee kwake,na Tanzania si exception.

Tuna mwingiliano mkubwa na India,hivyo ni muhimu tuchukue tahadhari kubwa sana.

Akili za kiasili zinaniambia hatutaweza kuhimili third wave katika nchi yetu,hivyo naomba sana serikali yetu itumie njia madhubuti kuzuia maambukizi kama yale.

Huyu mdudu anazidi kufanya mutation na kila anavyobadilika ndivyo anavyozidi kuifungua kinga ya miili yetu,hivyo tusitambe sana kwamba tuna kinga nzuri maana hatujui kwa undani nini kinaendelea kuhusu covid 19 virus na mutation gani itakuja kuwa janga letu.

Kwa sababu mimi ni muumini wa wale wasiotaka kurukia masuala ya chanjo kwa haraka(tujipe muda wa kutosha kujirishisha),hivyo naomba sana tujitahidi kudhibiti mipaka yetu na taratibu nyingine za kujikinga ndani ya jamii ziwe enforced kwa nguvu kubwa ili tuwe salama kuanzia sasa hadi pale tutakapojiridhisha kuhusu chanjo.
Ni hayo tu.

E0NhMwdXIAAW0HL (1).jpeg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom